Vijana wa Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Burundi Intamba mu
Rugamba imefuzu kucheza michuano ya kombe la mataifa ya Afrika ya vijana
wanaocheza ligi za nyumbani CHAN inayo taraji kuipigwa Mwakani Januari na
Februari huko nchini Afrika Kusini, baada ya kuilaza Sudan kwa matuta.
Timu ya Taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba |
Wenyeji Vijana wa Sudan ndio waliokuwa wa kwanza kuliona
lango la Intamba Murugamba lilokuwa linalindwa na Arakaza Arthur katika kipindi
cha kwanza cha mchuano huo uliochezeka mbele ya mashabiki lukuki wa Sudan.
Vijana wa Intamba Mu Rugamba hawakukata tamaa hadi kwenye
dakika ya 50 ya mchezo, mshambuliaji Kaze Demunga Gilbert, alisawazisha bao
hilo na kuzidisha kasi ya mchezo na kuonekana kuwa ngumu katika kila pande,
kwani Intamba walionyesha nia ya kusindiria msumari, bila mafaanikio huku
wenyeji Sudani nao vilevile walijaribu kushambulia bila kupata kitu.
Hadi kipenga cha mwisho tumu hizo zilikuwa sare ya bao Moja
kwa Moja na hivo kulazimika kupiga matuta. Vijana wa Burundi walifaulu
kupachika Penalti 4 dhidi ya tatu za vijana wa Sudan.
Mchuano huu ilikuwa ni duru ya pili au marudio ambapo
duru ya kwanza ilifanyika jijini Bujumbura majuma mawili yaliopita, ambapo timu
hizo zililazimishana sare ya bao moja kwa moja.
Hongera sana kwa vijana wa Intamba mu Rugamba kurejesha hadi
ya mpira wa miguu nchini Burundi.