Ijumaa, 7 Juni 2013

USAIN BOLT ASHINDWA KWA MARA YA KWANZA KWENYE MASHINDANO YA RIADHA YA ROME NA JUSTIN GATLI

Bingwa wa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki kwenye Mbio za mita mia moja Usain Bolt kwa mara ya kwanza ameshindwa kupata ushirini kwenye mashindano ya riadhaa ya Rome. Bolt alijikuta akimaliza kwenye nafasi ya pili kwa mara ya kwanza nyuma Justin Gatlin alyefanikiwa kumaliza mbio za mita mia moja kwa kutumia sekunde 9.94 kitu ambacho kilimuacha akistaajabu.

Gatlin ambaye ni raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 31 alifanikiwa kumshangaza Bolt ambaye ni raia wa Jamaica aliyekuwa akishinda kwenye kila mashindano anayoshiriki kwenye mita mia moja na mia mbili.
Bolt ambaye ni mshindi wa medali tatu za dhahabu kwenye Mashindano ya Olimpiki mwaka 2012 nchini Uingereza alibaki anashaa baada ya kujikuta anamaliza kwenye nafasi ya pili kwenye mashindano ya Rome.
Mshindi huyo wa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki mwenye umri wa miaka 26 amesema hana wasiwasi kama kiwango chake kimeshuka na badala yake anahitaji miezi miwili kabla ya kurejea katika kiwango chake.
Bolt ambaye hajawahi kushindwa na Gatlin alionekana amebaki akishangaa baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ya Rome ya mita mia moja na yeye kuamliza katika nafasi ya pili.
Wafuatiliaji wa mashindano ya riadha yameendelea kusema kushindwa kwa Bolt kwenye mashindano ya Rome haiwezi ikawa ishara kuwa kiwango chote kimeanguka na badala yake wasubiri atakachokifanya kwenye mashindano yajayo.
Wapinzani wa Bolt hapo kabla walikuwa ni Yohan Blake na Tyson Gay ambao kwa muda mrefu wameshindwa kumshinda kwenye mashindano mbalimbali ambayo wameshiriki kwa miaka kadhaa.