Jumatano, 20 Julai 2022
TAIFA STARS YA TANZANIA YASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI YALAZIMISHWA SARE NA ZIMBABWE
Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imetoka sare ya bila kufungana na timu ya Taifa ya Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa iliyopo katika kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la mpira wa miguu (FIFA), iliyopigwa jana jumanne kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa Tanzani, Kim Poulsen, alilalamikiwa na mashabiki waliohudhuria mechi hiyo, kwa kushindwa kufanya marekebisho ya wachezaji walioshindwa kumudu mchezo.
Hata hivyo, Kipa Ivo Mapunda ambaye kwa muda mrefu hajaitumikia Taifa Stars alionekana kufanya vizuri langoni kwake na kuinusuru Stars kufungwa.
Kwa upande wake Zimbabwe ilitumia wachezaji wengi chipukizi huku Taifa Stars ikiwatumia wachezaji watano wanaocheza soka la nje ya nchi.
Awali Taifa Stars ilitakiwa kucheza na Harambee Stars ya Kenya, lakini Shirikisho la soka nchini Kenya FKF lilituma taarifa likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.
Jumatatu, 25 Oktoba 2021
JESHI LA SUDAN LAFUTILIA MBALI SERIKALI YA MPITO LAAHIDI KUUNDA BARAZA JIPYA LA UONGOZI
Mkuu wa bazara la uongozi wa kijeshi nchini Sudan, jenerali Abdel Fattah al Burhan, ametangaza kulivunja bazara hilo na bazara la mawaziri baada ya kutangaza hali ya dharura nchini humo, katika hali ya kutokea kwa mapinduzi ya serikali ya mpito mapema leo.
Baada ya kukamatwa kwa waziri mkuu na wanajeshi mapema leo, mitandao ya kijamii ilifungwa, wanajeshi wakionekana kushika doria jijini Khartoum, mkuu wa baraza la uongozi nchini humo Abdel Fatta Al Burhan akitangza hali ya dharura nchini humo na kusitisha safari za kimataifa, kutanza kuwa serikali mpya ya mpito itangazwa kubla ya mwisho wa mwezi Novemba.
Serikali ya mpito inayoundwa kati ya raia na Baraza la kijeshi iliundwa mwaka 2019 baada ya kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa muda mlrefu Omar Al Bashir kufuatia maandamano ya wananchi, na ilipaswa kuongoza mpaka 2023 na kupisha Uchaguzi Mkuu.
x
x
Mkuu wa bazara la uongozi wa kijeshi nchini Sudan, jenerali Abdel Fattah al Burhan, ametangaza kulivunja bazara hilo na bazara la mawaziri baada ya kutangaza hali ya dharura nchini humo, katika hali ya kutokea kwa mapinduzi ya serikali ya mpito mapema leo.
Baada ya kukamatwa kwa waziri mkuu na wanajeshi mapema leo, mitandao ya kijamii ilifungwa, wanajeshi wakionekana kushika doria jijini Khartoum, mkuu wa baraza la uongozi nchini humo Abdel Fatta Al Burhan akitangza hali ya dharura nchini humo na kusitisha safari za kimataifa, kutanza kuwa serikali mpya ya mpito itangazwa kubla ya mwisho wa mwezi Novemba.
Serikali ya mpito inayoundwa kati ya raia na Baraza la kijeshi iliundwa mwaka 2019 baada ya kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa muda mlrefu Omar Al Bashir kufuatia maandamano ya wananchi, na ilipaswa kuongoza mpaka 2023 na kupisha Uchaguzi Mkuu.
x
x
Ijumaa, 23 Februari 2018
HASIRA YA TAWALA MJINI DAPCHI SIKU 4 BAADA YA KUTOWEKA KWA WASICHANA 111Lai Mohammed
Lai Mohammed Waziri wa habari nchini Nigeria |
Siku
nne baada ya kutokea kwa shambulio katika shule moja mjini Dapchi
nchini Nigeria, kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika mji huo uliopo
kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako vikosi vya usalama
vimekabiliana na wananchi wenye hasira ambao hadi sasa hawajuwi wapi
walipo binti zao.
Polisi
imethibitisha kuwa wasichana 111 wa shule la wasichana mjini Dapchi
wametoweka tangu kutokea kwa shambulio la kundi la kijihadi la Boko
Haram
hofu
imeendelea kutanda katika eneo hilo ikihofiwa kutokea kwa Chibok
mpya, jimbo lililopo jirani na mji wa Borno ambako kundi la Boko
Haram liliwateka wasichana 276 April mwaka 2014, tukio lililolaaniwa
ulimwengu mzima.
