Thomas Ntimpirangeza, |
Thomas
Ntimpirangeza, rais wa Mahakama ya rufaa mjini Gitega na Prime
Habiyambere, jaji katika mahakama hiyo, wametiwa nguvuni hivi majuzi
kufuatia waranti ya kukamatwa kwao kutoka kwa hakimu mkuu wa
jamuhuri.
Wawili
hao walikamatwa kwa nyakati tofauti, ambapo mmoja alikamatwa ofisini
kwake huko Gitega, huku mwingine akikamatwa akiwa ziarani jijini Bujumbura. Wote
wawili kwa sasa wamewekwa korokoroni katika jela kuu la Mpimba.
Taarifa
za awali zilieleza kwamba wawili hao walikamatwa baada ya kumuacha
huru mshukiwa wa wizi wa dheruji ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa
miguu, ambapo ilikuwa ni msaada kutoka Ikulu ya Rais.
Huku habari nyingine zikieleza kwamba rais Mahakama ya rufaa alikamatwa baada ya kurusha kwenye mitandasno ya kijamii kampeni ya kura ya hapana katika uchaguzi wa kura ya maoni ujao nchini Burundi.
Hata
hivyo hakimu mkuu wa Jamuhuri Sylvestre Nyandwi anasema wawili hao
wamekamatwa kwa makosa ya Rushwa huku akikanusha taarifa kwamba wawili gao wamekamatwa kutokana na kuendesha kampeni ya hapana.