Ijumaa, 30 Agosti 2013

RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZIZA AREJEA NCHINI BAADA YA MAPUMZIKO YAKE JIJINI DAR ES SALAAM - TANZANIA

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amemaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini Tanzania na tayari amerejea nchini. Hapo ni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalim Julius Kambarage Nyerere akiagana na makam wa rais wa jamuhuti ya Muungano wa Tanzania, Dr Gharib Bilal

Alhamisi, 29 Agosti 2013

LE MAJORDOME FILAMU ILIOMFANYA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA KUANGUSHA CHOZI


Rais wa Marekani Barack Obama amethibitisha juzi Jumanne kwamba aliangusha chozi wakati alipoona filamu "Le Majordome", filamu ambayo ilionyesha mapambano ya watu weusi nchini Marekani katika kutafuta haki kwa wote kupitia mfanyakazi mweusi kwenye Ikulu ya rais ya Marekani ya White House.



Sikulia kwa sababu tu nilifkiria kuona wafanyakazi waliohudumu hapa Ikulu ya White House, lakini pia kizazi cha watu waliokuwa na uwezo na wenye vipaji, lakini walikuwa wakiwazuia kutokana na sheria ya ubaguzi wa rangi iliokuwepo “"

Obama aliongeza kuwa

"Kwa hadhi na mshikamano, waliamka kila siku kuelekea kazini huku wakivumilia mambo mengi kwa sababu walikuwa wanatarajia kuandaa maisha bora kwa watoto wao.”


Jumanne, 27 Agosti 2013

AJABU NA KWELI WANAUME WAWILI WAKUBALIANA KUESHI NA MWANAMKE MMOJA

Kwa kweli sina mengi zaidi mbali na kukupa nafasi ya kuangalia video hii inayoonyesha mkataba wa wanaume wawili waliokubaliana kueshi na mwanamke mmoja huko Kenya katika mji wa Mombasa.


KOCHA MKUU WA CHELSEA JOSE MORIHNO AMPA WAYNE ROONEY SAA 48 KUFANYA MAAMUZI


Kocha mkuu wa Klabu ya Chelsea daraja la kwanza nchini Uingereza Jose Mourinho amempa Wayne Rooney saa 48 kutangaza hadharani nia ya kuondoka Manchester United kuhamia Chelsea au la.

Chelsea ilipepetana jana na Manchester United na kulazimishana sare ya 0-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford jana Jumatatu usiku.

akizungumza na waandishi wa habari Jose Morinho amemtaka  Wayne Rooney kwamba sasa anatakiwa kumaliza hadithi aliayoianzisha.

 Mashabiki wa United waliimba jina la Rooney wakati wa mchezo na Mourinho akasema anataka kupeleka ofa nyingine.

Chelsea imekwishapeleka mezani ofa mbili kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa England na iatuma ofa ya tatu ikiwa Rooney atatangaza kuondoka. 

Kocha huyo wa Chelsea amemuambia Rooney kwamba ni wakati wa kufanya maamuzi. na kumsifu katika mchezo uliomalizika na kusema kwamba ni mwanasoka kweli, amejaribu kushinda, kufunga, ameshamiri uwanjani.

"Baada ya hiyo ikiwa anataka kuondoka, anatakiwa kusema. Ikiwa hataki kuondoka tena, tutaheshimu hilo na tutasema asante na kuendelea,".


Jumatatu, 26 Agosti 2013

TAMASHA LA AMANI KUFANYIKA MJINI GOMA MWISHONI MWA MWEZI AGOSTI

Albert Nkulu msanii wa Burundi aliye shiriki katika tamasha la Amani mwaka uliopita

Tamasha la Amani linatarajiwa kuzinduliwa jijini Goma Agosti 30 mwaka huu na kutamatishwa Septemba Mosi, ikiwa ni moa miongoni mwa tamasha lenye lengo la kuwaleta pamoja wasanii kutoka katika mataifa mbalimbali katika hali ya kuhamasisha maridhiano katika ukanda wa maziwa makuu.

Miongoni mwa wasanii wataoshiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Youssoupha, msanii wa Congo anaikipinga nchini Ufaransa, Picha, msanii wa Congo anaye eshi nchini Ubelgiji na Freddy Massamba msanii wa Congo Brazaville anaye eshi nchini Ubelgiji.

Moja miongoni mwa kundi la wasanii wa Goma wakionyesha makeke jukwani

Mbali na wasanii hao watakuwepo pia wasanii wa ukanda wa maziwa makuu hususan Rwanda, Burundi na Uganda pamoja na makundi ya muziki wa jadi ytayo wakilisha makabila yote ya Mkoa wa Kivu ya Kaskazini.

kwa mujibu wa Eric Lamote aliye andaa tamasha hili, lengo hasa ni kutowa wito kwa ulimwengu kwa kuwaleta pamoja watu kutoka katika mataifa mbalimbali ili kukomesha madhila yanayowakumba wananchi wa eneo hilo, aidha kuhusu swala la Usalama amesema majeshi ya Kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini DRCongo Monusco ndiyo yatayo husika na ulinzi wa Usalama.

Kwa wasanii wa kimataifa ambao wangelipenda kushiriki katika tamssha hilo wametolewa wito wa kujitolea bila kujali kupewa malipo.


