Jumatatu, 26 Agosti 2013

TAMASHA LA AMANI KUFANYIKA MJINI GOMA MWISHONI MWA MWEZI AGOSTI

Albert Nkulu msanii wa Burundi aliye shiriki katika tamasha la Amani mwaka uliopita

Tamasha la Amani linatarajiwa kuzinduliwa jijini Goma Agosti 30 mwaka huu na kutamatishwa Septemba Mosi, ikiwa ni moa miongoni mwa tamasha lenye lengo la kuwaleta pamoja wasanii kutoka katika mataifa mbalimbali katika hali ya kuhamasisha maridhiano katika ukanda wa maziwa makuu.

Miongoni mwa wasanii wataoshiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Youssoupha, msanii wa Congo anaikipinga nchini Ufaransa, Picha, msanii wa Congo anaye eshi nchini Ubelgiji na Freddy Massamba msanii wa Congo Brazaville anaye eshi nchini Ubelgiji.

Moja miongoni mwa kundi la wasanii wa Goma wakionyesha makeke jukwani

Mbali na wasanii hao watakuwepo pia wasanii wa ukanda wa maziwa makuu hususan Rwanda, Burundi na Uganda pamoja na makundi ya muziki wa jadi ytayo wakilisha makabila yote ya Mkoa wa Kivu ya Kaskazini.

kwa mujibu wa Eric Lamote aliye andaa tamasha hili, lengo hasa ni kutowa wito kwa ulimwengu kwa kuwaleta pamoja watu kutoka katika mataifa mbalimbali ili kukomesha madhila yanayowakumba wananchi wa eneo hilo, aidha kuhusu swala la Usalama amesema majeshi ya Kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini DRCongo Monusco ndiyo yatayo husika na ulinzi wa Usalama.

Kwa wasanii wa kimataifa ambao wangelipenda kushiriki katika tamssha hilo wametolewa wito wa kujitolea bila kujali kupewa malipo.