Lai Mohammed Waziri wa habari nchini Nigeria |
Siku
nne baada ya kutokea kwa shambulio katika shule moja mjini Dapchi
nchini Nigeria, kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika mji huo uliopo
kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako vikosi vya usalama
vimekabiliana na wananchi wenye hasira ambao hadi sasa hawajuwi wapi
walipo binti zao.
Polisi
imethibitisha kuwa wasichana 111 wa shule la wasichana mjini Dapchi
wametoweka tangu kutokea kwa shambulio la kundi la kijihadi la Boko
Haram
hofu
imeendelea kutanda katika eneo hilo ikihofiwa kutokea kwa Chibok
mpya, jimbo lililopo jirani na mji wa Borno ambako kundi la Boko
Haram liliwateka wasichana 276 April mwaka 2014, tukio lililolaaniwa
ulimwengu mzima.
Waziri
wa ulinzi nchini Nigeria Jenerali Mansour Dan Ali amesema wasichana
wengi walikimbia kutokana na uoga na baadhi wameanza kurejea shuleni.