KITIM TIM LEO KATI YA CHELSEA NA MANCHESTER UNITED LIGI KUU NCHINI UINGEREZA

Klabu ya Chelsea inawapokea Mashetani wekundu leo jioni, ikiwa ni siku saba ngumu kwa Klabu ya Manchester United kwenye ligi kuu ya Soka ya England msimu huu.

Ugumu huo unatokana na mechi mbili ambazo klabu hiyo bingwa mtetezi wa ligi kuu hiyo itacheza dhidi ya Chelsea leo Jumatatu kwenye uwanja wa Old Trafford na na kisha Liverpool Jumapili. Man United ilioachana na kocha wake mkongwe Alex Furguson mwisho wa msimu uliopita na sasa ipo chini ya David Moyes kocha aliyekuwa akiinoa Everton. 

BAADA YA DAR ES SALAAM SASA NI ZAMU YA JIJI LA BUJUMBURA

Baada ya serikali ya Tanzania kuingia kwenye mfumo wa Digital tangu mwaka uliopita, serikali ya burundi nayo inajiandaa kuingia kwenye mfumo huo. kulingana na Makam wa kwa za wa rais wa serikali ya Burundi, Terence Sinunguruza, amesema mfumo huo utaanza kufanyakazi kuanzia Julay Mosi mwaka 2015.

Kwa sasa jijini Dar Es Salaam kama huna kidigiti(Decodeur) huwezi kuona TV. Hii imepelekea idadi ya wananchi waliokuwa wakifuatilia habari mbalimbali kwenye TV wakikosa fursa hiyo, hivyo muda bado upo wa kujipanga kuhakikisha hakuna athari zozote zitazojitokeza baada ya kuingia kwenye mfumo huu.


WATU WAWILI WAPOTEZA MAISHA KATIKA MAANDAMANO HUKO GOMA

Baada ya kuawa kwa watu watu mjini Goma na makombora yaliorushwa katika mji huo wakati wa mapambano baina ya waasi wa kundi la M23 na wanajeshi wa serikali wa FARDC, wananchi mjini Goma wamepatwa na hasira na hivo kuandamana mwishoni mwa juma.Watu wawili wamepoteza maisha katika maandamano hayo. 

Umoja wa Mataifa unasema umeanzisha uchunguzi kubaini ikiwa kweli wanajeshi wake wa kulinda wa amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walihusika na vifo vya watu wawili mjini Goma mwishoni mwa wiki iliyopita.

Walioshuhudia mauaji hayo wanasema kuwa wanajeshi wa MONUSCO raia wa Uruguay waliwapiga risasi watu wawili wakati walipokuwa wanasambaratisha kundi la waandamanaji lililokuwa limevamia kambi ya jeshi hilo.

Mauaji haya yametokea siku moja tu baada ya kutokea kwa shambulizi la guruneti mjini Goma na kusabisha vifo vya watu watatu na kuwajeruhiwa wanajeshi watatu wa kulinda amani.

Wiki iliyopita, waasi wa M 23 na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamekuwa wakipambana karibu na mji wa Goma huku kila upande ukituhumiana kuanzisha makabiliano hayo.

Ukosefu wa amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeilazimu serikali ya Uingereza kuwataka raia wake wote wanaoishi na kufanya kazi mjini Goma kuondoka kwa kuhofia usalama wao.

Kiongozi wa kundi la M 23 Betrand Bissimwa amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akilalamikia kuhusika kwa jeshi la kulinda amani katika mzozo wa Mashariki mwa nchi hiyo na kutekeleza mauaji .

Jeshi la serikali kwa upande wake linasema kuwa litaendelea kulinda mipaka ya nchi hiyo na pia kukabiliana na makundi ya waasi likiwemo la M 23 ikiwa litaanza kuwavamia.

Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M 23 yamegonga mwamba jijini Kampala Uganda suala ambalo limeendelea kuhatarisha usalama Mashariki mwa nchi hiyo.

Jumapili, 25 Agosti 2013

HALI YA HEMED SULEIMANI YAENDELEA KUIMARIKA BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA

Msanii wa Bongo Fleva lakini pia muigiza wa filamu za kibongo za Bongo Movies,  Hemed Suleimani a.k.a PHD hapo jana usiku amepata ajali mbaya ya barabarani ambapo gari alilokuwa akiendesha limeharibika vibaya.
Muonekano wa Hemed Suleimani baada ya kupata ajali

Taarifa kutoka jijini Dar Es Salaam ajali hiyo ilitokea wakati Hemedi alipokuwa akimsindikiza msanii mwenzie Gerry wa Rythmes nyumbani kwake Sinza jiji Dar Es Salaam. Taarifa zaidi zinasema kwamba hali ya msanii huyo inaendelea vizuri.

HAPPY BIRTHDAY JEREMI'S PRODUCTION


Msanii na Producer muanzilishi wa muziki wa kizazi kipya nchini Burundi Hakeshimana Jeremie a.k.a Jeremi's Pro, leo hii Jumapili Agosti 25 anaadhimisha sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.










