Jumanne, 2 Aprili 2013

BRARUDI YAKUSANYA MILLIONI 30 KATIKA TAMASHA LA HARAMBEE KWA WAATHIRIKA WA SOKO KUU

Kiwanda kinachotengeneza vinjwaji nchini Burundi cha Brarudi kimekusanya takriban Franka za Burundi Millioni thalathini katika tamasha LA pasaka liloandaliwa kwa ajili ya kukusanya fedha zitazo changia kwa waathirika wa soko kuu la jijini Bujumbura.

Wapenzi wa Muziki na Burudani walijitokeza kwenye uwanja wa mpira wa shule la Lycee Nyakabiga, Zamani EFI/Nyakabiga hapo zamani wakati wa siku kuu ya Pasaka Machi 31 kushuhudia burudani iliotolewa na wasanii wa Burundi ambao walikuwa wamejiandaa vya kutosha kuhakikisha wanatowa Burudani inayo ridhisha.











































Wakati Burudani ikiendelea Mkurugenzi mkuu wa Brarudi Maarten Schuurman alijitokeza na kutowa shukrwani za dhati kwa waliohudhuria tamasha hilo na wasanii waliokubali kushiriki bila pengamizi lakini pia waandishi wa habari ambao waliendesha matangazo kuhakikisha watu wengi wanahamasishwa. Mkurugenzi huyo ametumia fursa hiyo kutangaza kiwango cha pesa kilichokusanywa ambacho kilifikia Franka za Burundi millioni thalatini.

Upande wake Mkurugenzi mkuu wa shirika la wafanyabiashara na viwanda CFCIB Christian Nkengurutse baada ya kukabidhiwa hundi hiyo ya Faranga za Burundi millioni thalathini(30 Millions de FBU) amepongeza kiwanda hicho huku akiwahakikishia waliokuwepo kwamba hundi hiyo itawafikia wahusika bila shaka kupitia shirika “Burundi Bwacu” linalo saidia waliokumbwa na jinamizi la kuunguliwa na bidhaa zao katika soko kuu jijini Bujumbura mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu wa 2013.

Wadadisi wa maswala ya Muziki wanasema kwamba Brarudi imetowa changamoto kubwa kwa wanaoandaa maonyesho ya muziki jijini Bujumbura baada ya kurekebisha kasoro ambazo zilikuwa zikishuhuduwa hususan kuhusu vyombo, sauti, jukwaa(Podium) msongamano mlangoni na mengi mengi.