Jumatatu, 25 Oktoba 2021

JESHI LA SUDAN LAFUTILIA MBALI SERIKALI YA MPITO LAAHIDI KUUNDA BARAZA JIPYA LA UONGOZI


 Mkuu wa bazara la uongozi wa kijeshi nchini Sudan, jenerali Abdel Fattah al Burhan, ametangaza kulivunja bazara hilo na bazara la mawaziri baada ya kutangaza hali ya dharura nchini humo, katika hali ya kutokea kwa mapinduzi ya serikali ya mpito mapema leo.

















Baada ya kukamatwa kwa waziri mkuu na wanajeshi mapema leo, mitandao ya kijamii ilifungwa, wanajeshi wakionekana kushika doria jijini Khartoum, mkuu wa baraza la uongozi nchini humo Abdel Fatta Al Burhan akitangza hali ya dharura nchini humo na kusitisha safari za kimataifa, kutanza kuwa serikali mpya ya mpito itangazwa kubla ya mwisho wa mwezi Novemba.








Serikali ya mpito inayoundwa kati ya raia na Baraza la kijeshi iliundwa mwaka 2019 baada ya kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa muda mlrefu Omar Al Bashir kufuatia maandamano ya wananchi, na ilipaswa kuongoza mpaka 2023 na kupisha Uchaguzi Mkuu.
x
x