Jumatatu, 30 Septemba 2013

JAY FERNANDO ATOWA SHUKRANI ZA DHATI KWA WALIOJITOKEZA KATIKA SHEREHE YAKE YA BIRTHDAY


Msanii wa Burundi mwenye makaazi yake huko Ulaya, Jay Fernando wakati akiadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake alikusanyika pamoja na wapenzi mbalimbali huko Brusels kwa ajili ya Birthday hiyo.

Mambo ya mduara pia yalikuwepo
Ametowa shukrani za dhati kwa wale wote waliochangia kwa njia moja ama nyingine katika kufaanikisha sherehe hiyo iliofana baaada ya kuhudhuriwa na watu kutoka katika maeneo tofauti.
Wakati wa kuserebuka




Jumamosi, 28 Septemba 2013

MR HAPPY AENDELEA KUTANUA JIJINI NAIROBI BAADA YA KURIKODI NYIMBO ZAKE MBILI

Mr Happy akiwa na mwenyeji wake Jaguar
Kwa Mujibu wa taarifa kutoka jijini Nairobi msanii wa Burundi Mr Happy ama Happy Famba tayari amekwisha rikodi nyimbo zake mbili katika studio za Ogopa DJ.
Mr Happy akiwa nyumbani kwa mwenyeji wake Jaguar

Wakati wakipata lunch

Gari analo tembelea Jaguar

Mr Happy akiwa Studio za Ogopa DJ
Mr Happy akijifua kidogo kabla ya kuingia Studio
 


Ijumaa, 20 Septemba 2013

MR HAPPY FAMBA APEWA SHAVU YA KURIKODI SINGLE 2 NA OGOPA DJ NCHINI KENYA JUMA LIJALO


Msanii mwenye makeke katika jiji la Bujumbura ambaye amejijengea sifa tele kupitia style yake ya kuimba na kucheza, Mr Happy Famba, amepewa shavu na kampuni ya Show Bizz East Africa ya kwenda ku rikodi single zake mbili nchini Kenya.

Ogopa DJ ni moja miongoni mwa kampuni zinazo sifika Afrikari Mashariki kwa ustadi na uwezo wake wa hali ya juu wa kurikodi na kutengeneza Video. Wasanii kutoka katika mataifa mbalimbali Afrika Mashariki na kati wamekuwa na ndoto ya kutaka kufanya kazi na Kampuni hiyo



Kulingana na taarifa kutoka kwa msaniii huyo, Juma lijalo atakuwa nchini Kenya, kwa sasa mipango yote imekamilika, unasubiriwa muda tu wa safari, na utapo wadia atakuwa Nairobi nchini Kenya.

Mr Happy ameiambia ikoh.biz kwamba Katika single hizo mbili, moja itakuja kwa jina Happy Birthday ambayo atashirikina na msani nguli wa Kenya Jaguar, huku nyingine atamshkirikisha msanii mwingine wa nchini humo Nameless.

Mr Happy Famba ni mmoja kati ya wasanii wasio kosa katika tamasha za kitaifa na za kimataifa ambazo hufanyika jijini Bujumbura, na hii ni kutokana na umaharufu mkubwa aliojijengea sio tu kwa kuwa msanii lakini kuwa miongoni mwa watu wanaotowa plani na kupanga mipango ya kufaanisha tamasha hizo.

Kwa sasa amekuwa katika harakati za kurikodi video ya wimbo wake Baby Girl ambao alimshirikisha msanii mwenziye, ukiwa ni moja miongoni mwa nyimbo zinazo vutia wapenzi wa mtindo wa Afro-zouk jijini Bujumbura.

Kinachosubiriwa kwa sasa ni je fursa hii ataitumia vipi msanii huyu?

ikoh.biz tunamtakia kila la kheri.