Jeremie ambaye amejijengea sifa kubwa katika kutengeneza muziki wa kizazi kipya nchini Burundi, kwa sasa amejichimbia makaazi huko Ubelgiji katika jiji la Anvers ambako mbali na shughuli za kutengeneza Muziki amekuwa pia akiimba kutunga na kushangiliwa na wengi huko Ulaya.
Ikoh Multiservice, tunamtakia Kila la Kheri, na kumuomba aangalia nyuma, kwani tangu aondoke, hajaangalia Nyuma

VIDEO CLIP BIRABABAJE NI MOJA MIONGONI MWA KAZI ZA IKOH MULTISERVICE

Angalia Clip Video Birababaje moja miongoni mwa kazi za kampuni ya Ikoh Multiservice


Alhamisi, 22 Agosti 2013

STERING WA SERIES YA PRISON BREAK AJITANGAZA KUWA SHOGA


Bingwa wa filamu ya Series ya Prison Break Wentworth Miller maharufu kama Michael Scotfild kijana mtanashati ambaye binti yeyote anayepumua angemtamani kumpata lakini kaamua kujitangaza rasmi yeye si ridhiki 'SHOGA, rufu yamsemo wa kimjini 

Mchizi huyu masela wengi wametokea kumkubali zaidi katika mfululizo wa series maarufu ya Prison Break akiwa kama Star 'STERINGI' wa mchezo mzima..

Jamaa huyu amejitangaza tarehe 21 agosti katika tamasha la filamu la Saint Petersburg, Akiandika barua ya wazi kuupinga mwaliko baada ya serikali ya Urusi kupitisha sheria inayopinga ushoga jamaa huyo mwenye miaka  41 aliandika hivi:

Thank you for your kind invitation. As someone who has enjoyed visiting Russia in the past and can also claim a degree of Russian ancestry, it would make me happy to say yes. However, as a gay man, I must decline.

I am deeply troubled by the current attitude toward and treatment of gay men and women by the Russian government. The situation is in no way acceptable, and I cannot in good conscience participate in a celebratory occasion hosted by a country where people like myself are being systematically denied their basic right to live and love openly.

Perhaps, when and if circumstances improve, I'll be free to make a different choice.

Until then. Wentworth Miller

Jumanne, 20 Agosti 2013

CHRIS DIZZO NA MAANDALIZI YA VIDEO NYINGINE WAKATI AKIJIANDAA KUACHIA VIDEO YA WIMBO NIMEDADA

Wakati akijiandaa kuachia Video yake ya Nimedata, Msanii wa Burundi anaekipiga huko Afrika Kusini Chris Dizzo yupo Studio la Soul kuandaa single nyingine zina, zitazo kwenda sanjari  na video.
Chris Dizzo na Producer wake La Sooul

Kuhusu Jina la Track ambazo anawaandalia mashabiki wake, Chris Dizzo amesema bado mapema kutowa taarifa, lakini mashabiki wakae mkao wa kusubiri, kwani kwa sasa amebadilika na kuingia kwenye hatuwa nyingine.

Aidha, kuhusu lini ataachi video yake ya Wimbo Nimedata, Chris Dizzo amesema kil akitu kipo tayari kwas asa anasubiri muda tu, na wakati utapofikia atatowa taarifa.



Ijumaa, 16 Agosti 2013

KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWA MSANII OLGA LORIE

Msanii wa Burundi wa kizazi kipya katika tasnia ya Muziki upande wa wanawake Ntaganzwa Olga Lorie, Maharufu kama Olga leo hii ameadhimisha sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Hatuna budi kumtakia kila la kheri Olga Lorie katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

         

Alhamisi, 15 Agosti 2013

AJIUA KWA RISASE AKIWA KATIKA WODI YA WAZAZI WAKATI MKEWE AKIJIFUNGUA.

Tukio hilo limetokea huko Marekani katika mji wa Texas Jumapili iliopita katika Hospitali ya Willowbrook ambapo Kendra aliingia wodini kwa ajili ya kujifungua. Saa moja baada ya kumleta duniani, mwanae, mumewe Michael aliamuwa kusitisha maisha yake kwa kujilipua na risase. Habari zinasema kwamba mke na mumewe walizozana sana wakiwa wodini, na baada ya mabishano Michael aliamuwa aliamuwa mambo mengine na kuchukuwa bastola na kujkiua mbele ya mkewe. Kwa bahati nzuri mtoto hakuwepo na mkewe hakujeruhiwa. Ma daktari walijaribu kumshughulikia bila mafaanikio.
Majumba yanaficha siri nyingi, vijana hawa ukiwaona utaona kwamba ni wenye furaha mno lakini huwezi amini kilichotokea
Familia ya Michael imeshindwa kuelewa na inatafuta sababu za Michael kuchukuwa uamuzi mzito kama huo na alionekana mwenye kuwa na usongo wa mawazo na hakuna aliejuwa kwamba angeliweza kuchuykuwa uamuzi kama huo.


Tukio hilo limezua mjadala kuhusu uslama katika maeneo ya umma nchini Marekani. Kawaida hairuhusiwi kuingia na silaha katika Hospitali hiyo. Wagonjwa wengi wameanza kujiuliza kuhusu usalama wao  katika Hospitali hiyo. Uongozi wa Hospitali hiyo ya Willowbook wamejizuia kuzungumzia tukio hilo.