Waziri
wa ulinzi nchini Nigeria Jenerali Mansour Dan Ali amesema wasichana
wengi walikimbia kutokana na uoga na baadhi wameanza kurejea shuleni.
RAIS WA MAHAKAMA YA RUFAA YA GITEGA NA JAJI, WATIWA KOROKORONI
Thomas Ntimpirangeza, |
Thomas
Ntimpirangeza, rais wa Mahakama ya rufaa mjini Gitega na Prime
Habiyambere, jaji katika mahakama hiyo, wametiwa nguvuni hivi majuzi
kufuatia waranti ya kukamatwa kwao kutoka kwa hakimu mkuu wa
jamuhuri.
Wawili
hao walikamatwa kwa nyakati tofauti, ambapo mmoja alikamatwa ofisini
kwake huko Gitega, huku mwingine akikamatwa akiwa ziarani jijini Bujumbura. Wote
wawili kwa sasa wamewekwa korokoroni katika jela kuu la Mpimba.
Taarifa
za awali zilieleza kwamba wawili hao walikamatwa baada ya kumuacha
huru mshukiwa wa wizi wa dheruji ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa
miguu, ambapo ilikuwa ni msaada kutoka Ikulu ya Rais.
Huku habari nyingine zikieleza kwamba rais Mahakama ya rufaa alikamatwa baada ya kurusha kwenye mitandasno ya kijamii kampeni ya kura ya hapana katika uchaguzi wa kura ya maoni ujao nchini Burundi.
Hata
hivyo hakimu mkuu wa Jamuhuri Sylvestre Nyandwi anasema wawili hao
wamekamatwa kwa makosa ya Rushwa huku akikanusha taarifa kwamba wawili gao wamekamatwa kutokana na kuendesha kampeni ya hapana.
Alhamisi, 17 Oktoba 2013
MRADI WA "DADA AISHA NAJALI " ULIVYO FANA KATIKA SHEREHE ZA EID NA WATOTO MAYATIMA
Katika
kuadhimisha sherehe za Eid el Adha, ambayo huadhimishwa na waislam
kila baada ya Hijja, Mtangazaji Aisha Amuri Ndimubandi wa Kituo cha
Radio ya Umma R.P.A alitekeleza mpango wake wa “Dada
Aisha najali” kwa kuandaa Ghafla maalum kwa ajili ya kuchangia siku
kuu hiyo na watoto mayatima wa kituo cha kulelea watoto kilicho
tarafani Kinama cha AVOVOU.
Akizungumza
na safuu hii, Aisha Ndimubandi amesema, ameamuwa kucnagia Eid na
watoto mayatima huku akiwashirikisha wasanii mbalimbali na wadau
kutoka jijini Bujumbura, ameendelea kuwa, hii ni hatuwa ya kwanza
mpango huo utaendelea huku kukiwa pia na program ya kuwasaidia
kinamama wenye kuw ana matatizo ya saratani.
Ghafla
hiyo iliofanyika kwenye ukumbi mahrufu wa lycee du Lac jijini
Bujumbura imehudhuriwa na wasanii wengi wanaongurumisha muziki wa
kizazi kipya nchini Burundi.
Muhusika
mwenyewe amesema, akianzisha mradi huo alipata msaada kutoka nje na
ndani ya Burundi, ambapo mtoto wa rais wa Tanzania, Ridhiwani
Kikwete, mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe na Hussein Njovu walichangia
kufaanikisha mradi wake wa “Aisha Najali”
Aidha
ameendelea kuwa katika kuakmilisha ghafla hiyo kampuni ya Ikoh
Multiservice imechangia pakubwa pamoja na dreams House na Oxygine
Company, bila kumsahau Josue ambaye ni raia wa Kenya.
Msanii
Yoya Jamal ambaye alikuwa miongoni mwa wanamuziki walioashiriki
katika ghafla hiyo amesema huu ni mfano mzuri wa kuigwa na watu
wengine kwa kuwakumbuka watu wenye kukabiliwa na matatizo hususan
watoto kama hawa.
