Klabu ya mpira wa kikapu ya Urunani kutoka
Burundi imefaanikiwa kushinda kombe la michuano ya vilabu kutoka katika nchi za
ukanda wa Afrika Mashariki na kati ama Zone 5, kwa kuilaza Espoir ya Rwanda kwa
vikapu 65 kwa 59.
Halaiki ya wapenzi wa mpira wa kikapu
walimiminika kwa wingi kushuhudia mechi hiyo iliokuwa na mvuto, kwani kila timu
ilionyesha juhudi za kutaka kushinda. Lakini kama mjuavyo, mshindi
alitakiwa kupatikana.
Mwishowe Urunani ndio ilioonekana kuwa na
vikapo vingi zaidi ya Espoir ya Rwanda. Ushindi huo wa Urunani unaashiria
kufuzu moja kwa moja kwa klabu hiyo kwenye michuano ya kombe la Afrika ambayo itafanyika hivi karibuni.