Rais wa
Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso atamatisha ziara yake ya siku tatu nchini
Burundi.
Rais Sassou
Nguesso amezuru nchini Burundi ambapo pamoja na mwenyeji wake Pierre Nkurunziza
wameweka mashahada ya maua kwenye makaburi kwanza ya kinara wa Uhuru wa Burundi
mwanamfalme Louis Rwagasore, pamoja na
Kinara wa Demokrasia hayati Melchior Ndadaye.
Baada ya
hapo viongozi hao wawili walitembelea kiwanda kinacho tengeneza majani ya Chai
cha Teza na kuzuru miradi mbalimbali ya maendeleo iliopo katika mikoa ya
Kayanza na Ngozi kaskazini mwa Burundi.
Lengo hasa
la ziara hiyo ilikuwa ni kudumisha uhisiano bora uliopo bain aya nchi hizo
mbili.
Rais Sassou
Nguesso amepongeza juhudi ya maendeleo ilipogwa nchini Burundi tangu kumalizaka
kwa vita vya wenye kwa wenyewe miaka kadhaa iliopita.