Jumatatu, 2 Septemba 2013

RAIS OBAMA AANZISHA HARAKATI ZA KUWASHAWISHI WAJUMBE WA BARAZA LA CONGRESS JUU YA KUISHAMBULIA SYRIA

 Rais wa Marekani ameanzisha harakati za kuwashawishi wajumbe wa baraza la Congress juu ya mpango wa kuishambulia Syria Kijeshi. Juma moja kabla ya kufanyika kwa kikao cha baraza la Congress, rais Barack Obama, makam wake Joe Biden na kiongozi wa ikulu ya Marekani ya White House, wamezidisha kasi kwa kuwasiliana kwa njia ya simu na wajumbe wa baraza la Congress (baraza la wawakilishi  pamoja na wajumbe wa baraza la Senet) kuwashawishi kukubali mpango huo wa kuishambulia Syria Kijeshi.

Rais Obama anakutana leo Jumatatu na kwenye ofisi za Ikulu ya White House na John McCain  kiongozi mwenye ushawishi mkubwa upande wa chama cha Republican ambaye alisema hayupo tayari kutowa idhini kwa Marekani kuishamblia Syria.

Mawasiliano kwa njia ya simu yanatarajiwa kufanyika Jumatatu hii kwa wajumbe wa baraza la Congress kuwashawishi kuidhinisha mpango huo wa mashambulizi.

Maswali ya kujiuliza ni je juhudi hizi zitafaulu? na ikiwa zitafaulu nini kitatokea? Syria itakuwa kama Iraq au Libya? 

What and see