Jumatano, 27 Machi 2013

HALI YA AFYA YA MSANII MAISHA MUSTAPHA YAIMARIKA

Msanii nguli wa miondoko mchanganyiko ambae pia ni mtengenezaji wa muziki "Producer" Maisha Mustapha, aliewahi kutamba na vibao vyake "Cikangali Kachi", "mama" na vingine, afya yake yaimarika baada ya kuripotiwa kuwa mgogoro siku za nyuma kutokan na kupata maumivu ya mwili alioyachukulia kuwa ya kawaida, lakini baadae, hali ilizidi kuwa mbaya zaidi na kujikuta hawezi kutoka chini.




Akizungumza na Ikoh Biz, Maisha Mustapha amesema hali yake ya afya ilianza kudhohofika pale alipoanza kusikia udhaifu wa mwili  na kulichukulia kuwa hali ya kawaida lakini baadae alishituka pale alipo amka na kujiskia hawezi kutembea na kulazimika kwenda Hospitalini ambako alipata matibabu na kulazimishwa na dactari mapunziko ya kutosha.

Kutokana na kauli yake mwenyewe msanii huyo, amekuwa kwa muda mrefu katika shughuli za muziki bila kupata mapumzumziko ya muda mrefu.


Kwa sasa ameendelea kusema afya yake inaendelea kuimarika, na ametumia fursa hii kutowa shukrani za dhati kwa wale wote waliokwenda kumjulia hali wakati alipokuwa kitandani.


Maisha Mustafa ni mmoja kati ya wasanii wa Burundi wanaopiga Muziki kwa kutumia Band na wakati huu yupo katika harakati za kuandaa Album yake ambayo hata hivo amesema atatangaza jina wakati muafaka.


Nasi hatuna budi kumtakia afya njema na kurejea katika hali yake ya kawaida