Kwa muda mrefu kumekuwa na kilio kisichokoma kwa wasanii wsa Burundi kuomba serikali iwalindie kazi zao, kwani wamekuwa wakifanya kazi lakini wanaonufaika na matunda ya kazi zao ni watu wengine ambao hu kopi kazi zao na kujipatia pesa bila hata hivyo kugharimu chochote.
hili lina dhihirika katika kila kona ya nchi nyimbo za wasanii zinachezwa sana, lakini ukiwauliza wanaozicheza wapi wamezipata, inakuwa ngumu kueleza kwani wengi huzipata kwa njia isiokuwa halali ingawaje baadhi hupokea kutoka kwa wasanii wenyewe
Serikali kupitia wizara ya michezo vijana na utamaduni iliunda ofisi ya ulinzi wa kazi za wasanii na watunzi tangu mwezi Juni mwaka 2012 ingawaje shughuli za uundwaji wa taasi hiyo zilianza tangu mwaka 2011 wakati wa uongozi wa wizara hiyo wa Jean Jacques Nyenimigabo ambapo kabla ya kuondoka kwenye wizara hiyo aliwatolea wito viongozi tawala kuhamasisha ili watunzi na wasanii waorodheshe kazi zao kwenye taasisi hiyo iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu na gamu na wasanii pamoja na watunzi mbalimbali nchini.
Akizungumza na Ikoh biz, mkurugenzi wa taasisi hiyo, Donatien Niyungeko amesema, wanaendelea na harakati za kuhamasisha wasanii ikiwa ni hatuwa moja kubwa katika kufikia malengo muhimu ya ulinzi wa kazi zao, kwsani ameendelea kusema itakuwa vigumu serikali ilinde kazi hewa, hivyo kuna umuhimu kujuwa kana kwamba kweli kazi hii ni ya msanii huyo na labda imefayiwa kopi na huyo na sheria hapa zinafuata mkondo wake.
Mkurugenzio huyo ameimbia Ikoh Biz kwamba wasanii wengi wamekuwa wakija kuomba wapewe muelezoi kuhusu taasisi ambayo ipo kwa ajili yao.
Katika kutamatisha Donatien Niyungeko amesema ataeashangaa wasanii ambao watanedelea kuomba kiupitia vyombo mbalimbali ya habari nchini Burundii wapewe haki zao wakati hawajihamasishi kujulisha kazi zao.
Kwa hatuwa hii mabadiliko yanahitajika katika kila nyanja kuhakikisha msanii anakula kutokana na jasho lake, lakini pia mabadiliko yanahitajika katika kazi za wasanii kuwa makini katika kutengeneza kazi zenye kukidhi viwango.