Jumatano, 14 Agosti 2013

VIJANA ZAIDI YA MIA MOJA WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UJAMBAZI JIJINI BUJUMBURA


Jeshi la polisi nchini Burundi, limewatia nguvuni genge la vijana zaidi ya mia moja wa kiume akiwemo msichana mmoja kwa tuhuma za kujihusisha na wizi ujambazi na uporaji wa mali ya raia wa maeneo ya mitaa ya Bwiza, Jabe, Nyakabiga, Mutanga na ambao wamekuwa wakijificha katika mto Ntahangwa.

Kundi la vijana waliokamatwa na polisi
Katika siku zote hizi za nyuma wananchi wakaazi wa tarafa za Mutanga, Jabe, Nyakabiga na Kigobe wanalalama kukithiri kwa wizi hususan katika barabara ya Imprimerie kuanzia kwenye daraja la mto Ntahangwa eneo la kaskazini barabara ya Novemba 28 hadi kwenye daraja la mto huo eneo la kati la barabara iliobatizwa Peuple Murundi.

Katika miaka ya nyuma eneo hilo lilikuwa likitumiwa na majambazi ambao walikuwa wakiendesha wizi katika mita mbalimbali ya manispaa ya jiji la Bujumbura kwa kutumia jiwe lililoitwa Katarina na kujificha katika eneo hilo na kuitwa Avenue de la Mort kufuatia vile lilikuwa eneo hatari. Wakati huo wa uongozi wa rais Bagaza alitangaza adhabu ya kunyongwa kwa wa Katarina na wa fatuma wote na hivo kukomesha vitendo hivyo.

Hivi karibuni msanii mwenye jina jijini Bujumbura Yoya Jamal alianguka kwenye mtengo wa majambazi hao waliompora kila kitu alichokuwa nacho na kumuacha mtupu huku akiwa hana fahamu baada ya kumjeruhi. Mungu alipita kati alipata wasamaria waliompeleka Hospitalini ili kuokowa maisha yake.

Hatuwa madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa ili kukomesha vitendo hivyo.