Bus
la Kampuni ya Usafiri la Taqwa lililokuwa na abiria 51 likisafiri kutokea jijini
Bujumbura nchini Burundi kuelekea Dar es Salaam Tanzania, usiku wa
jana kuamkia leo Jumatano Octoba 2, limetekwa na majambazi katika eneo la Mirade kata
ya Iguguno Mkoani Singida.
Majambazi
hao waliweka mawe makubwa barabarani na kuyafunika kwa majani.
Dereva wa Bus hilo aligonga mawe hayo na hivo tairi za bus hilo
kupasuka na kusababisha bus hilo kuanguka kwenye korongo.
Majambazi
hao walilazimisha abiria kushuka ndani ya Bus mmoja baada ya
mwingine.
Kwa
Mujibu wa kamanda wa Polisi katika Mkao wa Singida Joseph Kamelwa,
takriban dola za Marekani elfu moja, Shilingi za Tanzania milioni
tano na franka za Burundi laki mbili, zimeporwa
Abiria
20 wamejeruhiwa kwa kupigwa, huku vitu mbalimbali vya thamni
vikiporwa.
Polisi inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika.