Jumanne, 30 Aprili 2013

RALLY JOE KUANDAA WIMBO WAKE MPYA CHINI YA PRODUCER BOTCHOUM


Studio Ikoh Multiservice itampokea studioni msanii wa mwaka, Rally Joe ambae atakuja ku rikodi wimbo wake mpya chini ya Producer Botchoum.

Rolly Joe msanii ambae anafanya vizuri kwa sasa nchini Burundi baada ya kujinyakulia tuzo kadhaa mwaka jana likiwemo tuzo la Primusic, lililomfikisha hadi Nairobi nchini Kenya ambako alijiunga na Legendary wa muziki wa Burundi Jean Pierre Nimbona “Kidum” na kutengeneza wimbo wa pamoja "Impanuro" ikimaanisha ushauri, na unaofanya vizuri kwa sasa.

Rally Joe amesema atakuwa Gitega katika siku kuu ya wafanyakazi ya Mei Mosi(1.5.2013) siku ya Jumatano, ambako atatowa Burudani katika Mkoa huo wenye kuwa na wapenzi wengi wa muziki.

Baada ya harakati hizo ndipo ataingia studio Ikoh Multiservice ku rikodi wimbo wake mpya, huku akiahidi wapenzi wa muziki kukaa mkao wa kula

R.FLOW AINGIA STUDIO "IKOH MULTISERVICE" KURIKODI WIMBO WAKE MPYA

Msanii wa Burundi mwenye sauti ya kuvutia ambae amekuwa akifafanya vizuri katika kushiriki (Featuring) kwenye nyimbo za wasanii wengi jijini Bujumbura Riche Florin a.k.a R.Flow, ameingia studio kurikodi wimbo wake mpya utaokuja kwa jina la “Ibuka” ikimaanisha “Kumbuka”.

Akichonga na Ikoh.Biz, R.Flow amesema yupo Studio Ikoh Multiservice kutengeneza wimbo wake huo na amekataa kuzungumzia mengi kuhusu wimbo huo katika kile alichosema anahofia kukata ladha kwa wapenzi wa muziki wake kabla hata ya wimbo huo kusikika.


Ametetea hoja yaki hii kwa kusema kwamba wasanii wengi wamekuwa wakizungumzia wimbo yaliomo katika wimbo huo kabla hata wapenzi wa muzki hawajasikiliza, na hii ndio sababu kumekuwa na minong'ono ya kuibiana mashahiti bila hata hivyo kuwepo na viashiria halisi.


R.Flow amesema Chini ya Producer Botchoum, anaimani kwamba wimbo huo utakonga nyoyo za wapenzi wa muziki nchini Burundi.

Jumatano, 17 Aprili 2013

BI KIDUDE AFARIKI DUNIA

Msanii mkongwe, wa miondoko ya Taarab asilia kutokea visiwani Zanzibar nchini Tanzania, alitamnba katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati, Fatuma Binti Baraka maharufu kama Bi Kidude amefariki dunia leo jumatano huko Zanzibar.

Bi kidude anaye kadiriwa kuwa na umri wa miaka 100 alikuwa maharufu sana hasa kutokana na umri wake mkubwa  lakini pia uwezo wa kumudu jukwaa ipasavyo anapotumbwiza halaiki ya watu.

Kwa mujibu wa mpwa wa Bi Kidude Baraka Abdallah Baraka, shangazi yake alikuwa anasumbuliwa na maradhi aina mbalimbali ikwemo kisukari, mapafu kuungua kutokana na sigara, Kongosho na chango.
Bibi Kidude mmoja kati ya waimbaji maarufu wa muziki wa asili alianza kujishuhgulisha na fani ya muziki mnamo mwaka 1920 akiwakilisha vyema kueneza utamaduni na muziki visiwani Zanzibar na nje ya Zanzibar.
Shughuli za mazishi zimepangwa kufanyika kesho Alhamisi huko huko visiwani Zanzibar 

QUESTION G, WAFANYAKAZI KWA VITENDO NA SIO KWA MANENO.

Mwishoni mwa juma lililopita kundi la Question G, lenye Maskani yake tarafani Bwiza katika manispaa ya jiji la Bujumbura, wame rikodi video zao mbili kwa pamoja na kudaikuwa hawafanyi kazi kwa maneno bali kwa vitendo.

akichonga mawili matatu na Ikoh.biz, Josdi Prince mmoja miongoni mwa vijana wanaunda kundi hilo amesema waliahidi kuwa mwaka huu watafanya kazi kwa vitendo, na ndicho wanachokifanya kwa sasa, baada ya kurikodi Audio ya wimbo wao 'Inauma sana' na kumshirikisha msanii wa Burundi anaekichanga huko Afrika Kusini mshiriki wa tuzo za Kora Awards 2012, Chris Dizzo, na sasa wapo jikoni kuipika video hiyo ambayo hata hivyo itakuwa tayari ziku za usoni.

Aisha ameendelea kuwa wimbo mwingine unaotengenezewa video kwa sasa ni wimbo wa Bella na Shella, wimbo wa kundi hilo.

Question G ni moja miongoni mwa makundi yaliowahi kutikisa jiji la Bujumbura katika miaka iliopita baada ya kujizolea mashabiki wengi kutoka katika tarafa mbalimbali za manispaa ya jiji la Bujumbura.

Vijana wa kundi hili wamekuwa wakipata mialiko ya huku na kule kwa ajili ya kuendesha burudani ambapo hivi karibuni walikuwa Mkoani Gitega kukonga myoyo ya wapenzi wa Muziki katika eneo hilo la nchi.

MIKE BASUZWA AENDELEA KUKOMAA KWENYE TASNIA YA MUZIKI LICHA YA KUJICHANGANYA NA KAZI NYINGINE


Mike Basuzwa ni msanii wa Burundi aliejichimbia makazi nchini Afrika Kusini katika jiji la Cape Town eneo kunako itwa Sea Point na ambae anaendelea ku komaa kwenye game licha ya kujishughulisha na kazi nyingine mbali na Muziki.


Mike Basuzwa ni mmoja kati ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi la G.O.N chini ya uongozi wa msanii mkongwe katika game la muziki wa kizazi kipya, Baby G.

Akizungumza mawili matatu na ikoh.biz, Mike Basuzwa amesema kwas asa anajiandaa kuingia studio kutengeneza wimbo mpya alioshirikishwa na msani imwingine kutoka Lubumbashi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, track itayo kuja kwa jina la Fadher G, kabla ya kuanza harakati za kutengeneza video hiyo chini ya Producer Keshy Video Lab.
Akiulizwa kuhusu mtazamo wake juu ya Muziki wa Burundi na wa vijana wa Afrika Kusini, Mike Basuzwa amesema Muziki wa vijana wa Afrika Kusini upo juu zaidi, kiasi cha kuupimanisha na muziki wa Ulaya, kwani heshima, sheria zinafanya kazi, wasanii wanapata haki yao. Lakini kwa upande wa wasanii wa Burundi wa kizazi kipya ambao wanafanya muziki nchini Afrika Kusini, msanii huyo amesema kwa upande huo afadhali Burundi kwakuwa kuna mashabiki wengi wanaoupenda muziki wa kizazi kipya.

Akiendelea kulizungumzia hilo Mike Basuzwa amesema sio rahai msanii kuvuma ukiwa ungenini, inabidi kujituma na kufanya kazi kwa bidii, ili kufikia kiwango cha juu.

Mike Basuzwa ameendelea kusema kuwa licha ya kwamba hajabahatikiwa kupata mafaanikio yoyote kupitia muziki, bado hajachoka kwakuwa safari bado ni ndefu anaendelea kutia matumaini kwamba ipo siku ataeshi kwa kutegemea Muziki kwakuwa hatuwa alioifikia ni ya kuridhisha


Akiulizwa kuhusu kitu ambacho hatokisahau tangu alipoingia katika game la muziki, Mike Basuzwa amesema hatosahau kamwe vurugu walizozifanya wakati akiwa na ma chiz wake wa kundi la G.O.N alikoanzia musiki pamoja na Baby G ambaye bado yupo Buja, Kiminikis ambae kwa sasa yupo Tanzania, na Taz Mas ambapo wote kwa sasa kila mmoja yupo nchi tofauti na mwingine.

