Kwa
mujibu wa Utafiti ulioendeshwa na kituo cha Marekani cha Burson–Marsteller kuhusu matumizi ya mtandao wa kijamii wa Twitter dhidi ya
viongozi 505 duniani, kwenye gazi ya marais, mawaziri wakuu,
mawaziri wa mambo ya nje, na viongozi wa kidini.
Waziri
mkuu wa Uganda Amama Mbabazi anaongoza duniani kwa kutumia mtandao
huu wa kijamii wa Twitter hasa katika kushiriki mijadala na kutowa
majibu katika mijadala inayotolewa, akifuatiwa na rais wa Rwanda Paul Kagame ambao
wanamzidi mbali rais wa Marekani Barack Obama, licha ya kuwa na
marafiki wanaozidi milioni 34.
Utafiti
huo unaonyesha kuwa, kuongoza na idadi kubwa ya marafiki wengi sana kwenye mtandao huo wa
kijamii wa Twitter sio kuwa na umaarufu, kwani wengi hawana
mawasiliano na marafiki zao kama ilivyo kwa viongozi hao wanaongoza
katika utafiti huu.
Hata
hivyo Utafiti huu umeweka bayana orodha ya marais wa Bara la Afrika walio na
umaharufu mkubwa kwenye mtandao huu wa kijamii wa Twitter, ikiwa ni pmoja na rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akifuatiwa na Uhuru Kenyatta rais wa
Kenya, Moncef Marzouki rais wa Tunisia, Paul Kagame rais wa Rwanda
anachukuwa nafasi ya nne akifuatiwa na Jakaya Mrisho Kikwete rais wa Tanzania kwenye
nafasi ya tano.
Hao
ni viongozi ambao wamejizolea umaarufu mkubwa sana kwenye mtandao huu
wa kijamii wa Twitter.
Ripoti
hii inaonyeshakuwa asilimia 71 ya viongozi wa bara la Afrika wapo
kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, lakini maskitiko ni kwamba
viongozi wengi wamekuwa wakitumia mtandao huu kwa ajili ya kampeni za
uchaguzi na baada ya kuchaguliwa hawaonekani tena.