Majambazi
waliokuwa kwenye pikipiki walijaribu kumuibia bila mafaanikio
mkurugenzi wa utawala na fedha wa chuo kikuu cha kibinafsi nchini Burundi cha Universite
Espoir d'Afrique. Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika eneo la tukio,
majambazi hao walilenga kuiba kitita kinacho lingana na Dola za
Marekani elfu ishirini (20.000) pamoja na franka za Burundi milioni
kumi na saba (17.000.000).
Jiji la Bujumbura |
Jambazi
alieuawa ambaye anasadikiwa kuwa ndiye alieye kuwa kiongozi wa genge
hilo ni afisaa wa jeshi mwenye cheo cha Kepteni ambaye hivi karibu
alirejea kutoka nchini Somalia ambako alikuwa katika Operesheni ya
kulinda amani AMISOM.
Kikosi
cha Brigade Maalum Brigade Special ndicho ambacho kiliingilia kati
tukio hilo lilitokea Julay 15 saa tatu usiku kwenye barabara numbari
3(RN3) eneo la tarafa ya Kinindo kwenye barabara inayoelekea Rumonge
kusini mwa Burundi.
Duru
zaidi zaeleza kuwa huenda dereva wa gari alilokuwa akisafiria
mkurugenzi wa chuo hicho anahusika katika kutowa taarifa kwa njia ya
simu kuhusu barabara watayo tumia. Mkurugenzi huyo alikuwa makini na
kutowa taarifa kwa polisi ilioingilia kati mapema baada ya
kushambuliana kwa risase na wahalifu hao.