HUYU NDIYE MWANAUME MWENYE UMRI WA MIAKA 66 AMBAYE HAJAWAHI KUOGA TANGU MWAKA 1974

Kwa watu wengi kote duniani sio rahisi kumuona mtu anafanya siku nzima bila kuoga, lakini kwa baba huyo Kailash Singh mzee mwenye umri wa miaka 66, raia wa India hajaoga tangu miaka 38 iliopita na anasema kuwa mwenye furaha kama watu wengine wanaooga kila siku. Kipi kilichomfanya achukuwe uamuzi kama huu? Kailash amesema alichukuwa uamuzi huo tangu mwaka 1974 baada ya kufunga ndoa kwa fikira kwamba itamsaidia kupata mtoto, amesema kuna Padri mmoja alimthibitishia kwamba akiacha kuoga atapata mtoto, jambo ambalo alitekeleza hadi leo, na hajawahi kuguza nywele zake.


Mkewe Kalavati Devi upande wake amesema alimshawishi kiasi awezavyo bila mafaanikio ambapo alikuwa na wakati mgumu katika kuizoea hali hiyo.

Familia yake nayo pia ilijaribu kumkamata kwa nguvu na kumpeleka mtoni, lakini aliponyoka na kukimbia huku akisema kwamba kuliko kuoga afadhali afe.


Inaaminika kwamba huyu ndiye mwanaume mwenye kunuka zaidi duniani.

MAJESHI YA SOMALIA NA YA AMISOM YASHTUMIWA UBAKAJI

Kikosi cha umoja wa Afrika kilicho kwenye Operesheni ya kulinda amani nchini Somalia kinafanya uchunguzi kuhusu shutma za vitendo vya ubakaji vilivyofanywa na Wanajeshi kadhaa dhidi ya Mwanamke mmoja, tukio lililoamsha ghadhabu jijini Mogadishu, Umoja wa Afrika umeeleza. Mwanamke wa kisomali amedai kuwa alikamatwa, kuburuzwa na kisha kubakwa na Wanajeshi wa Serikali ya Somalia na wa AMISOM.  




Kikosi cha AMISOM kimekiri kuwa kimepokea shutma hizo dhidi ya Wanajeshi wake. Kauli ya AMISOM imesema kuwa jeshi lake na lile la Somalia limeandaa kikosi ambacho kitafanya uchunguzi na baadae hatua stahiki zitachukuliwa baada ya kubainika ukweli juu ya shutuma hizo.

 


Majeshi ya Umoja wa Afrika yaliyo kwenye Operesheni nchini Somalia yamekemea vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji. Vikosi vya Umoja wa Afrika vinavyojumuisha Wanajeshi kutoka nchi tano, Burundi, Djibouti, Kenya, Sierra Leone na Uganda vimekuwa vikipambana na Wanamgambo wa Al Shabab wenye uhusiano na Al-Qaeda, tangu mwaka 2007.

 

Ikiwa itathibitika kuwa kweli Wanajeshi wa Vikosi hivyo wamejihusisha na vitendo vya ubakaji itaathiri heshima ya Vikosi vya Umoja wa Afrika iliyojiwekea mbele ya uso wa jumuia ya kimataifa. Jeshi la Somalia awali liliwahi kushutumiwa na makundi ya kutetea haki za binaadam kuwa Wanajeshi wake wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya Wanawake vikiwemo vitendo vya ubakaji.

  


Shutma juu ya Vitendo vya ubakaji dhidi ya Mwanamama huyo kutekelezwa na Wanajeshi wa AMISOM imewashtua Walio wengi.



Jumatano, 14 Agosti 2013

VIJANA ZAIDI YA MIA MOJA WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UJAMBAZI JIJINI BUJUMBURA


Jeshi la polisi nchini Burundi, limewatia nguvuni genge la vijana zaidi ya mia moja wa kiume akiwemo msichana mmoja kwa tuhuma za kujihusisha na wizi ujambazi na uporaji wa mali ya raia wa maeneo ya mitaa ya Bwiza, Jabe, Nyakabiga, Mutanga na ambao wamekuwa wakijificha katika mto Ntahangwa.

Kundi la vijana waliokamatwa na polisi
Katika siku zote hizi za nyuma wananchi wakaazi wa tarafa za Mutanga, Jabe, Nyakabiga na Kigobe wanalalama kukithiri kwa wizi hususan katika barabara ya Imprimerie kuanzia kwenye daraja la mto Ntahangwa eneo la kaskazini barabara ya Novemba 28 hadi kwenye daraja la mto huo eneo la kati la barabara iliobatizwa Peuple Murundi.

Katika miaka ya nyuma eneo hilo lilikuwa likitumiwa na majambazi ambao walikuwa wakiendesha wizi katika mita mbalimbali ya manispaa ya jiji la Bujumbura kwa kutumia jiwe lililoitwa Katarina na kujificha katika eneo hilo na kuitwa Avenue de la Mort kufuatia vile lilikuwa eneo hatari. Wakati huo wa uongozi wa rais Bagaza alitangaza adhabu ya kunyongwa kwa wa Katarina na wa fatuma wote na hivo kukomesha vitendo hivyo.

