Jumatano, 20 Julai 2022

VIONGOZI WA EAC KUKUTANA MJINI ARUSHA JULAI 21 NA 22 MWAKA 2022


 Viongozi wa nchi 7 zinazounda Jumuoiya ya Afrika mashariki EAC wanakutana kesjho na kesho kutwa mjini Arusha nchini Tanzania katika mkutano wa 22 wa kawaida wa wakuu hao kwenye makao makuu ya Jumuiya hiyo. Awali viongozi hao walikutana katika vikao vilivyofanyika kwa njia ya mtadao.


TAIFA STARS YA TANZANIA YASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI YALAZIMISHWA SARE NA ZIMBABWE


Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imetoka sare ya bila kufungana na timu ya Taifa ya Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa iliyopo katika kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la mpira wa miguu (FIFA), iliyopigwa jana jumanne kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Tanzani, Kim Poulsen, alilalamikiwa na mashabiki waliohudhuria mechi hiyo, kwa kushindwa kufanya marekebisho ya wachezaji walioshindwa kumudu mchezo.
Hata hivyo, Kipa Ivo Mapunda ambaye kwa muda mrefu hajaitumikia Taifa Stars alionekana kufanya vizuri langoni kwake na kuinusuru Stars kufungwa.

Kwa upande wake Zimbabwe ilitumia wachezaji wengi chipukizi huku Taifa Stars ikiwatumia wachezaji watano wanaocheza soka la nje ya nchi.
Awali Taifa Stars ilitakiwa kucheza na Harambee Stars ya Kenya, lakini Shirikisho la soka nchini Kenya FKF lilituma taarifa likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.