Ijumaa, 23 Februari 2018

HASIRA YA TAWALA MJINI DAPCHI SIKU 4 BAADA YA KUTOWEKA KWA WASICHANA 111Lai Mohammed

Lai Mohammed Waziri wa habari nchini Nigeria
Siku nne baada ya kutokea kwa shambulio katika shule moja mjini Dapchi nchini Nigeria, kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika mji huo uliopo kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako vikosi vya usalama vimekabiliana na wananchi wenye hasira ambao hadi sasa hawajuwi wapi walipo binti zao.

Polisi imethibitisha kuwa wasichana 111 wa shule la wasichana mjini Dapchi wametoweka tangu kutokea kwa shambulio la kundi la kijihadi la Boko Haram

hofu imeendelea kutanda katika eneo hilo ikihofiwa kutokea kwa Chibok mpya, jimbo lililopo jirani na mji wa Borno ambako kundi la Boko Haram liliwateka wasichana 276 April mwaka 2014, tukio lililolaaniwa ulimwengu mzima.

Waziri wa ulinzi nchini Nigeria Jenerali Mansour Dan Ali amesema wasichana wengi walikimbia kutokana na uoga na baadhi wameanza kurejea shuleni.


RAIS WA MAHAKAMA YA RUFAA YA GITEGA NA JAJI, WATIWA KOROKORONI

Thomas Ntimpirangeza,
Thomas Ntimpirangeza, rais wa Mahakama ya rufaa mjini Gitega na Prime Habiyambere, jaji katika mahakama hiyo, wametiwa nguvuni hivi majuzi kufuatia waranti ya kukamatwa kwao kutoka kwa hakimu mkuu wa jamuhuri.

Wawili hao walikamatwa kwa nyakati tofauti, ambapo mmoja alikamatwa ofisini kwake huko Gitega, huku mwingine akikamatwa akiwa ziarani jijini Bujumbura. Wote wawili kwa sasa wamewekwa korokoroni katika jela kuu la Mpimba.

Taarifa za awali zilieleza kwamba wawili hao walikamatwa baada ya kumuacha huru mshukiwa wa wizi wa dheruji ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu, ambapo ilikuwa ni msaada kutoka Ikulu ya Rais.

Huku habari nyingine zikieleza kwamba rais Mahakama ya rufaa alikamatwa baada ya kurusha kwenye mitandasno ya kijamii kampeni ya kura ya hapana katika uchaguzi wa kura ya maoni ujao nchini Burundi.


Hata hivyo hakimu mkuu wa Jamuhuri Sylvestre Nyandwi anasema wawili hao wamekamatwa kwa makosa ya Rushwa huku akikanusha taarifa kwamba wawili gao wamekamatwa kutokana na kuendesha kampeni ya hapana.