Alhamisi, 10 Oktoba 2013

MTANGAZI BAKARI UBENA AANZISHA KIPINDI "DIAPORA SHOW" BARANI ULAYA

Mtangazi wa zamani wa Radio ya Umma RPA nchini Burundi Bakari Ubena, ambaye kwa sasa anaeshi nchini Ubelgiji, ameanzisha kipindi maalum kupitia runinga, cha "Diaspora Show" ambacho kinatowa nafasi kwa watu mbalimbali kutoka katika ukanda wa Afrika mashariki nakati waishio mbali na Afrika, kujuwa wanafanya nini.

Makala ya kwanza ya kipindi hiki yamemkaribisha msanii wa kizazi kipya nchini Burundi Jay Fernando ambaye anafanya kazi hiyo ya Muziki huko barani Ulaya, chini ya Producer Bahame Newton ambaye pia ni raia wa Burundi anaendesha kazi zake mbalimbali barani Ulaya.


Kwa mujibu wa muhusika mwenyewe, kipindi hicho kitakuwa kikiwapokea watu mbalimbali wakiwemo wasanii, wanamichezo na wanasiasa kuzungumzia mambo mbalimbali. Mbali na watu ambao wanaeshi barani Ulaya Asia, Marekani, wale wanatembelea katika maeneo hayo watapewa fursa ya kushikiri kwenye makala mbalimbali za Diaspora Show.

Makala hizo za Dispora show zitakuwa zikirushwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini Burundi.

Ikoh.biz, hatuna budi kuwatakia kila la kheri, Bakari Ubena na Isac Bahame Newton.