Upande
wake R.Flow amesema ukiwaangalia watoto hawa kwa siku ya leo huwezi
kujuwa kama ni watoto mayatima, na hii ndio iliotupa msukumo wa kuja
kuchangia nao siku kuu hii ya Eid, ili kuwafanya wajihisi kwamba nao
pia ni sehemu ya familia.
Aisha na Producer Amir Pro |
Bruno
Memba ambaye ni rais wa shirika la wanamuziki nchini Burundi,
amewatolea wito viongozi mbalimbali kuwatolea msaada watoto wa aina
hii na kuwafanya wajihisi kuwa wanayo familia inayo wajali.
Naye
Manaja mkuu wa kampuni ya Ikoh Multiservice Haruna Ikoriciza ametowa
pongezi wa mtangazaji Aisha Amuri kwa kuwafkiria watoto mayatima,
kwakuwa watoto hawa hawakupenda kuwa mayatima. Amewataka wadau
mbalimbali kuwafikiria watu wasiojiweza na kuwakumbuka kwa kuwatolea
msaada na sio tu siku za sherehe bali na siku zingine.
Aisha na Rally Joe |
Kali
hii ya Ikoricica Haruna imetiliwa mkazo na Manager Director wa
kampuni ya Ikoh Multiservice Abdallaha “The Carter” yatima
hakumbukwi tu siku za sherehe, watu wengine wanaweza kuchukuw amfano
kwa hatuwa hii iliofikiw ana dada yetu na kuliendeleza taifa letu
ambapo hakuna anaye juwa miongoni mwa watoto hawa watatokea kina
nani.
Crew
ya Ikohm.blogspot hatunabudi kumpa pongezi dada yetu Aisha kwa mradi
wake huo na kumuombea Mungu amjalie kwa kupiga hatuwa zaidi kwa
kwenda mbele.
Jumanne, 15 Oktoba 2013
EID MUBARAK KWA WAISLAM WOTE ULIMWENGUNI
Ikoh Multiservice na Ikoh.biz, tunawatakia waislam wote ulimwenguni siku kuu njema ya Eid Adha, siku kuu ya Kuchinja. Kila la kheri hapo ulipo mpendwa.
Jumapili, 13 Oktoba 2013
PAPA WEMBA AFANYA FEATURING NA NYOKA LONGO, JB MPIANA NA BARBARA KANAM
Papa Wemba le Grand Nkuru |
katika maandalizi ya Album yake iliobeba jina « Maître de l’école « yaani mkuu wa shule, kiongozi wa Bendi ya Muziki nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRCongo Viva-la-Musica. Papa Wemba, amefanya featuring na wasanii Nyoka Longo de Zaïko Langa Langa Nkolo Mboka, JB Mpiana, kiongozi wa kundi la Wenge Musica Bon Chic, Bon Genre, pamoja na mwanamuziki wa kike Barbara Kanam, ambaye tayari ameweka sauti katika wimbo » Sur mesure «
Kwa sasa wanasubiriwa Nyoka Longo na JB Mpiana.Katika kusubiri tayari viungo vya sauti ya album hiyo » Maître de l’école » vimepelekwa jijini Paris kwa ajili ya maandalizi ya album hiyo yenye track 13. Kama ilivyokawaida Papa Wemba ametowa nafasi kwa Barabara Kanam kuwa huru katika kutowa mchango wake kwenye kibao Sur Mesure. Barabara Kanam amemshawishi Papa Wemba na wanamuziki wengine wa kundi la Viva la Musica kwa kuwajibika vya kutosha.
Ijumaa, 11 Oktoba 2013
Alhamisi, 10 Oktoba 2013
NATHALIE MAKOMA AKANUSHA UVUMI KUHUSU KIFO CHAKE
Mtunzi wa wimbo wa Injili « No Jesus, no life » amepigwa na mshangao pale alipo pata habari zinazo zagaa kwenye mtandao amefariki na kukanisha taarifa hiyo na kusema kwamba yuu salama bukheri wa Afya na anashkuru Mungu bado anamjalie kumpa pumzi.
Kumekuwa na uvumi uliotanda tangu mwanzoni mwa juma hili jijini Kinshasa na Brazaville kwamba Nathalie Makoma amefariki ghafla, uvumi ambao umeleta mshtuko mkubwa katika familia ya wanamuziki nchini DRCongo na Congo Brazaville.
Nathalie Makoma amemuombea msamaha kwa Mungu yeyote yule ambaye amekuwa akizagaza taarifa hizi ambazo hazina ukweli wowote.
