Jumanne, 30 Julai 2013

JESHI LA BURUNDI LAENDELEA KUKANUSHA UWEPO WA VIKOSI VYAKE KATIKA ARDHI YA DRCONGO

Msemaji wa jeshi la Burundi Kanali Gaspard Baratuza amesema hakuna Ujumbe rasmi wa vikosi vya Burundi katika ardhi ya DRCongo. Hii inakuja baada ya wananchi wa Tarafa ya Uvira Kusini mwa jimbo la Kivu ya Kusini, mpakani mwa Burundi kulaani vitendo viovu vinavyo tekelezwa na wanajeshi wa Burundi.


Habari kutoka Uvira zaarifu kuwa wanajeshi wa Burundi wamekwenda katika eneo hilo kuwasaka wapiganaji waasi wa FNL. 

Gaspard Baratuza amesisitiza kuwa jeshi la Burundi haliwezi kuingia katika ardhi ya DRCongo bila idhini ya viongozi wa taifa hilo.

Msemaji wa serikali ya Kinshasa Lamberd Membe Omalanga amethibitisha taarifa ya jeshi la Burundi kwamba na kuongeza kuwa hakuna mkataba wowote ambao umesainiwa na Burundi. Makubaliano yalipo pekee yanahusu idara ya Ujasusi.

Jumatatu, 29 Julai 2013

MILIO YA RISASE YASIKIKA KATIKA JELA KUU LA MPIMBA MAPEMA ASUBUHI JULAY 29

Milio ya risase imesikika Jumatatu hii Julay 29 mwaka 2013 saa kumi asubuhi katika jela kuu la mpimba jijini Bujumbura. Duru katika eneo hilo zaarifu kuwa walinzi wa jela hilo walivurumisha risase hewani kuwatawanya wafungwa, baada ya kuzuka mtafaruku baina yao.
Chanzo cha mvutano huo kama ilivyoarifu duru katika eneo hilo ni baada ya wafungwa viongozi kuorodhesha majina ya wagungwa ambao watahamishwa katika jela nyingine ambapo kuna wafungwa waliopinga hatuwa hiyo na ndipo kuzuka mvutano.


Hata hivyo duru nyingine zaarifu kuwa wafungwa wa chama cha FNL na wale wa chama madarakani CNDD-FDD walishambuliana mapema leo asubuhi na hivo polisi inayolinda jela hiyo ikalazimika kuwatanya kwa kufistuwa risase hewani.

RAIS WA CONGO BRAZAVILLE ATAMATISHA ZIARA YAKE YA KIKAZI NCHINI BURUNDI

Rais wa Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso atamatisha ziara yake ya siku tatu nchini Burundi.
Rais Sassou Nguesso amezuru nchini Burundi ambapo pamoja na mwenyeji wake Pierre Nkurunziza wameweka mashahada ya maua kwenye makaburi kwanza ya kinara wa Uhuru wa Burundi  mwanamfalme Louis Rwagasore, pamoja na Kinara wa Demokrasia hayati Melchior Ndadaye.

Baada ya hapo viongozi hao wawili walitembelea kiwanda kinacho tengeneza majani ya Chai cha Teza na kuzuru miradi mbalimbali ya maendeleo iliopo katika mikoa ya Kayanza na Ngozi  kaskazini mwa Burundi.

Lengo hasa la ziara hiyo ilikuwa ni kudumisha uhisiano bora uliopo bain aya nchi hizo mbili.


Rais Sassou Nguesso amepongeza juhudi ya maendeleo ilipogwa nchini Burundi tangu kumalizaka kwa vita vya wenye kwa wenyewe miaka kadhaa iliopita.  

MANAJA ABDALLAH SHOKOLO ALMAHARUFU GOOGLE AONGELEA MIPANGO YA IKOH MULTISERVICE

Katika kipindi maharufu sana jijini Bujumbura kinacho rushwa na Radio ya Umma RPA inayo sikika nchini Burundi na duniani kote kupitia mtandao wa Internet, manaja wa Kampuni ya Ikoh Multiservice Abdallah Shokoloko a.k.a Google amekuwa mgrni katika kipindi cha East African Music kinacho ongozwa na mtangazaji Aisha Amuri Ndimubandi.

Google, amezungumzia mipango mbalimbali ya kampuni hiyo, na sherehe ya miaka 51 ya Uhuru wa Burundi iliofanyika katika nchi za famle za kiarabu mjini Dubai.


VIJANA WA INTAMBA MU RUGAMBA WAREJESHA HADHI YA MPIRA WA MIGUU NCHINI BURUNDI BAADA YA KUFUZU MICHUANO YA CHAN HUKO AFRIKA KUSINI MWAKANI

Vijana wa Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Burundi Intamba mu Rugamba imefuzu kucheza michuano ya kombe la mataifa ya Afrika ya vijana wanaocheza ligi za nyumbani CHAN inayo taraji kuipigwa Mwakani Januari na Februari huko nchini Afrika Kusini,  baada ya kuilaza Sudan kwa matuta.

