Rais
wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela hii leo anasherekea
siku yake ya kuzaliwa akiwa hospitalini huku familia yake ikisema
afya ya kiongozi huyo inaimarika. sherehe
ambazo zinakwenda sanjari na miaka kumi na tano ya ndoa yake na Graca
Machel.
Mtoto wa kiongozi huyo
Zindzi Mandela amewaambia wanahabari mjini Johanesberg kuwa afya ya
baba yake inaendelea kuimarika na huenda akaruhusiwa wakati wowote.
Nelson Mandela na mkewe Graca Machel |
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya Afrika Kusini inasema kuwa
madaktari wanaomtibu mzee Mandela wamedhibitisha kuwa afya ya kiongozi
huyo inaendelea vizuri na huenda akaruhusiwa kutoka hospitali.
Taarifa kuhusu afya ya Mandela zinatolewa wakati huu ambapo taifa
hilo hii leo linafanya sherehe ya kukumbuka kuzaliwa kwa kiongozi
huyo anaetimiza miaka 95 hii leo.
Mbali
na wananchi wa Afrika Kusini ambao hii leo wanasherehekea siku hiyo,
dunia pia inaadhimisha siku hii ambayo inatambuliwa pia na Umoja wa
Mataifa kama siku ya Mandela 'Mandela Day'. Mzee Mandela
anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa hospitalini ambako amelazwa
kwa zaidi ya mwezi mmoja hivi sasa kutokana na kusumbuliwa na maradhi
Viongozi
mbalimbali wa kidini nchini Afrika Kusini wametoa wito kwa wananchi
kumuombea kiongozi huyo ili aweze kurejea kwenye hali yake ya
kawaida. Dunia inaadhimisha siku hii kwa wananchi kushiriki shughuli
za kijamii kwa dakika sitini na saba, huku rais Jackob Zuma
akisherekea siku hii kwa kendesha harambee ya kuchangia mfuko wa
Nelson Mandela.
Siku
kama ya leo inatambuliwa na Umoja wa Mataifa kama siku
ya Mandela ambapo ulimwengu mzima unatakiwa kuendesha shughuli za
kijamii kwa muda wa dakika 67, kuenzi miaka 67 ya harakati za mzee
Nelson Mandela.