Jumatatu, 5 Agosti 2013

SHAZY KOOL HARERA APEWA SHAVU NCHINI UGANDA

Msanii wa Burundi anaekwenda na miondoko ya kitamaduni zaidi Shazy Kool Harera amepewa mualiko wa kushiriki kwenye Makala ya sita ya  tamasha  la Bayimba International Festival of the Arts, Kampala, Uganda.

Makala haya ya sita ya Tamasha hilo yamepangwa kutimua vumbi September 20 hadi 22 mwaka 2013 kwenye eneo la  Uganda National Cultural Centre jijini Kampala, nchini Uganda.

Shazy Kool pamoja na Bendi yake Ya Vumera Band watadumbwiza katika tamasha hilo litalo yaleta pamoja mataifa kadhaa kutoka katika ukanda wa Afrika.

Mbali na kudumbwiza katika matasha hilo, Shazy atapata furs aya kushirikiana na wasanii wa Uganda katika kufaanikisha tamasha hilo, na kuendesha mahojiano na vyombo vya habari vya nchini Uganda na vya kimataifa.

Akizungumza na Ikoh.biz, Shazy Kool amesema mipango yote imekamilika kuhakikisha wanashiriki katika tamasha hilo. Ametumia fursa hiyo kutowa shukrani za dhati kwa body ya waandalizi wa Makala haya ya sita ya tamasha la Bayumba na Fondation Bayumba. Shukran pia amezipeleka kwa mashabiki ambao wamekuwa kwenye mstari wa mbele katika kumpa sapoti kwenye safari yake hii ya Muziki.

Ikoh.biz hatuna budi kumpongeza Shazy Kool na kumtakia kila la kheri, lakini pia tunamtaka kuitumia vema fursa hii hadimu.