Jumapili, 30 Juni 2013

CHRIS DIZZO AANIKA SERA ZAKE MTANDAONI

Katika kile kinachoaminika kuwa ndio mipango iliopo kwa sasa, msanii wa Burundi anekipiga huko nchini Afrika Kusini Chris Dizzo, ametagaza sera zake kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na Twitter, huku akiweka wazi kuhusu mipango ya kuuza album yake. bila kurekebisha lolote Chris Dizzo aliandika hivi:
' Information kwa NDUGU na masapotazi wa mziki wangu, I konw mulokuwa mukisubiria nini itafata kabla yakutoka kORA..Actually ivi ndo itavio kuwa kama mungu akipenda, mwezi 8 ntakuwa tayari kuiachia NEW video ( NIMEDATA ft Chanelle ) And from there, My Album ya nyimbo 8 na video zake 6, itakuwa ndo imekamilika ku take over the land...ILA YOTE AYO KAMA MUNGU AKIPENDA...i AMMEN 

Haya kila la kheri na mafaaniko mema katika harakati hizo.http://www.facebook.com/dizzo.chris

YOYA KUKWEA PIPA KUELEKEA DUBAI

Msanii wa Burundi mwenye sifa zake, Yoya Jamal anaelekea kukwea pipa mwanzoni mwa juma lijalo kuelekea mjini Dubai katika nchi za falme za kiarabu ambapo kutakuwa na mpango wa kurikodi video ya wimbo Wake mpya aliotumia lugha ya kiswahili unaokuja kwa jina la 'Karibu nami' chini ya mkono wa Producer Botchoum Pro, baada ya kukubaliana kuingia mkataba na kampuni ya Ikoh Multiservice. Mengi zaidi nitajukuza Kadri ya mambo yatavyoendelea. Bila mtima nyingo nasema Kila la kheri Yoya.

WANANCHI WA UVIRA WAGHADHABISHWA NA KUTOFANYIKA KWA TAMASHA LA ALIKIBA

Uvira ni Tarafa iliopo katika Mkoa wa Kivu ya Kusini mashariki mwa jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayo pakana na Burundi kupitia kata ya Gatumba taraf aya Mutimbuzi  Mkoa wa Bujumbura vijijini. Ni moja kati ya tarafa ambazo huwapokea wasanii mbalimbali wanaoalikwa kwa ajili ya kuendesha burudani.

Hivi karibuni, msanii wa Bongo Fleva mwenye makeke, aliejizolea sifa tele katika nchi za Afrika mashariki na kati Diamond Platnumz, alikuwa katika eneo hilo na kuendesha burudani ya aina yake kabla ya kumalizia jijini Bujumbura nchini Burundi na tamasha la kihistoria.

Jana ilikuwa ni zamu ya msanii wa Bongo Fleva ambaye naye pia amejizoleakundi kubwa la mashabiki wa muziki kutoka katika nchi mbalimbali na kukonga nyoyo za wapenzi wengi wa muziki katika eneo hilo Ali Kiba, kilicho shangaza msanii huyo hakutokea, wakati ambapo kulikuwa na matangazo ambayo yalitolewa kwamuda mrefu juu ya onyesho la msanii huyo kutoka Bujumbura.

Ali Kiba anasubiriwa Jumapili hii Jijini Bujumbura, ambapo hofu imeanza kupanda kwa mashabiki wa msanii huyo amvbapo hadi tunaingia mitamboni ikiwa ni saa nne majira ya hapa Bujumbura msanii huyo alikuwa bado hajawasili. Tunaendelea kufuatilia habari hii

Ijumaa, 7 Juni 2013

USAIN BOLT ASHINDWA KWA MARA YA KWANZA KWENYE MASHINDANO YA RIADHA YA ROME NA JUSTIN GATLI

Bingwa wa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki kwenye Mbio za mita mia moja Usain Bolt kwa mara ya kwanza ameshindwa kupata ushirini kwenye mashindano ya riadhaa ya Rome. Bolt alijikuta akimaliza kwenye nafasi ya pili kwa mara ya kwanza nyuma Justin Gatlin alyefanikiwa kumaliza mbio za mita mia moja kwa kutumia sekunde 9.94 kitu ambacho kilimuacha akistaajabu.

Gatlin ambaye ni raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 31 alifanikiwa kumshangaza Bolt ambaye ni raia wa Jamaica aliyekuwa akishinda kwenye kila mashindano anayoshiriki kwenye mita mia moja na mia mbili.
Bolt ambaye ni mshindi wa medali tatu za dhahabu kwenye Mashindano ya Olimpiki mwaka 2012 nchini Uingereza alibaki anashaa baada ya kujikuta anamaliza kwenye nafasi ya pili kwenye mashindano ya Rome.
Mshindi huyo wa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki mwenye umri wa miaka 26 amesema hana wasiwasi kama kiwango chake kimeshuka na badala yake anahitaji miezi miwili kabla ya kurejea katika kiwango chake.
Bolt ambaye hajawahi kushindwa na Gatlin alionekana amebaki akishangaa baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ya Rome ya mita mia moja na yeye kuamliza katika nafasi ya pili.
Wafuatiliaji wa mashindano ya riadha yameendelea kusema kushindwa kwa Bolt kwenye mashindano ya Rome haiwezi ikawa ishara kuwa kiwango chote kimeanguka na badala yake wasubiri atakachokifanya kwenye mashindano yajayo.
Wapinzani wa Bolt hapo kabla walikuwa ni Yohan Blake na Tyson Gay ambao kwa muda mrefu wameshindwa kumshinda kwenye mashindano mbalimbali ambayo wameshiriki kwa miaka kadhaa.