Alhamisi, 19 Septemba 2013

KUNDI LA WAKALI POWER LAFUFUKA, LAPEWA SHAVU BONDENI KWA MANDELA

Jay Kizo
Kulingana na taarifa kutoka kwa Jay Kizo mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi hilo la wakali Power ambalo liliwahi kuwa kivutio kikubwa sana na kichocheo katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini Burundi, limefufuka na kupata mualiko wa kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya Burudani, lakini pia kupanga mikakati ya ku shoot video ya wimbo wao "Usiskie Corus" uliojipatia sifa tele jijini Bujumbura miaka ya nyuma mithili ya kugeuka wimbo wa taifa.
Black G

Akizungmza na Ikoh.Biz kutoka Ufaransa ambako amejichimbia makaazi, Jay Kizzo amesema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha safari hiyo inafana, kwa sasa amesema yeye yupo Ufaransa, Black G na Marechal Fyiroko Diriri wapo Bujumbura, huku D.Rop akiwa nchini Tanzania, watakutana wote nchini Afrika Kusini katika miezi miwili ijayo.
Marechal Fyiroko
Akiulizwa kuhusu ukimya wa muda mrefu, Jay Kizo amesema kwa sasa kila mmoja anatafuta maisha kwa upande wake, lakini haijamaanisha kwamba kundi limekufa, kwa sasa tunajipanga kuelekea nchini Afrika Kusini ambako mbali na kutowa Burudani, tutarikodi pia nyimbo zetu mbili, moja inaitwa Najuwa,  ameendelea kuwa kwa sasa D.Rop yupo Tanzania ambapo ametengeneza wimbo na Msanii wa Bongo T.I.D,  mimi nipo Ufaransa, wengine wapo Bujumbura, tunakwenda huko Afrika Kusini kwa mualiko wa Warundi waishio huko bondeni kwa ushirikiano mkubwa wa Keshy Video Lab ltd.























Akijhojiwa na Ikoh.biz, mwenyekiti wa kampuni ya Keshy Video lab ltd, Abdoul, amethibitisha taarifa na kuongeza kwamba kwa sasa taratibu za maandalizi zimeanza, na zitapo kamilika ndipo wataweka bayana kila kitu.

Ikoh.biz hatuna budi kuwatakia kila la kheri.

Jumatano, 18 Septemba 2013

SKENDO YA MADAWA YA KULEVYA YAWASABABISHIA USUMBUFU WASANII WA BONGO FLEVA

Kutokana na wasanii wa Bongo kukumbwa na skendo ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, wasanii Shetta na Chege ambao walikuwa wanasafiri kuelekea nje ya nchi yao na kutakiwa na idara ya upekuzi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalim Jilius Kambarage Nyerere, kupekuwa kila kilichokuwa ndani ya begi zao kama inavyoonyesha picha hiyo.

Biashara hii ya madawa ya kulevya imekuwa ikiichafulia jina nchi ya Tanzania baada ya raia wa Tanzania kukamatwa katika nchi mbalimbali duniani wakijihusisha na biashara hii haramu ya madawa ya kulevya.

AMISI TAMBWE MSHAMBULIAJI WA KIMATAIFA KUTOKA BURUNDI APACHIKA MANNE, SIMBA 6 MUGAMBO 0

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi Amisi Tambwe ambaye anakipiga katika Klabu ya Simba SC, maharufu kama wekundi wa Msimbazi ya jijini Dar Es salaam, amepachika mabao yake matatu katika mchezo wa Simba na Mugambo. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza mshambuliaji huyo aliye sajiliwa hivi karibuni kutoka katika klabu ya Vital'o ya Burundi anapachika bao katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom. Simba imeitamdika Mugambo mabao 6-0, huku mshambuliaji Chanogo akisaidia kusindiria msumari na kuipa simba mabao mawili.

Watani wao wajadi Yanga SC ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi hiyo wametoka sare ya bao 1-1 na Prisons. 

Neno Burundi, Mrundi linatajwa sana leo jijini Dar Es Salaam katika vyombo vya habari nchini Tanzania.

BAO LA 200 LA WAYNE ROONEY AKIWA NA MASHETANI WEKUNDU


Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United ambae alitajwa kuwa ataondoka msimu wa baridi uliopita Wayne Rooney mwenye umri wa miaka 27 ambaye tayari amecheza mechi moja na kufunga mabao 2 katika mechi ya daraja la kwanza na ambaye aliamuwa kusalia katika klabu yake ya Manchester United.








Hili ni moja miongoni mwa mambo yanayo mpa furaha kubwa kocha wa klabu hiyo David Moyes na mashabiki wa Klabu hiyo.