Mike Basuzwa anazungumzia wimbo wake wa kwanza katika kundi hilo la G.O.N uliobeba jina la ni ‘Soo ‘ambapo anasema kwake ni ukumbusho mkubwa sana ambao hatosahau maishani mwake.





Jumatatu, 15 Aprili 2013

PRODUCER WA VIDEO WA KAMPUNI YA IKOH MULTISERVICE AZURU JIJI LA DAR ES SALAAM

Producer mahiri wa video wa kampuni ya Ikoh Multiservice Gueraman anazuru jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi iliomkutanisha na ma Producer wa Tanzania na kuzungumzia kuhusu maendelea ya muziki wa Burundi.
Akiongea na Ikoh.biz, Gueraman amesema amepata fursa ya kutembelea studio mbalimbali na kukutana na ma Producer wa video wa nchini Tanzania, na kubadilishana maujanja kuhusu kutengeneza video zenye viwango.
Gueraman amesema amenufaika sana na ziara hiyoya wiki moja katika jiji la Dar Es Salaam ambapo amehidi kufanya vizuri zaidi katika kazi yake baada ya kugundua mambo mengi ambayo amesema wenzetu wanayo tumia katika kutengeneza video.
Mbali na hayo Gueraman amezungumzia pia changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo katika kutekeleza kazi yao, na kuongeza kwamba la muhimu ni ma meneja au wale wanaowasimamia wasanii kugharamia vya kutosha video za wasanii badala ya kubania baadhi ya mambo ambayo amesema ni ya muhimu katika kurikodi picha za video.
Akizungumzia baadhi ya changamoto, Gueraman amesema huwa inatokea mara nyingi sehemu ya kurikodia picha inakosekana dakika za mwisho, na wahusika kuamua kuchukuwa picha katika maeneo ambayo hayana mandhari mazuri, kwa kuhofia gharama.
Amewatolea wito wasanii na wasimamizi wao kugharamia video zao ili ziwe na viwango vya kutosha na kuweza kushindanishwa kimataifa.

Jumatano, 10 Aprili 2013

YOYA ANAKUJA KITAMADUNI ZAIDI

 Msanii mwenye mvuto na mwenye hadhi ya kipekee nchini Burundi ambae anafanya vizuri kwa sasa nchini humu Yoya Jamal almaharufu "Yoya" ameingia Studio Ikoh Multiservice kurikodi wimbo wake mpya chini ya producer Botchoum utaokuja kwa jina la "Haguruka" ikimaanisha"Simama" kwa lugha iliotukuka ya Kiswahili.

Yoya akiwa studioni huku Botchoum akifanya mambo
akizungumza na Ikoh.biz, Yoya amesema kwamba ni mara ya kwanza anatumia style ya kitamaduni na anataraji kuwa, wimbo huo utafanya vizuri baada ya kushirikiana na producer mahiri ambae amekuwa na ubunifu wa hali ya juu.

Producer Botchoum akichanganya sauti
Wimbo huo "Haguruka" unawatolea wito vijana wa Burundi kuwa wabunifu zaidi katika kupanga mbinu za kujiendeleza wenyewe pasina kutegemea kazi zinazo tolewa na serikali, na kwamba hakuna kisicho wezekana ikiwa kuna nia na bidii za kutosha.

Yoya amedokeza kwamba wimbo huu "Haguruka" utakuwa katika orodha ya nyimbo ambazo zita beba album yake ya kwanza ambayo amethibitisha kwamba itakuwa hewani kabla ya mwaka huu kumalizika.

Yoya Jamal akiwa katika pozi
Nyimbo kadhaa za msanii huyu mwenye mvuto wa kipekee ambazo zimekubalika na kutikisa jiji la Bujumbura ni pamoja na "Igiturire" wimbo ambao ulimsababishia kupata tuzo la shirika linalopiga vita rushwa nchini Burundi OLUCOME.

mwaka uliopita Yoya alitoka na kibao chake "Warahemutse" kibao ambacho kili konga nyoyo za wapenzi wengi wa muziki baada ya kuguswa na historia ilio beba kibao hicho.



