Bi kidude anaye kadiriwa kuwa na umri wa miaka 100 alikuwa maharufu sana hasa kutokana na umri wake mkubwa lakini pia uwezo wa kumudu jukwaa ipasavyo anapotumbwiza halaiki ya watu.
Kwa mujibu wa mpwa wa Bi Kidude Baraka Abdallah Baraka, shangazi yake alikuwa anasumbuliwa na maradhi aina mbalimbali ikwemo kisukari, mapafu kuungua kutokana na sigara, Kongosho na chango.
Bibi Kidude mmoja kati ya waimbaji maarufu wa muziki wa asili alianza kujishuhgulisha na fani ya muziki mnamo mwaka 1920 akiwakilisha vyema kueneza utamaduni na muziki visiwani Zanzibar na nje ya Zanzibar.
Shughuli za mazishi zimepangwa kufanyika kesho Alhamisi huko huko visiwani Zanzibar