Ronney alifaulu kupachika nyavuni mabao 2 katika mechi ya klabu bingwa barani Ulaya iliopigwa jana wakati wa mpambano wao na Bayern Leverkusen na kuandika historia ya kutimiza mabao 200 akiwa na klabu hiyo ya mashetani wekundu.

Wachezaji watatu pekee ndio ambao wanarikodi hiyo katika klabu hiyo ikiwa ni pamoja na Jack Rowley alitimiza mabao 211 Denis Law mabao 237 pamoja na Bobby Charlton aliefikisha mabao 249.

Wakati huo huo mshambuliaji mwingine wa klabu hiyo Robert Van Persie amesema anafurahia sana kucheza pamoja na Rooney kwa kuwa anajuwa kusaka mpira na unauwezo wa kucheza mipira mifupi na mirefu.

Matamshi ambayo yamempa matumaini makubwa kocha wa Manchester Unites David Moyes.

IKER CASILLAS AREJEA UWANJANI NA KUONDOKA KATIKA DAKIKA YA 15 BAADA YA KUPATA JERAHA

Golkipa Number 1 wa Klabu ya Real Madrid Iker Casillas ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa kipindi kadhaa na ambaye Kocha wa Klabu hiyo aliamuwa kumpa nafasi katika mechi baina ya Real Madrid na Galatasaray ya Uturuki, aliondolewa nje ya uwanja katika dakika ya 15 baada ya kugongana na mchezaji mwenzake Sergio Ramos. Casillas alionekana mwenye huzuni sana wakati anaondoka uwanjani. Hata hivo hana kinyongo na Ramos kama jinsi picha inavyoonyesha na ambayo aliweka kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter na kusindikiza na maneno: Kuna mtu anataka kuniuwa leo. Real Madrid ilishinda mechi hiyo kwa mabao 6-1

Ijumaa, 13 Septemba 2013

MSANII WA BURUNDI T.MAX NA ZIARA YAKE YA DUBAI


Msanii wa Burundi wa miondoko ya Hip Hop mzee wa michano, T. Max, amewasiliji mjini Dubai katika mji Deira hapo jana Alhamisi kwa ajili ya maamdalizi ya album video yake mpya itayo beba takriban nyimbo kumi. Bila shaka, mengi zaidi utayapata kupitia hapa.


Ijumaa, 6 Septemba 2013

MA RAIS PAUL KAGAME WA RWANDA NA JAKAYA MRISHO KIKWETE WAZUNGUMZA FARAGHANI

Asikudanganye mtu kwamba anafahamu walichokuwa wakitetea viongozi hawa wakati wakielekea kwenye mazungumzo yao ya faragha na hakuna anayejua walichozungumza. Baada ya shughuli za upigaji picha kama uonavyo, waandishi wa habari tupisheni tuzungumze yetu.







Jumatano, 4 Septemba 2013

YOUSOU NDOUR WAZIRI WA UTALII NCHINI SENEGAL ATUPWA NJE KATIKA SERIKALI

Waziri wa Utalii nchini Senegal Yousou Ndour ambaye pia ni msanii wa muda mrefu atupwa nje katika serikali baada yua kuhudumu kwenye uadhifa huo tangu pale rais Macky Sall alipochukuwa hatamu ya uongozi wa taifa hilo.

Mwishoni mwa juma lililopita rais Macky Salla alimfuta kazi waziri wake mkuu Abdoul Mbaye na kumteuwa Aminata Toure kwwnye uadhifa huo. mawaziri 7 wa serikali iliopita waliondolewa huku wengine wakipewa nafasi ya kuendelea kuhudumu licha ya kubadilishwa wizara.

KUNDI LA BLACK'S POWER KUTOKA BUKAVU LIPO JIKONI KUPIKA ALBUM YAO YA KWANZA


Vijana wa kundi la Black's Power lenye maskani yake mjini Bukavu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika Mkoa wa Kivu ya Kusini, wameingia studioni kwa ajili ya kurikodi album yao ya kwanza, baada ya kuwa na Track nyingi ambazo wamezitowa kwa nyakati tofauti.

