Ijumaa, 22 Machi 2013

CLIP VIDEO YA WIMBO "BIRABABAJE" IPO TAYARI

Clip Video ya Wimbo uliotengenezwa na kampuni ya Ikoh Multiservice ilioshirikiana na Amical des musiciens du Burundi, unaotoa pole kwa wafanyanyabiashara na raia wa kawaida waliopoteza mali zao katika soko kuu la jijini Bujumbura umefikia kwenye hatuwa za mwisho na hivi karibuni utakuwa tayari.

Geraman Producer wa Video Kampuni ya Ikoh Multiservice
Kulingana na Meneja wa kampuni ya Ikoh Multiservice Abdallah The Carter, wimbo huo umekamilika, kinacho baki ni Producer wa Video Geraman, anajaribu kuupitia kwa hatuwa ya mwisho kabla ya kuuachia. Carter ameendelea kuwa watahakikisha wimbo huo unatoka katika mandhari ya kuridhisha Afrika mashariki nzima na kati.

Akizungumza kuhusu kuchelewa kukamilika kwa video hiyo, Manaja The Carter amesema kulikuwa na muingiliano wa kazi nyingi kwa pamoja, na kazi ya video hii ilitakiwa kutengenezwa kwa umakani na istadi wa hali juu, lakini kwa sasa mambo yote yapo tayari picha zimekusanywa na kuungwa kinachobaki ni kuupitia kabla ya kuuachia.

Tarehe 27 Januari mwaka huu, soko kuu la jijini Bujumbura lilitekeketea kwa moto mapema asubuhi ambapo mali na vitu vilivyokuwemo viliteketea wengi wakajikuta wamepoteza mali zao huku wengine wakipoteza fahamu kufuatia hasara walizozipata, kuna hata waliopoteza maisha katika tukio hilo mbaya kuwahi kutokea jijini kati Bujumbura.

katika hali ya kuwafaraji waathirika wa soko hilo, Kampuni ya Ikoh Multiservice iliungana na wasanii pamoja na Amical des Musiciens du Burundi katika kutowa ujumbe wa pole.

Wimbo huo uliwashirikisha wasanii zaidi ya 20 wa Burundi waliojiunga kwa pamoja kuzipeleka salam za rambi rambi kwa wananchi wa Burundi.

wasanii walioshiriki katika wimbo huo ni pamoja na:

Chorus : Rally Joe, John, Florence & Olga

Verse 1 : Rally Joe, John, Shazi kool, Steven Sogo,

Verse 2 : Serge Nkurunziza, Gitero Lax, Alan (Djafris Boyz), Alpha (Divine Glory)

Verse 3 : Chanella, Silas Damara, Lolilo, R Flow, Albert Nkulu, Black G, Mkombozi, Yvan

Bridge : Fabrice (Divine Glory), Patient.