Hivi karibuni msanii mwenye jina jijini Bujumbura Yoya Jamal alianguka kwenye mtengo wa majambazi hao waliompora kila kitu alichokuwa nacho na kumuacha mtupu huku akiwa hana fahamu baada ya kumjeruhi. Mungu alipita kati alipata wasamaria waliompeleka Hospitalini ili kuokowa maisha yake.

Hatuwa madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa ili kukomesha vitendo hivyo.

TIMBULO NA VIDEO YAKE SINA MAKOSA.

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu hatimaye Timbulo avunja ukimya kwa kutowa bonge la Video ya wimbo wake unaofanya vizuri "Sina Makosa"

Jumapili, 11 Agosti 2013

NZIZA DESIRE AVUNJA UKIMYA

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hatimaye msanii mkongwe kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini Burundi, Nziza Desire ambaye amejichimbia makaazi yake huko nchini Marekani, amevunja ukimya na kutowa sababu za kutosikika kwa kipindi chote hiki.

Akichonga na Ikoh.biz, Nziza Desire amesema : Nipo katika maandalizi ya Video Clip za album yangu ya UN ambayo ninafanya kila jitihada kuhakikisha hadi mwishoni mwa mwaka huu zinakuwa tayari. ameendelea kuwa : Kuandaa Video Clip ukiwa nchi za ng'ambo kama vile USA sio jambo rahisi, linahitaji uwezo mkubwa sana, sio kama hapo nyumbani, tunatakiwa kutuliza akili fasi moja na kuwa na muda mrefu katika kupanga kila jambo huku pia tukiendeleza kazi nyingi mbali na muziki, kwakuwa majukumu ya familia yanahitajika zaidi, na ndio maana tunapambana huku na kule.

Katika album yake ya UN Nziza Desire kuna baadhi ya nyimbo ambazo tayari kisha recordi video na nyingine bado na sasa ndio shuhguhuli inayo mfanya kuwa kimya.

Jumamosi, 10 Agosti 2013

URUNANI YASHINDA KOMBE LA VILABU KUTOKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA KUILAZA ESPOIR YA RWANDA

Klabu ya mpira wa kikapu ya Urunani kutoka Burundi imefaanikiwa kushinda kombe la michuano ya vilabu kutoka katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na kati ama Zone 5, kwa kuilaza Espoir ya Rwanda kwa vikapu 65 kwa 59.

Halaiki ya wapenzi wa mpira wa kikapu walimiminika kwa wingi kushuhudia mechi hiyo iliokuwa na mvuto, kwani kila timu ilionyesha juhudi za kutaka kushinda. Lakini kama mjuavyo, mshindi alitakiwa kupatikana.


Mwishowe Urunani ndio ilioonekana kuwa na vikapo vingi zaidi ya Espoir ya Rwanda. Ushindi huo wa Urunani unaashiria kufuzu moja kwa moja kwa klabu hiyo kwenye michuano ya kombe la Afrika ambayo itafanyika hivi karibuni.

Alhamisi, 8 Agosti 2013

RAIA WAWILI WA UINGEREZA WAMWAGIWA TINDIKALI VISIWANI ZANZIBAR NCHINI TANZANIA

Raia wawili wa Uingereza wamemwagiwa tindi kali nchini Tanzania kwenye eneo la mji wa mkongwe visiwani Zanzibar "Stone Town" na sasa wamesafirishwa hadi jijini Dar es Salaam Tanzania bara kwa matibabu zaidi, polisi wamesema.

Raia hao wawili wasichana wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 wanaaminika kuwa walikuwa wakifanya kazi za kujitolea visiwani humo na kwamba tukio hili ni la kwanza kufanywa kwa raia wa Kigeni.

Kaimu kamanda wa Polisi Visiwani Zanzibar, Mkadam Khamis amewaambia waandishi wa habari visiwani humo kuwa watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki waliwakaribia wasichana hao na kisha kuwamwagia tindi kali.Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imekiri kuwa na taarifa hizo na kwamba wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha raia hao wanapatiwa matibabu ya haraka kuwanusuru na madhara zaidi ya acid hiyo.

Polisi wanasema bado wanaendelea na uchunguzi na kwamba mpaka sasa watu waliohusika na shambulio hilo hawajafahamika ila uchunguzi bado unaendelea na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kubaini wahusika. Wizara ya mambo ya nje imesema kuwa zaidi ya raia elfu 75 wa Uingereza ambao huetembeala Tanzania kila mwaka, hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi yakuwalenga raia wakigeni jambo ambalo linahatarisha usalama wao.

Wizara hiyo imeongeza kuwa kumekuwa na matukio ya uporaji wa mizigo ya raia wa kigeni hasa kwenye baadhi ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine hali ambayo hivi sasa inaonekana kuota mizizi. Hivi Karibuni watu wasiofahamika walimwagia tindi kali mufti msaidizi wa Zanzibar pamoja na kumpiga risasi padri wa kanisa Katoliki


USAFIRI WA NDEGE WA KIMATAIFA NCHINI KENYA WAREJEA TENA KWENYE UWANJA WA NDEGE WAKATI UCHUNGUZI UKIANZISHWA KUBAINI CHANZO CHA MOTO ULIOTOKEA JANA

Safari za ndege za Kimataifa hatimaye zimeanza tena katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya kufuatia hapo jana kusitishwa kutokana na ajali ya moto kwenye uwanja huo. 
Hapo jana Serikali ya Kenya ilitangaza kusitisha safari zote za kimataifa kwenye uwanja huo kutokana na kuungua kwa sehemu ya uwanja hasa kwenye eneo la kuwasili kwa abiria wa kimataifa pamoja na idara ya uhamiaji.

