Mshambuliaji wa klabu ya Manchester
United ambae alitajwa kuwa ataondoka msimu wa baridi uliopita Wayne
Rooney mwenye umri wa miaka 27 ambaye tayari amecheza mechi moja na
kufunga mabao 2 katika mechi ya daraja la kwanza na ambaye aliamuwa
kusalia katika klabu yake ya Manchester United.
Hili ni moja miongoni mwa mambo yanayo
mpa furaha kubwa kocha wa klabu hiyo David Moyes na mashabiki wa
Klabu hiyo.
Ronney alifaulu kupachika nyavuni mabao
2 katika mechi ya klabu bingwa barani Ulaya iliopigwa jana wakati wa
mpambano wao na Bayern Leverkusen na kuandika historia ya kutimiza
mabao 200 akiwa na klabu hiyo ya mashetani wekundu.
Wachezaji watatu pekee ndio ambao
wanarikodi hiyo katika klabu hiyo ikiwa ni pamoja na Jack Rowley
alitimiza mabao 211 Denis Law mabao 237 pamoja na Bobby Charlton
aliefikisha mabao 249.
Wakati huo huo mshambuliaji mwingine wa
klabu hiyo Robert Van Persie amesema anafurahia sana kucheza pamoja
na Rooney kwa kuwa anajuwa kusaka mpira na unauwezo wa kucheza mipira
mifupi na mirefu.
Matamshi ambayo yamempa matumaini
makubwa kocha wa Manchester Unites David Moyes.