Timu ya Taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba

Wenyeji Vijana wa Sudan ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la Intamba Murugamba lilokuwa linalindwa na Arakaza Arthur katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo uliochezeka mbele ya mashabiki lukuki wa Sudan.

Vijana wa Intamba Mu Rugamba hawakukata tamaa hadi kwenye dakika ya 50 ya mchezo, mshambuliaji Kaze Demunga Gilbert, alisawazisha bao hilo na kuzidisha kasi ya mchezo na kuonekana kuwa ngumu katika kila pande, kwani Intamba walionyesha nia ya kusindiria msumari, bila mafaanikio huku wenyeji Sudani nao vilevile walijaribu kushambulia bila kupata kitu.

Hadi kipenga cha mwisho tumu hizo zilikuwa sare ya bao Moja kwa Moja na hivo kulazimika kupiga matuta. Vijana wa Burundi walifaulu kupachika Penalti 4 dhidi ya tatu za vijana wa Sudan.

Mchuano huu ilikuwa ni duru ya pili au marudio ambapo duru ya kwanza ilifanyika jijini Bujumbura majuma mawili yaliopita, ambapo timu hizo zililazimishana sare ya bao moja kwa moja.

Hongera sana kwa vijana wa Intamba mu Rugamba kurejesha hadi ya mpira wa miguu nchini Burundi.

Alhamisi, 18 Julai 2013

PICHA MBALIMBALI ZA SHEREHE YA KUADHIMISHA MIAKA 51 YA UHURU WA BURUNDI HUKO DUBAI


Sehemu ya kwanza ya Kamati
Sehemu ya pili ya kamati
Balozi mdogo wa Burundi huko Dubai
                                      
Sehemu ya Wageni waalikwa
Balozi mdogo wa Burundi huko Dubai

Baadhi ya waliohudhuria

Sehemu ya waliohudhuria
Msanii Yoya akifanya yake jukwaani
Msanii Yoya akitowa Burudani

Watu wakiserebuka
Keki ya miaka 51 ya Uhuru wa Burundi

Vijana wakifurahia Burudani

Rais wa Shirika la Warundi waishio Dubai akigawa keki kwa Wageni waheshimiwa waalikwa
Sehemuu ya Wageni waheshimiwa waalikwa

Warembo pia walikuwepo
Rais wa shirika la warundi wa Dubai akisakata Rumba
Huyu bwana naye alikuwepo kunogrsha sherehe
wakati wa kukatwa Keki na Balozi mdogo huko Dubai akiambatana na mkewe na rais wa shirika la warundi wa Dubai



DUNIA YAADHIMISHA SIKU YA MANDELA


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela hii leo anasherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa hospitalini huku familia yake ikisema afya ya kiongozi huyo inaimarika. sherehe ambazo zinakwenda sanjari na miaka kumi na tano ya ndoa yake na Graca Machel.
Mtoto wa kiongozi huyo Zindzi Mandela amewaambia wanahabari mjini Johanesberg kuwa afya ya baba yake inaendelea kuimarika na huenda akaruhusiwa wakati wowote.
Nelson Mandela na mkewe Graca Machel
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya Afrika Kusini inasema kuwa madaktari wanaomtibu mzee Mandela wamedhibitisha kuwa afya ya kiongozi huyo inaendelea vizuri na huenda akaruhusiwa kutoka hospitali. Taarifa kuhusu afya ya Mandela zinatolewa wakati huu ambapo taifa hilo hii leo linafanya sherehe ya kukumbuka kuzaliwa kwa kiongozi huyo anaetimiza miaka 95 hii leo.

Mbali na wananchi wa Afrika Kusini ambao hii leo wanasherehekea siku hiyo, dunia pia inaadhimisha siku hii ambayo inatambuliwa pia na Umoja wa Mataifa kama siku ya Mandela 'Mandela Day'. Mzee Mandela anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa hospitalini ambako amelazwa kwa zaidi ya mwezi mmoja hivi sasa kutokana na kusumbuliwa na maradhi

Viongozi mbalimbali wa kidini nchini Afrika Kusini wametoa wito kwa wananchi kumuombea kiongozi huyo ili aweze kurejea kwenye hali yake ya kawaida. Dunia inaadhimisha siku hii kwa wananchi kushiriki shughuli za kijamii kwa dakika sitini na saba, huku rais Jackob Zuma akisherekea siku hii kwa kendesha harambee ya kuchangia mfuko wa Nelson Mandela.

Siku kama ya leo inatambuliwa na Umoja wa Mataifa kama siku ya Mandela  ambapo ulimwengu mzima unatakiwa kuendesha shughuli za kijamii kwa muda wa dakika 67, kuenzi miaka 67 ya harakati za mzee Nelson Mandela.

