KWA HALI KAMA HII
TUTAIKUZA VIPI INDUSTRY YA MUZIKI NCHINI BURUNDI ?
Hivi karibuni kiwanda kinacho tengeneza vinywaji cha Brarudi
kiliandaa mashindano yaliobatizwa Primusic ikiwa ni mwaka wa pili tangu pale
mashindano hayo yalipoanza kuandaliwa na kiwanda hicho.
Kila mtu anayo haki ya kuzungumzia mashindano haya kadri
awezavyo. Unaweza kusifu, kukosoa, na mengine mengi, lakini mimi katika makala
haya ninatowa mtazamo wangu ulio hasi kuhusiana na mashindano haya.
Kwanza nianze makala haya na maswali : 1. Mwaka uliopita
kuna msanii aliye shinda mashindano haya bila shaka, je, kuna mabadiliko yoyote
katika maisha yake ya muziki aliyo yapata kupitia ushindi huu ? 2. Katika
mfumo huu Industry ya Muziki nchini Burundi itapiga hatuwa vipi ? 3. Nani anaye
nufaika na mashindano haya ?
Mpenzi msomaji, Kama inavyoeleweka kiwanda cha Brarudi ni
kampuni kubwa nchini na ambayo ndiyo ya kwanza kama sio ya pili katika kulipa
kodi ya serikali, na ambayo imekuwa ikifadhili mambo mbalimbali nchini Burundi,
husuan Ligi kuu ya mpira wa miguu ya Primus.
Katika kila secta ambayo kiwanda hicho kinatowa ufadhili
tunashuhudia kupiga hatuwa na watu wengi hunufaika kwa pamoja, mathalan,
shirika la Mpira wa miguu, vituo mbalimbali vya Radio na TV, vilabu, wachezaji
na watu wa karibu na wachezaji husuan familia.
Nani asiye fahamu kwamba kiwanda kama hicho nchini DRCongo
ndicho kilicho waendeleza wasanii wa nchini humo kama vile akina JB Mpiana,
Werrason, Koffi Olomide na wengine?
Nchini Tanzania jijini Dar es Salaam kampuni ya Serengeti moja
kati ya kampuni zinazo tengeneza bia nchini humo kila mwaka hutowa sponsa kwa
ajili ya maandalizi ya Serengeti fiesta, ambapo wasanii, waandishi wa habari,
madereva, na watu wa kawaida hunifaika kupitia tamasha hili ambalo huandaliwa
kila mwaka.
Si hayo tu, Kampuni ya Kilimanjaro, kila mwaka hutowa tuzo
kwa wasanii kupitia kila categories ya Muziki, na hii inasaidia kuleta
ushindani na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kutaka kupata tuzo.
Kampuni ambayo ilitakiwa kutowa Sponsa kwa kukuza Musiki,
lakini sasa ndio ambayo inaandaa mashindano, tunausapoti muziki vipi katika
njia hii ?
Kama tukiendelea na mfumo huu, sanaa ya Muziki nchini Burundi
bado ipo mbali kabisa, na itakuwa vigumu kupiga hatuwa iwapo hatutoiga mifumo
ya nchi zingine.
Kama jinsi Brarudi inavyodhamini mashindano ya ligi kuu ya
mpira wa miguu nchini Burundi, hivi
ndivyo ilitakiwa kuwa upande wa tasnia ya muziki. Swala la kujiuliza hapa,
hakuna kampuni zenye uwezo wa kuandaa mashindano kama haya na kuyaboresha zaidi
kuliko ilivyo kwa sasa ???
Industry ya Muziki itapiga hatuwa pale, Sponsa itapatikana,
kupitia kampuni andalizi, vyombo vya habari vikinufaika, waandishi wa habari
wakinufaika, wafanyakazi wa kampuni andalizi wakinufaika, wasanii wakinufaika
hadi mpenzi wa muziki na yeye akinufaika hapo ndio tutakuwa tumepiga hatuwa
katika kukuza industry yetu ya Muziki, vinginevyo tutabaki kujisifu tu kila
wakati huku wenzetu wakizidi kusonga mbele.