Nathalie Makoma kwa sasa anaandaa wimbo wake ambao hivi karibuni utakuwa sokoni.
MTANGAZI BAKARI UBENA AANZISHA KIPINDI "DIAPORA SHOW" BARANI ULAYA
Mtangazi wa zamani wa Radio ya Umma RPA nchini Burundi Bakari Ubena, ambaye kwa sasa anaeshi nchini Ubelgiji, ameanzisha kipindi maalum kupitia runinga, cha "Diaspora Show" ambacho kinatowa nafasi kwa watu mbalimbali kutoka katika ukanda wa Afrika mashariki nakati waishio mbali na Afrika, kujuwa wanafanya nini.
Makala ya kwanza ya kipindi hiki yamemkaribisha msanii wa kizazi kipya nchini Burundi Jay Fernando ambaye anafanya kazi hiyo ya Muziki huko barani Ulaya, chini ya Producer Bahame Newton ambaye pia ni raia wa Burundi anaendesha kazi zake mbalimbali barani Ulaya.
Kwa mujibu wa muhusika mwenyewe, kipindi hicho kitakuwa kikiwapokea watu mbalimbali wakiwemo wasanii, wanamichezo na wanasiasa kuzungumzia mambo mbalimbali. Mbali na watu ambao wanaeshi barani Ulaya Asia, Marekani, wale wanatembelea katika maeneo hayo watapewa fursa ya kushikiri kwenye makala mbalimbali za Diaspora Show.
Makala hizo za Dispora show zitakuwa zikirushwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini Burundi.
Ikoh.biz, hatuna budi kuwatakia kila la kheri, Bakari Ubena na Isac Bahame Newton.
Jumatano, 2 Oktoba 2013
BUS LA TAQWA BUJUMBURA-DAR ES SALAAM LAANGUKA KATIKA MTEGO WA MAJAMBAZI
Bus la Kampuni ya Usafiri la Taqwa lililokuwa na abiria 51 likisafiri kutokea jijini Bujumbura nchini Burundi kuelekea Dar es Salaam Tanzania, usiku wa jana kuamkia leo Jumatano Octoba 2, limetekwa na majambazi katika eneo la Mirade kata ya Iguguno Mkoani Singida.
Majambazi hao waliweka mawe makubwa barabarani na kuyafunika kwa majani. Dereva wa Bus hilo aligonga mawe hayo na hivo tairi za bus hilo kupasuka na kusababisha bus hilo kuanguka kwenye korongo.
Majambazi hao walilazimisha abiria kushuka ndani ya Bus mmoja baada ya mwingine.
Kwa Mujibu wa kamanda wa Polisi katika Mkao wa Singida Joseph Kamelwa, takriban dola za Marekani elfu moja, Shilingi za Tanzania milioni tano na franka za Burundi laki mbili, zimeporwa
Abiria 20 wamejeruhiwa kwa kupigwa, huku vitu mbalimbali vya thamni vikiporwa.
Polisi inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika.
Jumatatu, 30 Septemba 2013
JAY FERNANDO ATOWA SHUKRANI ZA DHATI KWA WALIOJITOKEZA KATIKA SHEREHE YAKE YA BIRTHDAY
Msanii wa Burundi mwenye makaazi yake huko Ulaya, Jay Fernando wakati akiadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake alikusanyika pamoja na wapenzi mbalimbali huko Brusels kwa ajili ya Birthday hiyo.
Mambo ya mduara pia yalikuwepo |
Ametowa shukrani za dhati kwa wale wote waliochangia kwa njia moja ama nyingine katika kufaanikisha sherehe hiyo iliofana baaada ya kuhudhuriwa na watu kutoka katika maeneo tofauti.
