Moto
mkubwa umezuka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta
nchini Kenya leo alfajiri na kusababisha ndege zilizokuwa zikitarajia
kutua katika uwanja huo kuelekezwa katika viwanja vingine sambamba na
safari kuahirishwa na uwanja kufungwa wakati huu ambapo kikosi cha
dharura kinaendelea na jitihada za kuzuia moto huo kusambaa na
kutafuta chanzo chake.
Kiongozi
wa juu katika uwanja huo wa kimataifa Mutea Irigo amesema kuwa
jitihada za kila namna zinafanywa kujaribu kuzuia moto huo kusambaa
zaidi ingawa wizara ya mambo ya ndani imekiri kwamba wanakabiliwa na
hatari ya kuishiwa maji.
Taarifa
zinaeleza kuwa hadi sasa hakuna majeruhi wala maafa ambayo
yamejitokeza ingawa moto ulikuwa mkubwa amesema Irigo na kuongeza
kuwa vitengo vya abiria wanaowasili na uhamiaji vimeharibiwa kabisa.
Ndege
kadhaa ambazo zilitarajiwa kutua uwanjani hapo kutoka Dubai na Hong
Kong, zimeelekezwa kutua katika uwanja wa Port City uliko Mombasa na
kwamba kwa sasa moto umedhibitiwa.
Uwanja
huo umekuwa tegemeo kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki, pamoja na
ndege za kimataifa za masafa marefu zimekuwa zikitua katika uwanja
huo kuunganisha safari kwenye kanda nzima.
Aid
ha
barabara zote za karibu na uwanja huo zimefungwa isipikuwa kwa
dharura na hakuna watu wanaoruhusiwa kukaribia uwanjani hapo .
Moto
huo umezuka siku mbili baada ya safari kucheleweshwa kwa saa kadhaa
baada ya upungufu wa mafuta ya ndege kutokea.