Jumatano, 10 Aprili 2013

YOYA ANAKUJA KITAMADUNI ZAIDI

 Msanii mwenye mvuto na mwenye hadhi ya kipekee nchini Burundi ambae anafanya vizuri kwa sasa nchini humu Yoya Jamal almaharufu "Yoya" ameingia Studio Ikoh Multiservice kurikodi wimbo wake mpya chini ya producer Botchoum utaokuja kwa jina la "Haguruka" ikimaanisha"Simama" kwa lugha iliotukuka ya Kiswahili.

Yoya akiwa studioni huku Botchoum akifanya mambo
akizungumza na Ikoh.biz, Yoya amesema kwamba ni mara ya kwanza anatumia style ya kitamaduni na anataraji kuwa, wimbo huo utafanya vizuri baada ya kushirikiana na producer mahiri ambae amekuwa na ubunifu wa hali ya juu.

Producer Botchoum akichanganya sauti
Wimbo huo "Haguruka" unawatolea wito vijana wa Burundi kuwa wabunifu zaidi katika kupanga mbinu za kujiendeleza wenyewe pasina kutegemea kazi zinazo tolewa na serikali, na kwamba hakuna kisicho wezekana ikiwa kuna nia na bidii za kutosha.

Yoya amedokeza kwamba wimbo huu "Haguruka" utakuwa katika orodha ya nyimbo ambazo zita beba album yake ya kwanza ambayo amethibitisha kwamba itakuwa hewani kabla ya mwaka huu kumalizika.

Yoya Jamal akiwa katika pozi
Nyimbo kadhaa za msanii huyu mwenye mvuto wa kipekee ambazo zimekubalika na kutikisa jiji la Bujumbura ni pamoja na "Igiturire" wimbo ambao ulimsababishia kupata tuzo la shirika linalopiga vita rushwa nchini Burundi OLUCOME.

mwaka uliopita Yoya alitoka na kibao chake "Warahemutse" kibao ambacho kili konga nyoyo za wapenzi wengi wa muziki baada ya kuguswa na historia ilio beba kibao hicho.