Wakati wa kuserebuka |
Jumamosi, 28 Septemba 2013
MR HAPPY AENDELEA KUTANUA JIJINI NAIROBI BAADA YA KURIKODI NYIMBO ZAKE MBILI
Mr Happy akiwa na mwenyeji wake Jaguar Kwa Mujibu wa taarifa kutoka jijini Nairobi msanii wa Burundi Mr Happy ama Happy Famba tayari amekwisha rikodi nyimbo zake mbili katika studio za Ogopa DJ. |
Mr Happy akiwa nyumbani kwa mwenyeji wake Jaguar |
Wakati wakipata lunch |
Gari analo tembelea Jaguar |
Mr Happy akiwa Studio za Ogopa DJ |
Mr Happy akijifua kidogo kabla ya kuingia Studio |
Ijumaa, 20 Septemba 2013
MR HAPPY FAMBA APEWA SHAVU YA KURIKODI SINGLE 2 NA OGOPA DJ NCHINI KENYA JUMA LIJALO
Msanii mwenye makeke katika jiji la Bujumbura ambaye amejijengea sifa tele kupitia style yake ya kuimba na kucheza, Mr Happy Famba, amepewa shavu na kampuni ya Show Bizz East Africa ya kwenda ku rikodi single zake mbili nchini Kenya.
Ogopa DJ ni moja miongoni mwa kampuni zinazo sifika Afrikari Mashariki kwa ustadi na uwezo wake wa hali ya juu wa kurikodi na kutengeneza Video. Wasanii kutoka katika mataifa mbalimbali Afrika Mashariki na kati wamekuwa na ndoto ya kutaka kufanya kazi na Kampuni hiyo
Kulingana na taarifa kutoka kwa msaniii huyo, Juma lijalo atakuwa nchini Kenya, kwa sasa mipango yote imekamilika, unasubiriwa muda tu wa safari, na utapo wadia atakuwa Nairobi nchini Kenya.
Mr Happy ameiambia ikoh.biz kwamba Katika single hizo mbili, moja itakuja kwa jina Happy Birthday ambayo atashirikina na msani nguli wa Kenya Jaguar, huku nyingine atamshkirikisha msanii mwingine wa nchini humo Nameless.
Mr Happy Famba ni mmoja kati ya wasanii wasio kosa katika tamasha za kitaifa na za kimataifa ambazo hufanyika jijini Bujumbura, na hii ni kutokana na umaharufu mkubwa aliojijengea sio tu kwa kuwa msanii lakini kuwa miongoni mwa watu wanaotowa plani na kupanga mipango ya kufaanisha tamasha hizo.
Kwa sasa amekuwa katika harakati za kurikodi video ya wimbo wake Baby Girl ambao alimshirikisha msanii mwenziye, ukiwa ni moja miongoni mwa nyimbo zinazo vutia wapenzi wa mtindo wa Afro-zouk jijini Bujumbura.
Kinachosubiriwa kwa sasa ni je fursa hii ataitumia vipi msanii huyu?
ikoh.biz tunamtakia kila la kheri.
Kinachosubiriwa kwa sasa ni je fursa hii ataitumia vipi msanii huyu?
ikoh.biz tunamtakia kila la kheri.
Alhamisi, 19 Septemba 2013
KUNDI LA WAKALI POWER LAFUFUKA, LAPEWA SHAVU BONDENI KWA MANDELA
Jay Kizo
Kulingana na taarifa kutoka kwa Jay Kizo mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi hilo la wakali Power ambalo liliwahi kuwa kivutio kikubwa sana na kichocheo katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini Burundi, limefufuka na kupata mualiko wa kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya Burudani, lakini pia kupanga mikakati ya ku shoot video ya wimbo wao "Usiskie Corus" uliojipatia sifa tele jijini Bujumbura miaka ya nyuma mithili ya kugeuka wimbo wa taifa.
Akizungmza na Ikoh.Biz kutoka Ufaransa ambako amejichimbia makaazi, Jay Kizzo amesema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha safari hiyo inafana, kwa sasa amesema yeye yupo Ufaransa, Black G na Marechal Fyiroko Diriri wapo Bujumbura, huku D.Rop akiwa nchini Tanzania, watakutana wote nchini Afrika Kusini katika miezi miwili ijayo.
Marechal Fyiroko
Akiulizwa kuhusu ukimya wa muda mrefu, Jay Kizo amesema kwa sasa kila mmoja anatafuta maisha kwa upande wake, lakini haijamaanisha kwamba kundi limekufa, kwa sasa tunajipanga kuelekea nchini Afrika Kusini ambako mbali na kutowa Burudani, tutarikodi pia nyimbo zetu mbili, moja inaitwa Najuwa, ameendelea kuwa kwa sasa D.Rop yupo Tanzania ambapo ametengeneza wimbo na Msanii wa Bongo T.I.D, mimi nipo Ufaransa, wengine wapo Bujumbura, tunakwenda huko Afrika Kusini kwa mualiko wa Warundi waishio huko bondeni kwa ushirikiano mkubwa wa Keshy Video Lab ltd.
