Baada ya kukaa kimya
kwa muda mrefu, hatimaye msanii mkongwe kwenye tasnia ya muziki
wa kizazi kipya nchini Burundi, Nziza Desire ambaye amejichimbia makaazi yake
huko nchini Marekani, amevunja ukimya na kutowa sababu za kutosikika kwa kipindi chote
hiki.
Akichonga na
Ikoh.biz, Nziza Desire amesema : Nipo
katika maandalizi ya Video Clip za album yangu ya UN ambayo ninafanya kila
jitihada kuhakikisha hadi mwishoni mwa mwaka huu zinakuwa tayari. ameendelea kuwa : Kuandaa Video Clip ukiwa
nchi za ng'ambo kama vile USA sio jambo rahisi, linahitaji uwezo mkubwa sana,
sio kama hapo nyumbani, tunatakiwa kutuliza akili fasi moja na kuwa na muda mrefu katika kupanga kila
jambo huku pia tukiendeleza kazi nyingi mbali na muziki, kwakuwa majukumu ya familia yanahitajika zaidi, na ndio maana tunapambana huku na kule.
Katika album yake ya
UN Nziza Desire kuna baadhi ya nyimbo ambazo tayari kisha recordi video na
nyingine bado na sasa ndio shuhguhuli inayo mfanya kuwa kimya.