Wanariadha
wa huko Kenya wameshindwa kusafiri jana kuelekea nchini Urusi
kushiriki mashindano ya riadhaa ya dunia yatayo timua vumbi nchini
humo kuanzia Agosti 10 hadi tarehe 18 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka nchini humo safari za ndege kuelekea nje ya
nchi hiyo ziliparaganyika baada ya ndege zote zilizokuwa kwenye
orodha ya safari nchini humo hapo jana, kutakiwa kuwekwa mafuta.
Taarifa
hii imesema sio wanariadha pekee waliokumbwa na dhahama hii bali pia
wasafiri wote waliotakiwa kusafiri kwa ndege kuelekea nje ya taifa
hilo.
Safari
hizo za ndege ambazo zilitakiwa kufanyika jana, hatimaye zinafanyika
leo ambapo wanariadha hao wameanza safari yao kuiwakilisha Kenya
katika mashindano hayo ya riadha.