Jumanne, 4 Juni 2013

SHERIA TATA KUHUSU VYOMBO VYA HABARI YAIDHINISHWA NA RAIS WA BURUNDI

Licha ya waandishi wa habari nchini Burundi kupiga kelele kumtaka rais wa  nchi hiyo, Pierre Nkurunziza, kutoidhinisha muswa tata uliopasishwa na ma baraza ya bunge na seneti kuhusu uandishi wa habari, hatimaye rais huyo ameidhinisha sheria inayplenga kudhibiti utendaji kazi wa vyombo vya habari.
 Wanaharakati nchini humo wanaonakuwa rais Nkurunziza anaingilia uhuru wa vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa sheria hiyo imeharamishwa kuripoti  kuhusu maswala yanayoweza kuhujumu usalama wa taifa, hususan maswala ya jeshi na uchumi wa taifa hilo. Sheria hiyo pia inawalazimisha waandishi wa habari kuweka bayana vyanzo vyao vya habari pamoja na kuwatoza faini ya zaidi ya dola elfu tano ikiwa watakutikana na makosa.
Wadau mbalimbali wa vyombo vya habari nchini humo wameikosoa sheria hiyo na kusema kuna utata mkubwa uliogubikwa sheria na kuonekana kuwa tishio kubwa kwa uhuru wa vyombo vya habari katika nchi inayoitwa kuwa ya kidemokrasia.