Jumatano, 17 Julai 2013

JESHI LA DRCONGO LASEMA KUWA LIMEWASAMBARATISHA WAASI WA M23

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC limeendelea kukabiliana na wapiganaji waasi wa kundi la M23 mashariki mwa nchi hiyo siku mbili baada ya kuuawa kwa watu 130 wa kundi hilo. Msemaji wa jeshi la DRC, Kanali Olivier Hamuli amedhibitisha wanajeshi wake kukabiliana na waasi jirani na maeneo ya mji wa Goma wakati huu ambapo jeshi la nchi hiyo limeapa kuwasambaratisha wapiganaji hao.

Wanajeshi wa Congo wakielekea kwenye uwanja wa mapambano

Hayo yanajiri wakati, balozi wa DRC kwenye Umoja wa Mataifa UN ameendelea kuishutumu nchi ya Rwanda kwa kuendelea kuwafadhili kwa silaha waasi wa M23 na kuongeza kuwa wengi wa wapiganaji waliokamatwa nchini humo ni kutoka jeshi la Rwanda. Umoja wa Mataifa umevionya vikosi vyake vilivyoko mashariki mwa nchi hiyo na hasa vile vikosi maalumu vilivyopelekwa nchini humo kukabiliana na makundi ya waasi, kuwa tayari muda wote kutokana na kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano.

Kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa kilichopelekwa nchini humo bado hakijaanza kazi yake lakini huenda kikaruhusiwa hivi karibuni kuanza operesheni ya kuwakabili waasi hao. Waasi wa M23 ambao waliwahi kuushikilia mji wa Goma kwa siku kumi mwaka jana kabla ya kuondoka kutokana na shinikizo toka jumuiya ya kimataifa lilianza tena harakati zake za kutaka kutejea kwenye mji huo na ndio chanzo cha kuzuka kwa mapigano hayo.

Msemaji wa kundi la M23 Amani Kabasha amesemalicha ya jeshi lake kuelezwa kuzidiwa na wanajeshi wa Serikali yeye ameendelea kukanusha kuuawa kwa askari wake huku akisisitiza kuwa wanayashikilia maeneo ambayo awali walikuwa wanayakalia. Msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende amesisitiza jeshi la nchi hiyo kuwazidi nguvu waasi wa M23 na kwamba hivi karibuni watatangaza ushindi dhidi ya kundi hilo ambalo sasa linaelezwa kusaidiwa pia na wapiganaji wa Al-Shabab toka nchini Somali.

RAIA WA MAREKANI MWENYE ASILI YA RWANDA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIKA 10 KUTOKANA NA KUFICHA JUKUMU LAKE KATIKA MAUAJI YA KIMBARI MWAKA 1994


Raia mmoja wa Marekani mwenye asili ya Rwanda amehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela nchini Marekani na kupoteza uraia wake wa Marekani kwa ajili ya kuficha jukumu lake katika mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda mwaka 1994
Beatrice Munyenyezi 
Beatrice Munyenyezi, mwenye umri wa miaka 43, alishtakiwa tangu Juni 2010 na majaji shirikisho katika New Hampshire (kaskazini-mashariki) ili kupata uraia wake wa Marekani kinyume cha sheria, na kuficha jukumu lake katika mauaji ya kimbari ya 1994.
Imethibitika kwamba mshtakiwa Haikuwa mtazamaji tu binafsi bali alishiriki katika mauaji ya wanaume, wanawake na watoto kwa sababu tu wao waliitwa Watutsi." Alisema Jaji Stephen McAuliffe wakati akitowa hukumu.
Beatrice Munyenyezi alikuwa anaeshi jijini Butare kusini mwa Rwanda, wakati wa mauaji ya halaiki awali alikuwa ameficha jukumu lake katika chama tawala zama hizo cha MRND na kundi la vijana la chma hicho la “Interahamwe”ambapo alikuwa mwanachama.
Katika muktadha huu, mshitakiwa alishiriki, kusaidiana kuunga mkono vitendo vya mateso na mauaji ya Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari, ilisema taarifa hiyo, na kuongeza kwamba alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.
Wakati wa kesi yake, ambayo ilidumu siku 12, mashahidi waliiambia mahakama jinsi mtuhumiwa alivyokuwa akikagua katika kizuizi jijini Butare na kuamua nani apite, na nani akamatwe. Kwa mujibu wa hati ya kukamatwa, mama wa mumewe alikuwa kiongozi katika serikali.
Aliondoka nchini Rwanda Julai 1994 na kuelekea nchini Kenya, ambapo aliomba hadhi ya ukimbizi nchini Marekani. Alisema hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote kile cha kisiasa. Akiulizwa suala maalum la kama aliwahi "kushiriki katika mauaji au kumjeruhi mtu tangu Aprili 1, 1994," alijibu "hapana."