Jumatatu, 8 Aprili 2013

SHUKRANI ZA TIMBULO KWA MASHABIKI WAKE

Msanii wa Bongo Fleva anaekuja kwa kasi Ali Timbulo almaharufu Timbulo, ama ukitaka muite mzee  waleo wa kesho, amezindua wimbo wake wa Sina Makosa kwenye ukumbi wa Club Billcanas usiku wa jana Jumapili jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania.


Show hiyo ya uzinduzi wa Track mpya ya Timbulo Sina Makosa imeonakana kufana kwa kiasi kikubwa baada ya mashabiki wengi kujitokeza ili kutowa sapoti kwa msanii huyo ambae mbali na muziki kwa sasa amejikita pia katika filamu ambapo filamu yake ya kwanza kuigiza Life of Benefit itaachiwa wakati wowote.

Akizungumza na Ikoh.biz, Timbulo amesema anatowa shukrani za dhati kwa mashabiki wake na watu wote waliojitokeza pale Billcanas kwa ajili ya kutowa sapoti, kabla ya kuongeza kuwa amejipanga vizuri kuhakikisha anawaridhisha mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva.

Alhamisi, 4 Aprili 2013

WASANII NA WATUNZI NCHINI BURUNDI WAHIMIZWA KUORODHESHA KAZI ZAO.


Kwa muda mrefu kumekuwa na kilio kisichokoma kwa wasanii wsa Burundi kuomba serikali iwalindie kazi zao, kwani wamekuwa wakifanya kazi lakini wanaonufaika na matunda ya kazi zao ni watu wengine ambao hu kopi kazi zao na kujipatia pesa bila hata hivyo kugharimu chochote.
Donatien Niyungeko Mkurugenzi wa Ofisi inayo linda haki za wasanii n watunzi


hili lina dhihirika katika kila kona ya nchi nyimbo za wasanii zinachezwa sana, lakini ukiwauliza wanaozicheza wapi wamezipata, inakuwa ngumu kueleza kwani wengi huzipata kwa njia isiokuwa halali ingawaje baadhi hupokea kutoka kwa wasanii wenyewe
Serikali kupitia wizara ya michezo vijana na utamaduni iliunda ofisi ya ulinzi wa kazi za wasanii na watunzi tangu mwezi  Juni mwaka 2012 ingawaje shughuli za uundwaji wa taasi hiyo zilianza tangu mwaka 2011 wakati wa uongozi wa wizara hiyo wa Jean Jacques Nyenimigabo ambapo kabla ya kuondoka kwenye wizara hiyo aliwatolea wito viongozi tawala kuhamasisha ili watunzi na wasanii waorodheshe kazi zao kwenye taasisi hiyo iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu na gamu na wasanii pamoja na watunzi mbalimbali nchini.
Akizungumza na Ikoh biz, mkurugenzi wa taasisi hiyo, Donatien Niyungeko amesema, wanaendelea na harakati za kuhamasisha wasanii ikiwa ni hatuwa moja kubwa katika kufikia malengo muhimu ya ulinzi wa kazi zao, kwsani ameendelea kusema itakuwa vigumu serikali ilinde kazi hewa, hivyo kuna umuhimu kujuwa kana kwamba kweli kazi hii ni ya msanii huyo na labda imefayiwa kopi na huyo na sheria hapa zinafuata mkondo wake.
Mkurugenzio huyo ameimbia Ikoh Biz kwamba wasanii wengi wamekuwa wakija kuomba wapewe muelezoi kuhusu taasisi ambayo ipo kwa ajili yao.
Katika kutamatisha Donatien Niyungeko amesema ataeashangaa wasanii ambao watanedelea kuomba kiupitia vyombo mbalimbali ya habari nchini Burundii wapewe haki zao wakati hawajihamasishi kujulisha kazi zao.
Kwa hatuwa hii mabadiliko yanahitajika katika kila nyanja kuhakikisha msanii anakula kutokana na jasho lake, lakini pia mabadiliko yanahitajika katika kazi za wasanii kuwa makini katika kutengeneza kazi zenye kukidhi viwango.

