Ijumaa, 29 Machi 2013
HALI YA KUTOELEWANA BAINA YA WASANII WA MUZIKI WA KARAOKE NA UTAWALA
Mnamo siku zote hizi za nyuma, Kuna hali ya kutoelewana kati
ya wasanii wa muziki, hasa wale wanaodumbwiza kwa kutumia muziki wa bendi Ama
Karaoke katika kuwaburudisha wapenzi wa
muziki kwenye kumbi mbalimbali za
starehe na Hoteli pamoja na utawala ambapo kuna sheria inayodaiwa kutolewa na
ofisi ya mea wa jiji la Bujumbura ya kukataza shughuli za muziki zaidi ya saa
mbili usiku.
Kulingana na duru hii sheria amri hii imechukuliwa kufuatia kero
za wananchi waliokaribu na kumbi mbalimbali za starehe ambao wanasema
kukerahishwa na muziki wakati wa usiku ambapo ni wa kupumzika.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa sanaa kwenye wizara ya vijana
michezo na utamaduni Denis Nishirimbere, waziri wa vijana michezo na utamaduni
hajapewa taarifa yoyote kuhusu hatuwa hii ya kuwakataza wasanii wa muziki
kuburudisha zaidi ya saa mbili usiku.
Denis Nshimirimana amefahami sha kwamba kwas asa anasubiri
idhni ya waziri ili aweze kuendesha mkutano maalum kwa dhamira ya kulitafutia
ufumbuzi swala hili.
Baadhi ya wasanii wamejikuta wakikumbwa na amri hii ambayo
hata hivyo wanasema imetolewa na ofisi ya mea wa jiji la Bjumbura ili
kuwakandamiza wengi wao ambao wanaeshi kwa kutegemea kipato wanachokipata baada
ya kucheza muziki huo’Karaoke’
Wasanii waliozungumza na Ikoh Biz, wamesema sheria hii haina
nafasi wakati huu Burundi Usalama na amani vinatawala katika maeneo yote ya
nchi.
Jumatano, 27 Machi 2013
HALI YA AFYA YA MSANII MAISHA MUSTAPHA YAIMARIKA
Msanii nguli wa miondoko
mchanganyiko ambae pia ni mtengenezaji wa muziki "Producer" Maisha Mustapha, aliewahi kutamba na vibao vyake "Cikangali Kachi", "mama" na vingine, afya yake yaimarika baada ya kuripotiwa
kuwa mgogoro siku za nyuma kutokan na kupata maumivu ya mwili
alioyachukulia kuwa ya kawaida, lakini baadae, hali ilizidi
kuwa mbaya zaidi na kujikuta hawezi kutoka chini.
Akizungumza na Ikoh Biz, Maisha
Mustapha amesema hali yake ya afya ilianza kudhohofika pale alipoanza kusikia udhaifu wa mwili na kulichukulia kuwa
hali ya kawaida lakini baadae alishituka pale alipo amka na kujiskia
hawezi kutembea na kulazimika kwenda Hospitalini ambako alipata matibabu na kulazimishwa na dactari mapunziko ya kutosha.
Kutokana na kauli yake mwenyewe msanii
huyo, amekuwa kwa muda mrefu katika shughuli za muziki bila kupata
mapumzumziko ya muda mrefu.
Kwa sasa ameendelea kusema afya yake
inaendelea kuimarika, na ametumia fursa hii kutowa shukrani za dhati
kwa wale wote waliokwenda kumjulia hali wakati alipokuwa kitandani.
Maisha Mustafa ni mmoja kati ya wasanii
wa Burundi wanaopiga Muziki kwa kutumia Band na wakati huu yupo
katika harakati za kuandaa Album yake ambayo hata hivo amesema
atatangaza jina wakati muafaka.
Nasi hatuna budi kumtakia afya njema
na kurejea katika hali yake ya kawaida
Ijumaa, 22 Machi 2013
BOTCHOUM PRO, PRODUCER ASIE CHAKAA
Utakuwa ni ukosefu wa fadhila iwapo utauzungumzia muziki wa kizazi kipya nchini Burundi bila kutaja jina la Producer Botchoum Pro, aliejizolea sifa tele katika kuandaa na kutengeneza muzizi wa wasanii wengi wa kizazi kipya walioibuka miaka ya 90 na kuanza kuonyesha makeke kwenye tasnia hii ya Muziki ambayo ilianza kitambo tu, na Wasanii waliobeba majina makubwa kama vile akina hayati Chanjo Amisi, Christophe Matata, Afrika Nova Bahaga Prosper na wengine ambao waliwavutia sana wapenzi wa muziki wa Burundi katika zama hizo.
Kwa jina halisi ni Kwizera Freddy Khaled maharufu kama Botchoum alianza kucheza muziki kama Disc Joker ama DJ na baadae kuwa muandalizi wa Muziki kwenye Studio ya kwanza aliko anzia Felix Music iliokuwa chini ya mkono wa Felix Music aliekuwa DJ katika Club Archipel mwaka 2003.
Akiwa Feliz Music aliweza kutengeneza nyimbo za wasanii wengi chipukizi walioibukia tasnia ya muziki wa kizazi ambao leo wamejijengea majina na wengine waliaomuwa kuondoka kwenye game la muziki.