Ndege nyingi hapo jana zilizokuwa zikitarajiwa kutumia uwanja huo zililazimika kukatisha safari zao na kuelekea kwenye nchi jirani za Tanzania na Uganda huku baadhi zikielekezwa kwenye uwanja wa kimataifa wa Moi mjini Mombasa. Rais Uhuru Kenyatta pamoja na waziri wa masuala ya usafiri wa Kenya hapo jana waliahidi kufanya kila linalowezekana ili kufanikisha kurejeshwa kwa safari za kimataifa kwenye uwanja huo jambo ambalo limeanza kushuhudiwa hii leo.

Ndege ya kwanza kutua ilikuwa ikitokea nchini Uingereza na kutua majira ya ya saa kumi na mbili na nusu kwa saa za Afrika Mashariki. Ndege nyingine zilizoshuhudiwa zikitua kwenye uwanja huo ni pamoja na zile zilizotoka nchini Bangkok na kilimanjaro nchini Tanzania hali ambayo sasa inatoa matumaini ya kurejea kwa safari nyingi hii leo.

Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta ni uwanja mkubwa zaidi kutumika kwenye kanda hii ya Afrika Mashariki ambapo huudumia zaidi ya abiria elfu kumi na sita kwa siku. Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema kuwa kutokana na kuungua kwa sehemu ya uwanja huo na kusitishwa kwa safari nyingi hapo jana kumeathiri kwa kiasi hali ya uchumi wa taifa hilo kwakuwa uwanja huo umetegemewa kwa kuingiza watalii wengi zaidi.

Shughuli za usafiri wa Tax zilikosa wateja kutokana na moto huo huku wachuuzi wa barabarani pia nao wakidai kuathirika kutokana na ajali hiyo. Safari za ndege za ndani zenyewe zilianza hiyo jana mara baada ya moto mkubwa kudhibitiwa. Moto huo ulianza majira ya saa kumi za alfajiri usiku wa Jumatano na kusababisha kuunguza sehemu kubwa ya idara ya uhamiaji na sehemu ya kuingilia abiria wa kimataifa.

Uchunguzi tayari umeanza kubaini chanzo cha moto huo.


Jumatano, 7 Agosti 2013

YOYA JAMAL APONEA CHUPU CHUPU.

Msanii wa kizazi kipya nchini Burundi Yoya, juzi amenusurika baada ya kukabwa na kundi la watu wakati alipokuwa akirejea nyumbani Tarafani Nyakabiga.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumatatu (Lundi) kuamkia Jumanne (Mardi) Usiku wa saa tano, eneo linalo gawa Nyakabiga ya Tatu na Mutanga, pindi kundi la watu walimsimamisha wakati alikuwa ndani ya gari lake na kumpora vitu vyote alivyokuwa navyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msanii mwenyewe”Niliona watu wakanisimisha kama kawaida tu nikasimama, sikujuwa kumbe ni majambazi, wamenipora viato nilivyokuwa nimevaa, saa ya mkononi, simu yangu nzuri niliokuwa nimenunua hivi majuzi aina ya Sunsung Galaxys4, kwenye Wallet(Ngodo) nilikuwa na kiasi cha Franka za Burundi laki moja na elfu arobaini (140.000FBU) ambapo ni hela kidogo sana, inaskitisha

Yoya ameendelea kuwa wakati huo alipigwa na kupoteza fahamu. Wahalifu hao walimtelekeza na kutimka. Baada ya muda ndipo wasamaria wema waliokuwa wakipita katika eneo hilo, wakamuona na kumtambua, ingawaje ilikuwa ni usiku, na kumpeleka moja kwa moja Hospitali .

Yoya anatowa shukrani za dhati kwa watu hao pamoja pia na ma dakari na nesi waliomshukulikia kwenye Hospitali ya Clinique Central de Bujumbura hadi kufikia wakati.

Msanii huyo anaendelea kuuguza majeraha yake akiwa nyumbani baada ya kutibiwa kwenye Hospital hiyo yenye sifa zake jijini Bujumbura. 


SAFARI ZA NDEGE ZASITISHWA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA BAADA YA KUTOKEA MOTO MKUBWA MAPEMA LEO ASUBUHI


Moto mkubwa umezuka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya leo alfajiri na kusababisha ndege zilizokuwa zikitarajia kutua katika uwanja huo kuelekezwa katika viwanja vingine sambamba na safari kuahirishwa na uwanja kufungwa wakati huu ambapo kikosi cha dharura kinaendelea na jitihada za kuzuia moto huo kusambaa na kutafuta chanzo chake.

Kiongozi wa juu katika uwanja huo wa kimataifa Mutea Irigo amesema kuwa jitihada za kila namna zinafanywa kujaribu kuzuia moto huo kusambaa zaidi ingawa wizara ya mambo ya ndani imekiri kwamba wanakabiliwa na hatari ya kuishiwa maji.

