Jumatatu, 2 Septemba 2013

KITUO CHA USALAMA WA TAIFA NCHINI MAREKANI (NASA) KINAENDESHA UJASUSI KATIKA OFISI MBALIMBALI DUNIANI.


Kituo cha usalama wa taifa nchini Marekani NASA kimekuwa kikifanya ujasusi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, pamoja na shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki AIEA lakini pia wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa. Gazeti la kila wiki la nchini Ujerumani la Der Spiegel linalo taja faili lililowekwa kwa siri kubwa mwezi Juni ambalo lilitolewa na Edward Snowden afisaa wa Marekani ambaye anaswaka na serikali baada ya kuvujisha siri hizo.
Kuna taarifa zinazo sema kwamba idara ya ujasusi ya Marekani ilifaulu kuvunja mtandao wa kibinafsi unaounganisha Wizara ya Mambo ya Nje na balozi pamoja na ofisi za balozi ndogo (Consulat). Hati nyingine inaonyesha kwamba katika Septemba 2010, NSA ilivutiwa na mawasiliano kutoka ubalozi mjini Washington (jina la siri la Operesheni: "Wabash") na uwakilishi katika Umoja wa Mataifa mjini New York (jina la operesheni: "Blackfoot"), kwa kuweka microphone za kijasusi. Mbali na diplomasia gazeti hilo limesema kwamba NASA inavutiwa pia bila mshtuko na siri za viwanda vinavyotengeneza silaha nchini Ufaransa.

Shughuli za NSA ziliweka doa mahusiano yaliopo kati ya Marekani na Ufaransa mapema Julai, hali iliomfanya rais wa Ufaransa Francois Hollande kuomba kusitishwa mara moja kwa shughuli hizo na kusema kwamba serikali ya Paris haiwezi "kukubaliana na tabia hii kati ya washirika wake.

Kituo cha kunasa mawasiliano ya Marekani kilichopo nchini Ujerumani
Hollande alitaka waziri wake wa mambo ya nje kuwasiliana na mweiziwe wa Marekani John Kerry ili kupata muelezo kuhusu tabia hiyo ya Marekani kufanya ujasusi dhidi ya siri za mataifa mengine.

Kituo cha Aljazeera kilifanyiwa pia ujasusi na Marekani katika kupata taarifa za ndani ambazo ni siri ya ndani ya kituo hicho cha TV kilichopo nchini Qatar ambapo kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Snowden kituo hicho cha NASA kilifaulu kusoma taarifa iliokuwa imefichwa kutoka kwa watu mbalimbali katika lugha ya kiarabu.

SOFTWARE 85,000 ZIKO KATIKA MASHINE KOTE DUNIANI.

Kulingana na nyaraka zinazotolewa na Edward Snowden, Gazeti la Washington Post la nchini Marekani linasema kwamba Marekani ilizindua cyberattacks 231 mwaka 2011, kulenga nchi za Iran, Russia, China na Korea ya Kaskazini. Taarifa hiyo inatowa ushahidi zaidi na zaidi kuhusu utawala wa Obama kujipenyeza mitandao ya kompyuta na kuingilia kati maswala ya kazi za mataifa mengine na kuvuruga utendaji wake kazi. Limeandika gazeti hilo la Washington post likishikilia Badgeti ya shirika la ujasusi la Marekani kupitia taarifa iliotolewa na mkandarasi wa zamani wa Shirika la Usalama wa Taifa (NSA).