Jumanne, 2 Aprili 2013

BRARUDI YAKUSANYA MILLIONI 30 KATIKA TAMASHA LA HARAMBEE KWA WAATHIRIKA WA SOKO KUU

Kiwanda kinachotengeneza vinjwaji nchini Burundi cha Brarudi kimekusanya takriban Franka za Burundi Millioni thalathini katika tamasha LA pasaka liloandaliwa kwa ajili ya kukusanya fedha zitazo changia kwa waathirika wa soko kuu la jijini Bujumbura.

Wapenzi wa Muziki na Burudani walijitokeza kwenye uwanja wa mpira wa shule la Lycee Nyakabiga, Zamani EFI/Nyakabiga hapo zamani wakati wa siku kuu ya Pasaka Machi 31 kushuhudia burudani iliotolewa na wasanii wa Burundi ambao walikuwa wamejiandaa vya kutosha kuhakikisha wanatowa Burudani inayo ridhisha.











































Wakati Burudani ikiendelea Mkurugenzi mkuu wa Brarudi Maarten Schuurman alijitokeza na kutowa shukrwani za dhati kwa waliohudhuria tamasha hilo na wasanii waliokubali kushiriki bila pengamizi lakini pia waandishi wa habari ambao waliendesha matangazo kuhakikisha watu wengi wanahamasishwa. Mkurugenzi huyo ametumia fursa hiyo kutangaza kiwango cha pesa kilichokusanywa ambacho kilifikia Franka za Burundi millioni thalatini.

Upande wake Mkurugenzi mkuu wa shirika la wafanyabiashara na viwanda CFCIB Christian Nkengurutse baada ya kukabidhiwa hundi hiyo ya Faranga za Burundi millioni thalathini(30 Millions de FBU) amepongeza kiwanda hicho huku akiwahakikishia waliokuwepo kwamba hundi hiyo itawafikia wahusika bila shaka kupitia shirika “Burundi Bwacu” linalo saidia waliokumbwa na jinamizi la kuunguliwa na bidhaa zao katika soko kuu jijini Bujumbura mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu wa 2013.

Wadadisi wa maswala ya Muziki wanasema kwamba Brarudi imetowa changamoto kubwa kwa wanaoandaa maonyesho ya muziki jijini Bujumbura baada ya kurekebisha kasoro ambazo zilikuwa zikishuhuduwa hususan kuhusu vyombo, sauti, jukwaa(Podium) msongamano mlangoni na mengi mengi.

Jumatatu, 1 Aprili 2013

JUMA KASIM KIROBOTO "SIR NATURE ATANGAZWA KUWA MFALME WA TEMEKE KATIKA PAMBANO LA NANI MFALME WA TEMEKE


 katika mpambano wa kukata nashoka uliofanyika siku ya Jumapili wakati wa siku kuu ya Pasaka jijini Dar Es Salaam Tanzania katika uwanja wa Burudani Mbagala Zakhiem, uliokuwa ukiyakutanisha makundi mawili ya Manispaa ya Temeke, TMK wanaume Family na Mr Temba na Chege na lile la  TMK wanaume Halisi la Kinara Sir Nature na Inspector Harun,  kundi la wanaume Halisi ndilo lilitoangazwa kuwa mshindi wa pambano hilo.

Majaji wa pambano hilo wamemtangaza Sir Nuture kuwa ndie mfalme wa TMK baada ya kuwabwaga mahasimu wao TMK wanaume Family.

Katika pambano hilo mashabiki walimkubali Sir Nature kutokana na umiliki wake wa jukwaa na jinsi alvyo cheza na mashabiki kuwazidi wanaume Halisi na hatimae kutangazwa mshindi.


Mashabiki na wapenzi wa Burudani kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam walieshuhudia mpambano huo ulioondowa ubishi kati ya makundi hayo hasimu. Makundi hayo mawili yalikuwa yamejiandaa vya kutosha kuhakikisha ushindi unapatikana.
Prof Jay ndie aliekuwa mpambe wa mashindano hayo pamoja na Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa.

