Hivi karibuni kampuni ya Ikoh Multiservice, ikishirikiana na shirika la warundi waishio mjini Dubai iliandaa sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya uhuru wa Burundi, sherehe ambazo zilifanyika katika ukumbi wa Hotel Sheraton mjini Deira hapo Dubai. Kabla ya sherehe hizo kulikuwa na mashindano ya mpira wa miguu yaliozijumuisha timu mbili za warundi waishio jijini Dubai. Sherehe hizo zilianza kwa hotuba mbalimbali zilizotolewa na Muakilishi wa Warundi mjini Dubai iliofuatiwa na hotuba ya shukrani iliotolewa na mwenyekiti wa shirika la warundi waishio mjini Dubai. Msanii Yoya alipanda jukwaani baada ya kukatwa keki iliokuwa imeandaliwa kwa ajili ya sherehe hiyo. Watu waliokuwepo walivutiwa sana na burudani iliokuwa ikiendelea kabla ya kutamatika, ilikuwa fursa pia kwa wageni waalikwa mbalimbali kujitupa ukumbini kusakata Rumba.