Jumatano, 7 Agosti 2013

YOYA JAMAL APONEA CHUPU CHUPU.

Msanii wa kizazi kipya nchini Burundi Yoya, juzi amenusurika baada ya kukabwa na kundi la watu wakati alipokuwa akirejea nyumbani Tarafani Nyakabiga.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumatatu (Lundi) kuamkia Jumanne (Mardi) Usiku wa saa tano, eneo linalo gawa Nyakabiga ya Tatu na Mutanga, pindi kundi la watu walimsimamisha wakati alikuwa ndani ya gari lake na kumpora vitu vyote alivyokuwa navyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msanii mwenyewe”Niliona watu wakanisimisha kama kawaida tu nikasimama, sikujuwa kumbe ni majambazi, wamenipora viato nilivyokuwa nimevaa, saa ya mkononi, simu yangu nzuri niliokuwa nimenunua hivi majuzi aina ya Sunsung Galaxys4, kwenye Wallet(Ngodo) nilikuwa na kiasi cha Franka za Burundi laki moja na elfu arobaini (140.000FBU) ambapo ni hela kidogo sana, inaskitisha

Yoya ameendelea kuwa wakati huo alipigwa na kupoteza fahamu. Wahalifu hao walimtelekeza na kutimka. Baada ya muda ndipo wasamaria wema waliokuwa wakipita katika eneo hilo, wakamuona na kumtambua, ingawaje ilikuwa ni usiku, na kumpeleka moja kwa moja Hospitali .

Yoya anatowa shukrani za dhati kwa watu hao pamoja pia na ma dakari na nesi waliomshukulikia kwenye Hospitali ya Clinique Central de Bujumbura hadi kufikia wakati.

Msanii huyo anaendelea kuuguza majeraha yake akiwa nyumbani baada ya kutibiwa kwenye Hospital hiyo yenye sifa zake jijini Bujumbura.