Mike Basuzwa ni
msanii wa Burundi aliejichimbia makazi nchini Afrika Kusini katika jiji la Cape
Town eneo kunako itwa Sea Point na ambae anaendelea ku komaa kwenye game licha
ya kujishughulisha na kazi nyingine mbali na Muziki.
Mike Basuzwa ni
mmoja kati ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi la G.O.N chini ya uongozi wa
msanii mkongwe katika game la muziki wa kizazi kipya, Baby G.
Akizungumza mawili
matatu na ikoh.biz, Mike Basuzwa amesema kwas asa anajiandaa kuingia studio
kutengeneza wimbo mpya alioshirikishwa na msani imwingine kutoka Lubumbashi
nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, track itayo kuja kwa jina la Fadher
G, kabla ya kuanza harakati za kutengeneza video hiyo chini ya Producer Keshy
Video Lab.
Akiulizwa kuhusu
mtazamo wake juu ya Muziki wa Burundi na wa vijana wa Afrika Kusini, Mike
Basuzwa amesema Muziki wa vijana wa Afrika Kusini upo juu zaidi, kiasi cha
kuupimanisha na muziki wa Ulaya, kwani heshima, sheria zinafanya kazi, wasanii
wanapata haki yao. Lakini kwa upande wa wasanii wa Burundi wa kizazi kipya
ambao wanafanya muziki nchini Afrika Kusini, msanii huyo amesema kwa upande huo
afadhali Burundi kwakuwa kuna mashabiki wengi wanaoupenda muziki wa kizazi
kipya.
Akiendelea
kulizungumzia hilo Mike Basuzwa amesema sio rahai msanii kuvuma ukiwa ungenini,
inabidi kujituma na kufanya kazi kwa bidii, ili kufikia kiwango cha juu.
Mike Basuzwa
ameendelea kusema kuwa licha ya kwamba hajabahatikiwa kupata mafaanikio yoyote
kupitia muziki, bado hajachoka kwakuwa safari bado ni ndefu anaendelea kutia
matumaini kwamba ipo siku ataeshi kwa kutegemea Muziki kwakuwa hatuwa
alioifikia ni ya kuridhisha
Akiulizwa kuhusu
kitu ambacho hatokisahau tangu alipoingia katika game la muziki, Mike Basuzwa
amesema hatosahau kamwe vurugu walizozifanya wakati akiwa na ma chiz wake wa
kundi la G.O.N alikoanzia musiki pamoja na Baby G ambaye bado yupo Buja,
Kiminikis ambae kwa sasa yupo Tanzania, na Taz Mas ambapo wote kwa sasa kila mmoja
yupo nchi tofauti na mwingine.
Mike Basuzwa
anazungumzia wimbo wake wa kwanza katika kundi hilo la G.O.N uliobeba jina la ni
‘Soo ‘ambapo anasema kwake ni ukumbusho mkubwa sana ambao hatosahau
maishani mwake.