Raia
mmoja wa Marekani mwenye asili ya Rwanda amehukumiwa kifungo cha
miaka kumi jela nchini Marekani na kupoteza uraia wake wa Marekani
kwa ajili ya kuficha jukumu lake katika mauaji ya kimbari ya nchini
Rwanda mwaka 1994
Beatrice Munyenyezi |
Beatrice
Munyenyezi, mwenye umri wa miaka 43, alishtakiwa tangu Juni 2010 na
majaji shirikisho katika New Hampshire (kaskazini-mashariki) ili
kupata uraia wake wa Marekani kinyume cha sheria, na kuficha jukumu
lake katika mauaji ya kimbari ya 1994.
Imethibitika
kwamba mshtakiwa Haikuwa mtazamaji tu binafsi bali alishiriki katika
mauaji ya wanaume, wanawake na watoto kwa sababu tu wao waliitwa
Watutsi." Alisema Jaji Stephen McAuliffe wakati akitowa hukumu.
Beatrice
Munyenyezi alikuwa anaeshi jijini Butare kusini mwa Rwanda, wakati wa
mauaji ya halaiki awali alikuwa ameficha jukumu lake katika chama
tawala zama hizo cha MRND na kundi la vijana la chma hicho la
“Interahamwe”ambapo alikuwa mwanachama.
Katika
muktadha huu, mshitakiwa alishiriki, kusaidiana kuunga mkono vitendo
vya mateso na mauaji ya Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari, ilisema
taarifa hiyo, na kuongeza kwamba alihukumiwa kifungo cha miaka 10
jela.
Wakati
wa kesi yake, ambayo ilidumu siku 12, mashahidi waliiambia mahakama
jinsi mtuhumiwa alivyokuwa akikagua katika kizuizi jijini Butare na
kuamua nani apite, na nani akamatwe. Kwa mujibu wa hati ya kukamatwa,
mama wa mumewe alikuwa kiongozi katika serikali.
Aliondoka
nchini Rwanda Julai 1994 na kuelekea nchini Kenya, ambapo aliomba
hadhi ya ukimbizi nchini Marekani. Alisema hajawahi kuwa mwanachama
wa chama chochote kile cha kisiasa. Akiulizwa suala maalum la kama
aliwahi "kushiriki katika mauaji au kumjeruhi mtu tangu Aprili
1, 1994," alijibu "hapana."