Mashaki wengi waliondoka hapo wakithibitisha kwamba Sir Nature ndie mfalme wa Temeke.

MUZIKI UNALIPA KAMA UKIWA NA BIDII."JAY FERNANDO"



Katika dhamira yetu ya kutaka kukueletea habari za wasanii mbalimbali wa Burundi ambao wapo nje ya nchi, Ikoh biz tumetembelea nchini Ubelgiji ambako wapo wasanii wengi tu wa Burundi waliopiga kambo nchini hapo, lakini kwanza kabisa tumekutana na  msanii mzaliwa wa Burundi ambae kwa sasa anaeshi nchini hapo Ubelgiji Jay Fernando ama Junior The Legendary. Kwanza kabisa tulianza kumuuliza amezaliwa wapi na hapa tulipokutana ni wapi?



Jay Fernando: 
Mi ni mzaliwa wa Bujumbura nchini Burundi, lakini kwa sasa naeshi nchini Ubelgiji ndipo nilipo kwa sasa na hapa tulipo ni Brusels

 Ikoh biz: lini umeanza suhguhuli za muziki na tayari una nyimbo ngapi au album ngapi hadi leo?


Jay Fernando: Nnimeanza muziki mwaka 2003, na nina nyimbo tano, mbili nimeshirikishwa na washkaji zangu kutoka kundi la East Coast Buja, 3 ni za kwangu 2 ndizo nimeshaachiya moja sikuachia kwa sababu sikupenda zilivyo tengenezwa, zitafanyika marekebisho kwanza kabla ya kuziachia baadae.



ikoh biz: Nini kilichokuvutua katika muziki?



Jay Fernando: kwanza nilipenda muziki, pili nilikuja kuvutiwa na muziki pindi nilipoanza utunzi wa mziki mwaka 2003 na tena nimependelea kufanya mziki ili kuweza kuendeleza kundi la Nigger Soul Family alilokuwa akiongoza marehem kaka yangu Patrick W.Dog.




Ikoh biz: yapi mafaanikio yako katika tasnia hii ya muziki?



Jay Fernando: mafanikio niliyopata sio makubwa sana, ila namshukuru Mungu nimepata kufaHamika kidogo pande za Ulaya na nyumbani piya.



Ikoh biz: Vipi wauonaje Muziki wa kizazi kipya barani Ulaya na Afrika?



Jay Fernando: Muziki wa Afrika naweza kusema kuwa ni afadhali kidogo kuliko Ulaya, ingawaje sio rahisi kufaanikiwa, ila barani Afrika unapata opportinuty nyingi kuliko uylaya, hapa Ulaya mpaka mtu kufika kuwa msanii mkubwa inaomba support kubwa sana na labda upate Sponsa kubwa waweze kuku sign kwenye label kubwa, pili inabidi uimbe kwenye lugha ambayo watu wanaelewa, kwa ufupi naweza kusema nyumbani afadhali kuliko hapa Ulaya.




ikoh biz: Ni nyimbo gani kati ya nyimbo zako unafkiri kwamba zilikonga nyoyo za mashabiki sana?



Jay Fernando: Wimbo wangu wa pili I'm sorry nilio fanya na Romilio na Lena ndio ulikonga nyoyo za mashabiki pia hata mziki wangu mpya Let me be the one watu wameupokea vizuri.



Ikoh biz: Vipi kuhusu mipanfo yako ya baadae?



Jay fernando: 
mipango ninayo ni mingi kwanza najipanga ki maisha mungu akinipa uwezo na uhai in shaa Allah nina plan ya ku realise album yangu itakayo kwenda kwa jina la From The Ghetto To The Castle.











Ikoh biz: Vipi kuhusu lugha unazo tumia katika nyimbo zako huoni kwamba labda nyumbani watu wakashindwa kupokea nyimbo zako vizuri kutokana na lugha unayotumia?










