Jumatano, 4 Septemba 2013

KUNDI LA BLACK'S POWER KUTOKA BUKAVU LIPO JIKONI KUPIKA ALBUM YAO YA KWANZA


Vijana wa kundi la Black's Power lenye maskani yake mjini Bukavu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika Mkoa wa Kivu ya Kusini, wameingia studioni kwa ajili ya kurikodi album yao ya kwanza, baada ya kuwa na Track nyingi ambazo wamezitowa kwa nyakati tofauti.

Blacks power wakiwa kazini

Kundi hilo lemye kuundwa na watu kumi ambalo limekuwa likihamasisha vijana dhidi ya ukimwi katika eneo hilo, limekuwa likiandaa tamasha hadharani mara moja kwa miezi miwili chini ya ufadhili wa shirika la AFRICANS ARTISTS FOR DEVELOPMENT (AAD) lenye makao yake makuu nchini Ufaransa.

kwa mujibu wa kiongozi wa kundi hilo Kanyurhi Mpfree, Album  hiyo ya kwanza ya kundi hilo itabebe nyimbo zenye ujumbe wa kuhamasisha vijana na watu wazima kujilinda dhidi ya ukimwi ambao umekuwa tushio kubwa sana duniani.

Mbali na shirika la ADD linalotowa mchango katika shughuli hizo za uhamasishaji wa vijana kujilinda dhidi ya Ukimwi, shirika la SOS Sida  nalo linachangia kuhakikisha Album hiyo inakamilika.

wasanii wa kundi hilo wamekuwa wakitowa burudani katika tasnia ya filamu zenye mafunzo dhidi ya ukimwi.