Akilonga na Ikoh Biz Botchum amesema kwamba katika kipindi hiki tayari amepata mafaanikio makubwa lakini pia amekuwa akikutana na misukosuko ambayo ni kawaida katika kila nyanja ya maisha kukumbana na mauzauza.
Botchoum amesema kwamba ndoto yake kubwa ni kujiimarisha zaidi katika kazi yake, ili siku moja aweze kufanya kazi na wasanii wakubwa Dunia.
Kwa sasa Botchoum amesema anatulia kwenye Studio ya Kampuni ya Ikoh Multiservice kuhakikisha anainuwa wasanii wengi ambao wanania ya dhati ya kusonga mbele kwenye kwenye tasnia hii ya Muziki ambayo amesema inahitaji bidii ya kutosha na nguvu za ziada ili kuendelea kuwepo kwenye muziki.
Botchum Pro |
Kwa jina halisi ni Kwizera Freddy Khaled maharufu kama Botchoum alianza kucheza muziki kama Disc Joker ama DJ na baadae kuwa muandalizi wa Muziki kwenye Studio ya kwanza aliko anzia Felix Music iliokuwa chini ya mkono wa Felix Music aliekuwa DJ katika Club Archipel mwaka 2003.
Akiwa Feliz Music aliweza kutengeneza nyimbo za wasanii wengi chipukizi walioibukia tasnia ya muziki wa kizazi ambao leo wamejijengea majina na wengine waliaomuwa kuondoka kwenye game la muziki.
Akilonga na Ikoh Biz Botchum amesema kwamba katika kipindi hiki tayari amepata mafaanikio makubwa lakini pia amekuwa akikutana na misukosuko ambayo ni kawaida katika kila nyanja ya maisha kukumbana na mauzauza.
Botchoum amesema kwamba ndoto yake kubwa ni kujiimarisha zaidi katika kazi yake, ili siku moja aweze kufanya kazi na wasanii wakubwa Dunia.
Kwa sasa Botchoum amesema anatulia kwenye Studio ya Kampuni ya Ikoh Multiservice kuhakikisha anainuwa wasanii wengi ambao wanania ya dhati ya kusonga mbele kwenye kwenye tasnia hii ya Muziki ambayo amesema inahitaji bidii ya kutosha na nguvu za ziada ili kuendelea kuwepo kwenye muziki.
CLIP VIDEO YA WIMBO "BIRABABAJE" IPO TAYARI
Clip Video ya Wimbo uliotengenezwa na kampuni ya Ikoh Multiservice ilioshirikiana na Amical des musiciens du Burundi, unaotoa pole kwa wafanyanyabiashara na raia wa kawaida waliopoteza mali zao katika soko kuu la jijini Bujumbura umefikia kwenye hatuwa za mwisho na hivi karibuni utakuwa tayari.
Geraman Producer wa Video Kampuni ya Ikoh Multiservice |
Kulingana na Meneja wa kampuni ya Ikoh Multiservice Abdallah The Carter, wimbo huo umekamilika, kinacho baki ni Producer wa Video Geraman, anajaribu kuupitia kwa hatuwa ya mwisho kabla ya kuuachia. Carter ameendelea kuwa watahakikisha wimbo huo unatoka katika mandhari ya kuridhisha Afrika mashariki nzima na kati.
Akizungumza kuhusu kuchelewa kukamilika kwa video hiyo, Manaja The Carter amesema kulikuwa na muingiliano wa kazi nyingi kwa pamoja, na kazi ya video hii ilitakiwa kutengenezwa kwa umakani na istadi wa hali juu, lakini kwa sasa mambo yote yapo tayari picha zimekusanywa na kuungwa kinachobaki ni kuupitia kabla ya kuuachia.
Tarehe 27 Januari mwaka huu, soko kuu la jijini Bujumbura lilitekeketea kwa moto mapema asubuhi ambapo mali na vitu vilivyokuwemo viliteketea wengi wakajikuta wamepoteza mali zao huku wengine wakipoteza fahamu kufuatia hasara walizozipata, kuna hata waliopoteza maisha katika tukio hilo mbaya kuwahi kutokea jijini kati Bujumbura.
katika hali ya kuwafaraji waathirika wa soko hilo, Kampuni ya Ikoh Multiservice iliungana na wasanii pamoja na Amical des Musiciens du Burundi katika kutowa ujumbe wa pole.
Wimbo huo uliwashirikisha wasanii zaidi ya 20 wa Burundi waliojiunga kwa pamoja kuzipeleka salam za rambi rambi kwa wananchi wa Burundi.
wasanii walioshiriki katika wimbo huo ni pamoja na:
Chorus : Rally Joe, John, Florence & Olga
Verse 1 : Rally Joe, John, Shazi kool, Steven Sogo,
Verse 2 : Serge Nkurunziza, Gitero Lax, Alan (Djafris Boyz), Alpha (Divine Glory)
Verse 3 : Chanella, Silas Damara, Lolilo, R Flow, Albert Nkulu, Black G, Mkombozi, Yvan
Bridge : Fabrice (Divine Glory), Patient.