Milio ya risase imesikika Jumatatu hii Julay 29 mwaka 2013 saa kumi
asubuhi katika jela kuu la mpimba jijini Bujumbura. Duru katika eneo hilo
zaarifu kuwa walinzi wa jela hilo walivurumisha risase hewani kuwatawanya
wafungwa, baada ya kuzuka mtafaruku baina yao.
Chanzo cha mvutano huo kama ilivyoarifu duru katika eneo hilo ni baada
ya wafungwa viongozi kuorodhesha majina ya wagungwa ambao watahamishwa katika
jela nyingine ambapo kuna wafungwa waliopinga hatuwa hiyo na ndipo kuzuka
mvutano.
Hata hivyo duru nyingine zaarifu kuwa wafungwa wa chama cha FNL na wale
wa chama madarakani CNDD-FDD walishambuliana mapema leo asubuhi na hivo polisi
inayolinda jela hiyo ikalazimika kuwatanya kwa kufistuwa risase hewani.