Blacks power wakiwa kazini

Kundi hilo lemye kuundwa na watu kumi ambalo limekuwa likihamasisha vijana dhidi ya ukimwi katika eneo hilo, limekuwa likiandaa tamasha hadharani mara moja kwa miezi miwili chini ya ufadhili wa shirika la AFRICANS ARTISTS FOR DEVELOPMENT (AAD) lenye makao yake makuu nchini Ufaransa.

kwa mujibu wa kiongozi wa kundi hilo Kanyurhi Mpfree, Album  hiyo ya kwanza ya kundi hilo itabebe nyimbo zenye ujumbe wa kuhamasisha vijana na watu wazima kujilinda dhidi ya ukimwi ambao umekuwa tushio kubwa sana duniani.

Mbali na shirika la ADD linalotowa mchango katika shughuli hizo za uhamasishaji wa vijana kujilinda dhidi ya Ukimwi, shirika la SOS Sida  nalo linachangia kuhakikisha Album hiyo inakamilika.

wasanii wa kundi hilo wamekuwa wakitowa burudani katika tasnia ya filamu zenye mafunzo dhidi ya ukimwi.



CHANY QUEEN NA R.FLOW KWISH NEHI

Mashabiki wa wasanii wa kundi la The Cousins wamepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kuvunjika kwa mahusiano kati ya Msanii wa Kike nchini Burundi mwenye sauti ya aina yake Chany Queen na mpenzi wake R.Flow baada ya kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu.


Gitare Chanel Maharufu kama Chany Queen, amesema licha ya kuachana na mpenzi wake R.Flow, bado atasalia kuwa katika kundi walioanzisha wakiwa pamoja la "The Cousins" na kuongeza kuwa hana mtima nyongo na mpenzi wake huyo, bali amechukuwa maamuzi hayo baada ya kushindwa kuendelea kuvumilia masharti.

Akiweka wazi moja miongoni mwa sababu zilizo mfanya kuachana na mpenzi wake, ni kuwa yeye anatumia pombe na ni mtu wa kwenda out, na ku enjoy na kujichanganya na watu mbalimbali, jambo ambalo mpenzi wake hapendi na hatumii pombe.

Mbali na kuwa msanii wa kuimba, Chany Queen ni msanii pia wa maigizo na tayari aliwahi kuigiza filamu na wasanii wa bongo Movies, filamu iliokuja kwa jina la "Chupa Nyeusi" Filamu ambayo ilifanya vizuri, wadadisi wa mambo wanasema kwamba fursa hii aliyo pewa alishindwa kuitumia wakati huo ndio ulikuwa mwanzo wa kutoka.

Juhudi zetu za kumtafuta R.Flow juu ya kutaka kujuwa undani zaidi kuhusu taarifa hii, ziliambulia patupu baada ya sim yake kutopatikana.




NANI ALIYE COPY KWA MWENZIYE KATI YA DIAMOND NA MR FLAVOUR

Mr Flavour

Diamond Platnumz

Sina mengi zaidi ya kukupa nafasi ya kuangalia Video hizi mbili na kusikiliza beat, mwenyewe utajuwa nani ka copy mwenziye. Angalia na sikiliza hatuwa kwa hatuwa tena kwa umakini mwisho utajuwa na kuelewa kinachoendelea.



Jumanne, 3 Septemba 2013

HAMISI TAMBWE ANG'ARA KATIKA MECHI YA UTAMBULISHO WAKE KATIKA KLABU YA SIMBA, APACHIKA MAWILI


 Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka nchini Burundi Amisi Tambwe ambaye alisajiliwa hivi karibuni na klabu ya Simba Sports Club akitokea katika Klabu ya Vital'o Football Club ya jijini Bujumbura ameng'ara katika mchezo wa kirafiki baina ya Simba na Mafunzo ya Huko Zanzibar, kwenye uwanja wa Taifa hapo jana jiji Dar Es Salaam nchini Tanzania.

Amisi Tambwe amefunga mabao mawili kati ushindi wa 4-3 dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.

Mbali na kufunga mabao mawili, Tambwe pia alitowa pasi nzuri iliofaanikisha kupatikana kwa bao la pili la mchezo ikiwa ni salam kwa viongozi wa  Simba SC kwamba hawakukosea kumsajili.

Mchezaji huyo kutoka Vital'o ya Burundi na mfungaji bora wa klabu Afrika Mashariki na katika kombe la Kagame mwaka huu lililopigwa huko Sudan, aling'ara katika mchezo huo sawa na beki Kaze Gilbert waliyesajiliwa pamoja wote kutoka Vital'o.