Jay Fernando: 
Wimbo wangu I'm sorry nilitumia Kiswahili, Kingereza na Netherlands, hii track mpya “Let me be the one” nimetumia Kingereza.
 Ndio itakua ngumu nyumbani watu kuelewa ila najitahidi ku lenga jamii zinazo nizunguuka, na kuna baadhi ya watu ambao wamenishauri kuendelea kuimba kwa kiswahili kwa sababu ndio lugha ninayo floor vizuri.
 kwa hiyo nitajitahidi kuendelea kuimba kwa kiswahili huku nikichanga na kingereza.









Jay Fernando akiwa Studioni

Ikoh biz :Ukiangalia kiwango cha muziki wa Burundi labda unaweza kuwaambia au kuwaomba nini viongozi wa Burundi katika kuusaidia muziki wa kizazi kipya uweze kulipa?










Jay Fernando
: Ningeweza kuiomba, serekali iweze kuweka mkazo katika kulinda haki za wasanii ili wasani wa Burundi waweze kula kwa jasho zao, tizama Tanazania, Rwanda Uganda Kenya na na kwengineko muziki umepiga hatuwa lakini inasikitisha kuona wasanii wa nyumbani bado ni masikini inauma sana kwa kweli, serekili ijitolee sana kuwasaidia wasani wa nyumbani ili waweze kupata matunda mema baadae.








Ikoh biz: Wiki kadhaa zilizopita tulikutana na mkurugenzi mkuu wa ofisi ya haki miliki jijini Bujumbura ambapo alitueleza kwamba wasanii hawaorodheshi kazi zao hii unaizungumziaje? hapa serikali italinda nini?









Jay Fernando akiwa na Isaac Bahame

Jay Fernando: Kwakweli naweza sijui nisemeje burundi naona wasani hawapendi mziki wao ufike mbali, sijui wana ma lengo gani na mziki wao, fursa kama hiyo imetokea ndo muda wa kuvuna matunda, kama hawaorodheshi kazi zao vipi serekali itawasaidia? Vipi wataweza kupata kipato kidogo ili kufuta jasho? Kwa hiyo inabi wafunguwe macho na wafanye kazi kwa bidii.





Ikoh biz: kama ikibidi kutowa shukran unafkiri ni akina nani ambao unaweza kuwashukuru kukuwezesha kufikia hatuwa hii?

Jay fernando: Kuna watu wengi tu ambao ninaweza kuwamiminia shukran zangu, lakini shukran za dhati kwanza Mungu aanaendelea kunilinda hadi leo, kwa wazazi wangu ambao walifanya kila liwezekanalo kuhakikisha ninaelimika, lakini pia marafiki zangu ambao wamekuwa wakinisaidia kufanikisha muziki wangu ambapo ni Mohamed Rashidi na Fabrice Nyawakira,
sinto msahau Bahame Isac alienisaidi ku shoot Documentary yangu ya “let me be the one” pia na kwa wengine wote ambao walinisaidia kwa mbali au kwa karibu katika kufikia hatuwa hii.


Jikoh biz: Labda kwa kumalizia unawaambia nini mashabiki?















Jay Fernando akila pozi Studioni

Jay Fernando
: Mashabiki wangu nawaambia wakae mkao wa kula mengi zaidi yanakuja in future, kwa sasa ntachukua likizo ndefu sizani kama ntatowa muziki sasa hivi, ila nitafanya ushirikiano na wasanii wengine tayari nimeshapata mialiko huku na kule, najipanga ki maisha ili kesho niweze ku kamilisha ndoto zangu na ku kamilisha album yangu, na wa ahidi kufanya kazi nzuri na sidhani kwamba ntawaangusha, tuzidi kuomba uhai na uwezo kwa mwenyezi Mungu, subira yavuta kheri, in shaa Allah ipo siku mambo yatakuwa safi na nawa ahidi ku konga nyoyo zao kwa sana maana mambo mengi yako jikoni, kaeni mkao wakula







, lakini pia nawakumbusha kuwa documentary yangu ipo hewani kwa hiyo wanaweza kuitazama wakati wowote.


Ikoh biz: shukran
sana kwa kuwa nasi








Jay Fernando: 
Ni mimi wa ku kushukuru na kukutakia kila la kheri,