Producer mahiri wa video wa kampuni ya Ikoh Multiservice Gueraman anazuru jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi iliomkutanisha na ma Producer wa Tanzania na kuzungumzia kuhusu maendelea ya muziki wa Burundi.
Akiongea na Ikoh.biz, Gueraman amesema amepata fursa ya kutembelea studio mbalimbali na kukutana na ma Producer wa video wa nchini Tanzania, na kubadilishana maujanja kuhusu kutengeneza video zenye viwango.
Gueraman amesema amenufaika sana na ziara hiyoya wiki moja katika jiji la Dar Es Salaam ambapo amehidi kufanya vizuri zaidi katika kazi yake baada ya kugundua mambo mengi ambayo amesema wenzetu wanayo tumia katika kutengeneza video.
Mbali na hayo Gueraman amezungumzia pia changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo katika kutekeleza kazi yao, na kuongeza kwamba la muhimu ni ma meneja au wale wanaowasimamia wasanii kugharamia vya kutosha video za wasanii badala ya kubania baadhi ya mambo ambayo amesema ni ya muhimu katika kurikodi picha za video.
Akizungumzia baadhi ya changamoto, Gueraman amesema huwa inatokea mara nyingi sehemu ya kurikodia picha inakosekana dakika za mwisho, na wahusika kuamua kuchukuwa picha katika maeneo ambayo hayana mandhari mazuri, kwa kuhofia gharama.
Amewatolea wito wasanii na wasimamizi wao kugharamia video zao ili ziwe na viwango vya kutosha na kuweza kushindanishwa kimataifa.