Watu
mbali mbali wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege Julius
Nyerere na katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kwa
ajili ya kuupokea Mwili wa Marehemu Albert Mangwea uliowasili mchana
wa leo Jumanne kutokea nchini Afrika ya Kusini.
-Baada
ya mwili kuwasili uwanja wa ndege, utapelekwa katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili ambapo utapokelewa na kuhifadhiwa.
-Baada
ya kuhifadhi mwili, waombolezaji wataelekea Viwanja vya Leaders kwa
maombolezo.
-Kesho
saa 2 asubuhi mwili utakuwa Viwanja vya Leaders kwa ajili ya kuagwa
mpaka saa 6 mchana.
-Saa
6 mchana mwili utasafirishwa kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya
ratiba nyinginezo.