Michuano
ya Basketball kanda ya tano inayojumuisha vilabu vilivyo nyakuwa
ubingwa katika nchi za Afrika Mashariki na kati yanayofanyika jijini Bujumbura nchini Burundi
hapo jana yameendelea kutimua vumbi kwa siku ya pili.
Upande
wa timu za wanawake zilizojitupa uwanjani jana timu ya USIU kutoka
nchini Kenya ilichuana na KCCA ya Uganda na kushindana kwa vikapo 60
kwa 43 kwa faida ya USIU ya Kenya.
Don
Bosco ya Tanzania nao walilambishwa mchanga na Les Gazelles ya
Burundi kwa vikapo 52 kwa 47, huku mechi kati ya Eagle Wings ya Kenya
na APR ya Rwanda ikiahirishwa hadi siku ya alhamisi.
Upande
wa wanamume News Stars wa Burundi, iliwashinda Vijana kutoka Tanzania
kwa vikapo 91 kwa 53, Urunani nayo ya Burundi iliishinda kwa tabu
USIU ya Kenya kwa vikapo 61 kwa 60.
Timu
mbili zinazo shirika michuano hiyo tayari zimejikatia tiketi ya
kuendelea na michuano hiyo ikiw ani pamoja na Les Gazelles ya Burundi
pamoja na USIU ya Kenya.