Raia wawili wa Uingereza
wamemwagiwa tindi kali nchini Tanzania kwenye eneo la mji wa mkongwe visiwani
Zanzibar "Stone Town" na sasa wamesafirishwa hadi jijini Dar es
Salaam Tanzania bara kwa matibabu zaidi, polisi wamesema.
Raia hao wawili wasichana
wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 wanaaminika kuwa walikuwa wakifanya kazi
za kujitolea visiwani humo na kwamba tukio hili ni la kwanza kufanywa kwa raia
wa Kigeni.
Kaimu kamanda wa Polisi
Visiwani Zanzibar, Mkadam Khamis amewaambia waandishi wa habari visiwani humo
kuwa watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki waliwakaribia wasichana hao na kisha
kuwamwagia tindi kali.Wizara ya mambo ya nje ya
Tanzania imekiri kuwa na taarifa hizo na kwamba wanafanya kila linalowezekana
kuhakikisha raia hao wanapatiwa matibabu ya haraka kuwanusuru na madhara zaidi
ya acid hiyo.
Polisi wanasema bado
wanaendelea na uchunguzi na kwamba mpaka sasa watu waliohusika na shambulio
hilo hawajafahamika ila uchunguzi bado unaendelea na kuwaomba wananchi kutoa
ushirikiano kubaini wahusika. Wizara ya mambo ya nje
imesema kuwa zaidi ya raia elfu 75 wa Uingereza ambao huetembeala Tanzania kila
mwaka, hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi yakuwalenga raia wakigeni jambo
ambalo linahatarisha usalama wao.
Wizara hiyo imeongeza kuwa
kumekuwa na matukio ya uporaji wa mizigo ya raia wa kigeni hasa kwenye baadhi
ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine hali ambayo hivi sasa
inaonekana kuota mizizi. Hivi Karibuni watu
wasiofahamika walimwagia tindi kali mufti msaidizi wa Zanzibar pamoja na
kumpiga risasi padri wa kanisa Katoliki