UINGEREZA YAOMBA RADHI NA KUKUBALI KUTOA FIDIA KWA WAPIGANAJI MAU MAU WALIOPIGANIA UHURU WA KENYA


 Serikali ya Uingereza imekubali kulipa fidia kwa waathiriwa wa vita vya Mau Mau vilivyofanyika nchini Kenya ambapo taifa hilo lilikuwa linapigana kuhakikisha linapata uhuru kutoka kwa wakoloni. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hague ameliambia Bunge nchini huko kwamba serikali inasikitishwa na kile ambacho kilifanywa wakati wa vita vya Mau Mau na hivyo itatoa fidia yenye thamani ya pauni milioni 19.9.

Hague amekiri tukio lililofanywa na wanajeshi wa Uingereza kwa kuwanyanyasa na kuwatesa wapiganaji na hata wananchi wa kawaida ambao walikuwa wanadaia uhuru wao katika kipindi cha miaka ya 1950. Serikali ya Uingereza imetangaza kuwalipa waathirika 5,228 waliopitia madhira mengi kipindi cha vita vya Mau Mau ambapo wanajeshi wa taifa hilo walivamia hadi kambi za raia wa Kenya kipindi cha vita hivyo.

London kupitia Waziri Hague imeomba radhi kama ambavyo iliahidi na kisha kutangaza fidia hiyo kutokana na kuguswa na vitendo vya mateso vilivyowakumba wananchi wa Kenya walioshiriki vita vya Mau mau. Hatua ya Serikali ya London kuomba radhi na hatimaye kulipa fidia inakuja baada ya waathiriwa hao wa vita vya Mau Mau kufungua kesi wakilalamikia utesajwi waliokumbana nao wakati wa vita hivyo.

Waathiriwa hao wa vita vya Mau Mau kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakipambana kuhakikisha wanapata fidia hiyo baada ya kutokea vita vya kudai uhuru vilivyofanyika katika miaka ya 1950.

Jumatano, 5 Juni 2013

HALAIKI YA WATU WAJITOKEZA KUAGA MWILI WA MAREHEM ALBERT MANGWEHA

Matukio kwa picha  mbalimbali za watu waliotowa heshima zao za mwisho kwa marehemu Albert Mangweha msanii wa bongo Fleva aliefariki dunia juma lililopita nchini Afrika Kusini.
 Wote hawa walisubiri kutowa heshima na kuuaga mwili wa Marehemu Albert Mangweha























Jumanne, 4 Juni 2013

SHERIA TATA KUHUSU VYOMBO VYA HABARI YAIDHINISHWA NA RAIS WA BURUNDI

Licha ya waandishi wa habari nchini Burundi kupiga kelele kumtaka rais wa  nchi hiyo, Pierre Nkurunziza, kutoidhinisha muswa tata uliopasishwa na ma baraza ya bunge na seneti kuhusu uandishi wa habari, hatimaye rais huyo ameidhinisha sheria inayplenga kudhibiti utendaji kazi wa vyombo vya habari.
 Wanaharakati nchini humo wanaonakuwa rais Nkurunziza anaingilia uhuru wa vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa sheria hiyo imeharamishwa kuripoti  kuhusu maswala yanayoweza kuhujumu usalama wa taifa, hususan maswala ya jeshi na uchumi wa taifa hilo. Sheria hiyo pia inawalazimisha waandishi wa habari kuweka bayana vyanzo vyao vya habari pamoja na kuwatoza faini ya zaidi ya dola elfu tano ikiwa watakutikana na makosa.
Wadau mbalimbali wa vyombo vya habari nchini humo wameikosoa sheria hiyo na kusema kuna utata mkubwa uliogubikwa sheria na kuonekana kuwa tishio kubwa kwa uhuru wa vyombo vya habari katika nchi inayoitwa kuwa ya kidemokrasia.
 

MWILI WA MAREHEM NGWEHA KUAGWA SIKU YA JUMATANO VIWANJA VYA LEADERS JIJINI DAR ES SALAAM

Watu mbali mbali wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege Julius Nyerere na katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kuupokea Mwili wa Marehemu Albert Mangwea uliowasili mchana wa leo Jumanne kutokea nchini Afrika ya Kusini.



-Baada ya mwili kuwasili uwanja wa ndege, utapelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo utapokelewa na kuhifadhiwa.
-Baada ya kuhifadhi mwili, waombolezaji wataelekea Viwanja vya Leaders kwa maombolezo.

-Kesho saa 2 asubuhi mwili utakuwa Viwanja vya Leaders kwa ajili ya kuagwa mpaka saa 6 mchana.
-Saa 6 mchana mwili utasafirishwa kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya ratiba nyinginezo.