Akijhojiwa na Ikoh.biz, mwenyekiti wa kampuni ya Keshy Video lab ltd, Abdoul, amethibitisha taarifa na kuongeza kwamba kwa sasa taratibu za maandalizi zimeanza, na zitapo kamilika ndipo wataweka bayana kila kitu.
Ikoh.biz hatuna budi kuwatakia kila la kheri.
Jay Kizo |
Akizungmza na Ikoh.Biz kutoka Ufaransa ambako amejichimbia makaazi, Jay Kizzo amesema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha safari hiyo inafana, kwa sasa amesema yeye yupo Ufaransa, Black G na Marechal Fyiroko Diriri wapo Bujumbura, huku D.Rop akiwa nchini Tanzania, watakutana wote nchini Afrika Kusini katika miezi miwili ijayo.
Marechal Fyiroko |
Akiulizwa kuhusu ukimya wa muda mrefu, Jay Kizo amesema kwa sasa kila mmoja anatafuta maisha kwa upande wake, lakini haijamaanisha kwamba kundi limekufa, kwa sasa tunajipanga kuelekea nchini Afrika Kusini ambako mbali na kutowa Burudani, tutarikodi pia nyimbo zetu mbili, moja inaitwa Najuwa, ameendelea kuwa kwa sasa D.Rop yupo Tanzania ambapo ametengeneza wimbo na Msanii wa Bongo T.I.D, mimi nipo Ufaransa, wengine wapo Bujumbura, tunakwenda huko Afrika Kusini kwa mualiko wa Warundi waishio huko bondeni kwa ushirikiano mkubwa wa Keshy Video Lab ltd.
Akijhojiwa na Ikoh.biz, mwenyekiti wa kampuni ya Keshy Video lab ltd, Abdoul, amethibitisha taarifa na kuongeza kwamba kwa sasa taratibu za maandalizi zimeanza, na zitapo kamilika ndipo wataweka bayana kila kitu.
Ikoh.biz hatuna budi kuwatakia kila la kheri.
Jumatano, 18 Septemba 2013
SKENDO YA MADAWA YA KULEVYA YAWASABABISHIA USUMBUFU WASANII WA BONGO FLEVA
Kutokana na wasanii wa Bongo kukumbwa na skendo ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, wasanii Shetta na Chege ambao walikuwa wanasafiri kuelekea nje ya nchi yao na kutakiwa na idara ya upekuzi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalim Jilius Kambarage Nyerere, kupekuwa kila kilichokuwa ndani ya begi zao kama inavyoonyesha picha hiyo.
Biashara hii ya madawa ya kulevya imekuwa ikiichafulia jina nchi ya Tanzania baada ya raia wa Tanzania kukamatwa katika nchi mbalimbali duniani wakijihusisha na biashara hii haramu ya madawa ya kulevya.
AMISI TAMBWE MSHAMBULIAJI WA KIMATAIFA KUTOKA BURUNDI APACHIKA MANNE, SIMBA 6 MUGAMBO 0
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi Amisi Tambwe ambaye anakipiga katika Klabu ya Simba SC, maharufu kama wekundi wa Msimbazi ya jijini Dar Es salaam, amepachika mabao yake matatu katika mchezo wa Simba na Mugambo. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza mshambuliaji huyo aliye sajiliwa hivi karibuni kutoka katika klabu ya Vital'o ya Burundi anapachika bao katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom. Simba imeitamdika Mugambo mabao 6-0, huku mshambuliaji Chanogo akisaidia kusindiria msumari na kuipa simba mabao mawili.
Watani wao wajadi Yanga SC ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi hiyo wametoka sare ya bao 1-1 na Prisons.
Neno Burundi, Mrundi linatajwa sana leo jijini Dar Es Salaam katika vyombo vya habari nchini Tanzania.
BAO LA 200 LA WAYNE ROONEY AKIWA NA MASHETANI WEKUNDU
Mshambuliaji wa klabu ya Manchester
United ambae alitajwa kuwa ataondoka msimu wa baridi uliopita Wayne
Rooney mwenye umri wa miaka 27 ambaye tayari amecheza mechi moja na
kufunga mabao 2 katika mechi ya daraja la kwanza na ambaye aliamuwa
kusalia katika klabu yake ya Manchester United.