Katika
kuadhimisha sherehe za Eid el Adha, ambayo huadhimishwa na waislam
kila baada ya Hijja, Mtangazaji Aisha Amuri Ndimubandi wa Kituo cha
Radio ya Umma R.P.A alitekeleza mpango wake wa “Dada
Aisha najali” kwa kuandaa Ghafla maalum kwa ajili ya kuchangia siku
kuu hiyo na watoto mayatima wa kituo cha kulelea watoto kilicho
tarafani Kinama cha AVOVOU.
Akizungumza
na safuu hii, Aisha Ndimubandi amesema, ameamuwa kucnagia Eid na
watoto mayatima huku akiwashirikisha wasanii mbalimbali na wadau
kutoka jijini Bujumbura, ameendelea kuwa, hii ni hatuwa ya kwanza
mpango huo utaendelea huku kukiwa pia na program ya kuwasaidia
kinamama wenye kuw ana matatizo ya saratani.
Ghafla
hiyo iliofanyika kwenye ukumbi mahrufu wa lycee du Lac jijini
Bujumbura imehudhuriwa na wasanii wengi wanaongurumisha muziki wa
kizazi kipya nchini Burundi.
Muhusika
mwenyewe amesema, akianzisha mradi huo alipata msaada kutoka nje na
ndani ya Burundi, ambapo mtoto wa rais wa Tanzania, Ridhiwani
Kikwete, mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe na Hussein Njovu walichangia
kufaanikisha mradi wake wa “Aisha Najali”
Aidha
ameendelea kuwa katika kuakmilisha ghafla hiyo kampuni ya Ikoh
Multiservice imechangia pakubwa pamoja na dreams House na Oxygine
Company, bila kumsahau Josue ambaye ni raia wa Kenya.
Msanii
Yoya Jamal ambaye alikuwa miongoni mwa wanamuziki walioashiriki
katika ghafla hiyo amesema huu ni mfano mzuri wa kuigwa na watu
wengine kwa kuwakumbuka watu wenye kukabiliwa na matatizo hususan
watoto kama hawa.
Upande
wake R.Flow amesema ukiwaangalia watoto hawa kwa siku ya leo huwezi
kujuwa kama ni watoto mayatima, na hii ndio iliotupa msukumo wa kuja
kuchangia nao siku kuu hii ya Eid, ili kuwafanya wajihisi kwamba nao
pia ni sehemu ya familia.
Aisha na Producer Amir Pro |
Bruno
Memba ambaye ni rais wa shirika la wanamuziki nchini Burundi,
amewatolea wito viongozi mbalimbali kuwatolea msaada watoto wa aina
hii na kuwafanya wajihisi kuwa wanayo familia inayo wajali.
Naye
Manaja mkuu wa kampuni ya Ikoh Multiservice Haruna Ikoriciza ametowa
pongezi wa mtangazaji Aisha Amuri kwa kuwafkiria watoto mayatima,
kwakuwa watoto hawa hawakupenda kuwa mayatima. Amewataka wadau
mbalimbali kuwafikiria watu wasiojiweza na kuwakumbuka kwa kuwatolea
msaada na sio tu siku za sherehe bali na siku zingine.
Aisha na Rally Joe |
Kali
hii ya Ikoricica Haruna imetiliwa mkazo na Manager Director wa
kampuni ya Ikoh Multiservice Abdallaha “The Carter” yatima
hakumbukwi tu siku za sherehe, watu wengine wanaweza kuchukuw amfano
kwa hatuwa hii iliofikiw ana dada yetu na kuliendeleza taifa letu
ambapo hakuna anaye juwa miongoni mwa watoto hawa watatokea kina
nani.
Crew
ya Ikohm.blogspot hatunabudi kumpa pongezi dada yetu Aisha kwa mradi
wake huo na kumuombea Mungu amjalie kwa kupiga hatuwa zaidi kwa
kwenda mbele.