Mnamo siku zote hizi za nyuma, Kuna hali ya kutoelewana kati
ya wasanii wa muziki, hasa wale wanaodumbwiza kwa kutumia muziki wa bendi Ama
Karaoke katika kuwaburudisha wapenzi wa
muziki kwenye kumbi mbalimbali za
starehe na Hoteli pamoja na utawala ambapo kuna sheria inayodaiwa kutolewa na
ofisi ya mea wa jiji la Bujumbura ya kukataza shughuli za muziki zaidi ya saa
mbili usiku.
Kulingana na duru hii sheria amri hii imechukuliwa kufuatia kero
za wananchi waliokaribu na kumbi mbalimbali za starehe ambao wanasema
kukerahishwa na muziki wakati wa usiku ambapo ni wa kupumzika.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa sanaa kwenye wizara ya vijana
michezo na utamaduni Denis Nishirimbere, waziri wa vijana michezo na utamaduni
hajapewa taarifa yoyote kuhusu hatuwa hii ya kuwakataza wasanii wa muziki
kuburudisha zaidi ya saa mbili usiku.
Denis Nshimirimana amefahami sha kwamba kwas asa anasubiri
idhni ya waziri ili aweze kuendesha mkutano maalum kwa dhamira ya kulitafutia
ufumbuzi swala hili.
Baadhi ya wasanii wamejikuta wakikumbwa na amri hii ambayo
hata hivyo wanasema imetolewa na ofisi ya mea wa jiji la Bjumbura ili
kuwakandamiza wengi wao ambao wanaeshi kwa kutegemea kipato wanachokipata baada
ya kucheza muziki huo’Karaoke’
Wasanii waliozungumza na Ikoh Biz, wamesema sheria hii haina
nafasi wakati huu Burundi Usalama na amani vinatawala katika maeneo yote ya
nchi.