Taarifa zinaeleza kuwa hadi sasa hakuna majeruhi wala maafa ambayo yamejitokeza ingawa moto ulikuwa mkubwa amesema Irigo na kuongeza kuwa vitengo vya abiria wanaowasili na uhamiaji vimeharibiwa kabisa.

Ndege kadhaa ambazo zilitarajiwa kutua uwanjani hapo kutoka Dubai na Hong Kong, zimeelekezwa kutua katika uwanja wa Port City uliko Mombasa na kwamba kwa sasa moto umedhibitiwa.

Uwanja huo umekuwa tegemeo kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki, pamoja na ndege za kimataifa za masafa marefu zimekuwa zikitua katika uwanja huo kuunganisha safari kwenye kanda nzima.
Aid

ha barabara zote za karibu na uwanja huo zimefungwa isipikuwa kwa dharura na hakuna watu wanaoruhusiwa kukaribia uwanjani hapo .

Moto huo umezuka siku mbili baada ya safari kucheleweshwa kwa saa kadhaa baada ya upungufu wa mafuta ya ndege kutokea.

MICHUANO YA BASKETBALL KANDA YA VI YAENDELEA KUTIKISA JIJINI BUJUMBURA


Michuano ya Basketball kanda ya tano inayojumuisha vilabu vilivyo nyakuwa ubingwa katika nchi za Afrika Mashariki na kati yanayofanyika jijini Bujumbura nchini Burundi hapo jana yameendelea kutimua vumbi kwa siku ya pili.

Upande wa timu za wanawake zilizojitupa uwanjani jana timu ya USIU kutoka nchini Kenya ilichuana na KCCA ya Uganda na kushindana kwa vikapo 60 kwa 43 kwa faida ya USIU ya Kenya.

Don Bosco ya Tanzania nao walilambishwa mchanga na Les Gazelles ya Burundi kwa vikapo 52 kwa 47, huku mechi kati ya Eagle Wings ya Kenya na APR ya Rwanda ikiahirishwa hadi siku ya alhamisi.

Upande wa wanamume News Stars wa Burundi, iliwashinda Vijana kutoka Tanzania kwa vikapo 91 kwa 53, Urunani nayo ya Burundi iliishinda kwa tabu USIU ya Kenya kwa vikapo 61 kwa 60.

Timu mbili zinazo shirika michuano hiyo tayari zimejikatia tiketi ya kuendelea na michuano hiyo ikiw ani pamoja na Les Gazelles ya Burundi pamoja na USIU ya Kenya.



Jumanne, 6 Agosti 2013

MICHUANO YA KIKAPO YA AFRIKA MASHARIKI YATIMUA VUMBI JIJINI BUJUMBURA


Michuano ya kikapo inayojumuisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na kati Zone V, imezinduliwa jana jijini Bujumbura. Hii ni mara ya pili Burundi inakuwa mwenyeji wa michuano hiyo. Mechi ya kwanza ya ufunguzi imezipambanisha timu za wanawake les Gazelles ya Burundi na APR wa Rwanda, na kushuhudia le Gazelles wakiilaza APR kwa vikapo 50 kwa 35.
Mechi iliofuatia na ambayo ilikuwa ikisubiriwa na wengi ilizikutanisha timu bingwa wa michuano hiyo mwaka 2012 Espoir ya Rwanda pamoja na Urunani ya burundi ambayo iliwahi kutwaa kombe la michuano hiyo mwaka 2011. Licha ya kucheza mbele ya mashabiki wake, Urunani ililazwa na Espoir kwa vikapo 60 kwa 41
Berco Stars ambayo ilianza michuano hiyo kwa matumaini, lakini ilijikuta ikimaliza mechi kwa maskitiko. Timu ya Kenya ya USIU (United states international university) waliibuka washinda kwa vikapo 76 kwa 71. kati ya wachezaji 12 wa Kenya, wanne ni kutoka Burundi katika Mkoa wa Ngozi. Nao ni : Diane Richesse Nikuze, Ghislaine Munezero, Magnifique Ndayikengurukiye pamoja na Cynthia Kaburundi.
Mechi ya mwisho kwa siku ya jana ilizipambanisha Riham Warriors, ya Uganda na New Stars wa Burundi. Waganda ndio walikuwa wanaongoza awamu ya kwanza ya mchezo kwa vikapo 19 kwa 17 kabla ya umeme kukatika kwenye uwanja wa wizara ya michezo vijana na utamaduni.
Baada ya muda wa saa nzima hivi kabla ya shirika la maji na umeme Regideso kurejesha umeme. Timu hizo zilirejea uwanjani huku kila upande ukionyesha ushindani mzuri, lakini hata hivyo Vijana wa Uganda waliwashinda warundi kwa vikapo 93 kwa 69 huku kila upande ukionyesha mchezo mzuri.
Michuano hiyo inaendelea leo ambapo News Stars wanachuana na Vijana kutoka Tanzania.

HII NI WAZIMA AU UTOTO, JUSTIN BIEBER ANGALIA ANAVYO WATEMEA MATE MASHABIKI


Sijui ndio kulewa sifa au.

Justin Bieber amekuwa akionyesha tabia isio ridhisha dhidi ya mashabiki wake ambapo ukiangalia kwenye Video hii alivyokuwa akiwatemea mate mashabiki ambao walikuwa hotelini wakimsubiri, utakubaliana na mimi kwamba huenda kijana huyu amelewa sifa.