Jumanne, 16 Julai 2013

JAMBAZI MMOJA AUAWA KATIKA SHAMBULIO LA RISASE, WATATU WAJERUHIWA NA WENGINE WATATU WATIWA NGUVUNI

Majambazi waliokuwa kwenye pikipiki walijaribu kumuibia bila mafaanikio mkurugenzi wa utawala na fedha wa chuo kikuu cha kibinafsi nchini Burundi cha Universite Espoir d'Afrique. Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika eneo la tukio, majambazi hao walilenga kuiba kitita kinacho lingana na Dola za Marekani elfu ishirini (20.000) pamoja na franka za Burundi milioni kumi na saba (17.000.000).

Jiji la Bujumbura
Jambazi alieuawa ambaye anasadikiwa kuwa ndiye alieye kuwa kiongozi wa genge hilo ni afisaa wa jeshi mwenye cheo cha Kepteni ambaye hivi karibu alirejea kutoka nchini Somalia ambako alikuwa katika Operesheni ya kulinda amani AMISOM.

Kikosi cha Brigade Maalum Brigade Special ndicho ambacho kiliingilia kati tukio hilo lilitokea Julay 15 saa tatu usiku kwenye barabara numbari 3(RN3) eneo la tarafa ya Kinindo kwenye barabara inayoelekea Rumonge kusini mwa Burundi.

Duru zaidi zaeleza kuwa huenda dereva wa gari alilokuwa akisafiria mkurugenzi wa chuo hicho anahusika katika kutowa taarifa kwa njia ya simu kuhusu barabara watayo tumia. Mkurugenzi huyo alikuwa makini na kutowa taarifa kwa polisi ilioingilia kati mapema baada ya kushambuliana kwa risase na wahalifu hao.

Alhamisi, 11 Julai 2013

YOYA JAMAL ALIVYO MILIKI JUKWAA HUKO DUBAI

Hivi karibuni kampuni ya Ikoh Multiservice, ikishirikiana na shirika la warundi waishio mjini Dubai iliandaa sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya uhuru wa Burundi, sherehe ambazo zilifanyika katika ukumbi wa Hotel Sheraton mjini Deira hapo Dubai. Kabla ya sherehe hizo kulikuwa na mashindano ya mpira wa miguu yaliozijumuisha timu mbili za warundi waishio jijini Dubai. Sherehe hizo zilianza kwa hotuba mbalimbali zilizotolewa na Muakilishi wa Warundi mjini Dubai iliofuatiwa na hotuba ya shukrani iliotolewa na mwenyekiti wa shirika la warundi waishio mjini Dubai. Msanii Yoya alipanda jukwaani baada ya kukatwa keki iliokuwa imeandaliwa kwa ajili ya sherehe hiyo. Watu waliokuwepo walivutiwa sana na burudani iliokuwa ikiendelea kabla ya kutamatika, ilikuwa fursa pia kwa wageni waalikwa mbalimbali kujitupa ukumbini kusakata Rumba.

MAMA WA MSANII NGULI WA HIP HOP NCHINI TANZANIA PRO JAY AFARIKI DUNIA

 Msanii nguli wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania Joseph Haule a.k.a Professor Jay amempoteza mama yake mzazi Rosemary Majanjara katika ajali ya gari iliotokea maeneo ya Mbezi mwisho huko nchini Tanzania. Ikoh Multiservice tunatoa salam za rambirambi kwa mkongwe wa Hip Hop na kwa ndugu wa familia wa karibu
 
 

HAWA NDIO WAREMBO WA BONGO WALIONASWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI

Video Queen wa Bongo Fleva Agnes Gerald Masogange anadaiwa kukamatwa nchini Afrika Kusini akiwa na Mrembo Mellisa Edward wakiwa na  kilo mia moja na hamsini ya madawa ya kulevya. siku chache kabla ya kumatwa kwake Video Queen Agnes Masogange aliweka picha hii kwenye mtandao wa kijamii wa Instangram. hivi kama ukisoma au kuona picha hii kisha siku chache baadae unasikia taarifa hii ya kukamatwa kwa wasichana hawa inakupa picha gani mdau?

              Melissa Edward
Agnes Gerald Masogange

Jumatano, 10 Julai 2013

YOYA ALIVYO ENJOY SAFARI YAKE YA DUBAI

Hivi karibuni msanii Yoya Jamal alikuwa na ziara ndefu katika nchi za falme za kiarabu jijini Dubai ambako alikuwa amekwenda kuandaa mazingira ya kurikodi video ya wimbo Wake mpya ambao ameahidi kuachia hivi karibuni.

  Yoya Jamal akiendelea ku Enjoy katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dubai