USAFIRI WA NDEGE WAWAKWAMISHA WANARIADHA WA KENYA KUELEKEA NCHINI URUSI


Wanariadha wa huko Kenya wameshindwa kusafiri jana kuelekea nchini Urusi kushiriki mashindano ya riadhaa ya dunia yatayo timua vumbi nchini humo kuanzia Agosti 10 hadi tarehe 18 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo safari za ndege kuelekea nje ya nchi hiyo ziliparaganyika baada ya ndege zote zilizokuwa kwenye orodha ya safari nchini humo hapo jana, kutakiwa kuwekwa mafuta.
Taarifa hii imesema sio wanariadha pekee waliokumbwa na dhahama hii bali pia wasafiri wote waliotakiwa kusafiri kwa ndege kuelekea nje ya taifa hilo.
Safari hizo za ndege ambazo zilitakiwa kufanyika jana, hatimaye zinafanyika leo ambapo wanariadha hao wameanza safari yao kuiwakilisha Kenya katika mashindano hayo ya riadha.

Jumatatu, 5 Agosti 2013

SHAZY KOOL HARERA APEWA SHAVU NCHINI UGANDA

Msanii wa Burundi anaekwenda na miondoko ya kitamaduni zaidi Shazy Kool Harera amepewa mualiko wa kushiriki kwenye Makala ya sita ya  tamasha  la Bayimba International Festival of the Arts, Kampala, Uganda.

Makala haya ya sita ya Tamasha hilo yamepangwa kutimua vumbi September 20 hadi 22 mwaka 2013 kwenye eneo la  Uganda National Cultural Centre jijini Kampala, nchini Uganda.

Shazy Kool pamoja na Bendi yake Ya Vumera Band watadumbwiza katika tamasha hilo litalo yaleta pamoja mataifa kadhaa kutoka katika ukanda wa Afrika.

Mbali na kudumbwiza katika matasha hilo, Shazy atapata furs aya kushirikiana na wasanii wa Uganda katika kufaanikisha tamasha hilo, na kuendesha mahojiano na vyombo vya habari vya nchini Uganda na vya kimataifa.

Akizungumza na Ikoh.biz, Shazy Kool amesema mipango yote imekamilika kuhakikisha wanashiriki katika tamasha hilo. Ametumia fursa hiyo kutowa shukrani za dhati kwa body ya waandalizi wa Makala haya ya sita ya tamasha la Bayumba na Fondation Bayumba. Shukran pia amezipeleka kwa mashabiki ambao wamekuwa kwenye mstari wa mbele katika kumpa sapoti kwenye safari yake hii ya Muziki.

Ikoh.biz hatuna budi kumpongeza Shazy Kool na kumtakia kila la kheri, lakini pia tunamtaka kuitumia vema fursa hii hadimu.

Alhamisi, 1 Agosti 2013

AMAMA MBABAZI WAZIRI MKUU WA UGANDA NA RAIS PAUL KAGAME WAONGOZA KATIKA MATUMIZI YA MTANDAO WA KIJAMII WA TWITTER


Kwa mujibu wa Utafiti ulioendeshwa na kituo cha Marekani cha Burson–Marsteller kuhusu matumizi ya mtandao wa kijamii wa Twitter dhidi ya viongozi 505 duniani, kwenye gazi ya marais, mawaziri wakuu, mawaziri wa mambo ya nje, na viongozi wa kidini.
Waziri mkuu wa Uganda Amama Mbabazi anaongoza duniani kwa kutumia mtandao huu wa kijamii wa Twitter hasa katika kushiriki mijadala na kutowa majibu katika mijadala inayotolewa, akifuatiwa na rais wa Rwanda Paul Kagame ambao wanamzidi mbali rais wa Marekani Barack Obama, licha ya kuwa na marafiki wanaozidi milioni 34.
Utafiti huo unaonyesha kuwa, kuongoza na idadi kubwa ya marafiki wengi sana kwenye mtandao huo wa kijamii wa Twitter sio kuwa na umaarufu, kwani wengi hawana mawasiliano na marafiki zao kama ilivyo kwa viongozi hao wanaongoza katika utafiti huu.
Hata hivyo Utafiti huu umeweka bayana orodha ya marais wa Bara la Afrika walio na umaharufu mkubwa kwenye mtandao huu wa kijamii wa Twitter, ikiwa ni pmoja na rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akifuatiwa na Uhuru Kenyatta rais wa Kenya, Moncef Marzouki rais wa Tunisia, Paul Kagame rais wa Rwanda anachukuwa nafasi ya nne akifuatiwa na Jakaya Mrisho Kikwete rais wa Tanzania kwenye nafasi ya tano.
Hao ni viongozi ambao wamejizolea umaarufu mkubwa sana kwenye mtandao huu wa kijamii wa Twitter.
Ripoti hii inaonyeshakuwa asilimia 71 ya viongozi wa bara la Afrika wapo kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, lakini maskitiko ni kwamba viongozi wengi wamekuwa wakitumia mtandao huu kwa ajili ya kampeni za uchaguzi na baada ya kuchaguliwa hawaonekani tena.